Polisi yachoshwa na ujambazi Kimara, Kawe

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
JESHI la Polisi katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema linatarajia kuhamishia nguvu zake za kupambana na wahalifu katika eneo la Kimara na Kawe, kwa kile lilichodai kuchoshwa na vitendo vya ujambazi na mauaji vilivyokithiri katika maeneo hayo.

Kamanda wa Kanda hiyo, Suleiman Kova, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa vitendo vya uhalifu katika maeneo hayo, vimekuwa sugu, hivyo jeshi limeamka na kubuni njia mpya za kukabiliana nazo.

Alisema tofauti na maeneo mengine, Kimara na Kawe ni maeneo yanayoonekana kukithiri kwa vitendo hivyo ambapo imefikia mahali hadi wakazi wa maeneo hayo wamekuwa waoga na kuamua kuyahama ili kuepuka madhara kutoka kwa majambazi hao.

“Nawaambia wananchi wa Kimara na Kawe kuwa wasiyahame maeneo hayo, kwa sasa Polisi wa Kanda zote tatu, Ilala, Kinondoni na Temeke wamejumuishwa ili kuhakikisha maeneo hayo yanakuwa salama sababu tumejishapanga katika kupambana na hali hiyo,” aliongeza Kova.

Katika hatua nyingine, Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Kinondoni, Charles Kenyela, alisema wanawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuhusika na ujambazi na kusababisha mauaji ya Elizabeth Njau (38) mkazi wa Kimara yaliyotokea Desemba 25, mwaka huu.

Alisema watuhumiwa hao waliokamatwa kwa ushirikiano wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, ndio wanaodhaniwa kuwa walihusika na kifo cha mwanamke huyo aliyekuwa muuguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili sambamba na kumjeruhi mumewe, Aminiel Njau (43) na kupora Sh 100,000.

Kenyela alisema dhumuni la watuhumiwa kufanya mauaji hayo, ilikuwa kupora bunduki inayomilikiwa kihalali na Njau ambayo hata hivyo hawakuipata.
 
Tutashukuru likiwa ni ahadi ya kweli. Nilishaanza kufungasha vyombo kuhama Kimara Temboni. Maeneo ya Temboni kushoto na kulia kwa barabara kuu, Kwa Msuguri na Suka ni tishio. Tunaishi tukiwa roho mikononi. Kukicha tunafurahi, jua likianza kuzama tunaogopa hata kurudi majumbani kuhofia majambazi

JESHI la Polisi katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema linatarajia kuhamishia nguvu zake za kupambana na wahalifu katika eneo la Kimara na Kawe, kwa kile lilichodai kuchoshwa na vitendo vya ujambazi na mauaji vilivyokithiri katika maeneo hayo.

Kamanda wa Kanda hiyo, Suleiman Kova, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa vitendo vya uhalifu katika maeneo hayo, vimekuwa sugu, hivyo jeshi limeamka na kubuni njia mpya za kukabiliana nazo.

Alisema tofauti na maeneo mengine, Kimara na Kawe ni maeneo yanayoonekana kukithiri kwa vitendo hivyo ambapo imefikia mahali hadi wakazi wa maeneo hayo wamekuwa waoga na kuamua kuyahama ili kuepuka madhara kutoka kwa majambazi hao.

“Nawaambia wananchi wa Kimara na Kawe kuwa wasiyahame maeneo hayo, kwa sasa Polisi wa Kanda zote tatu, Ilala, Kinondoni na Temeke wamejumuishwa ili kuhakikisha maeneo hayo yanakuwa salama sababu tumejishapanga katika kupambana na hali hiyo,” aliongeza Kova.

Katika hatua nyingine, Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Kinondoni, Charles Kenyela, alisema wanawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuhusika na ujambazi na kusababisha mauaji ya Elizabeth Njau (38) mkazi wa Kimara yaliyotokea Desemba 25, mwaka huu.

Alisema watuhumiwa hao waliokamatwa kwa ushirikiano wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, ndio wanaodhaniwa kuwa walihusika na kifo cha mwanamke huyo aliyekuwa muuguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili sambamba na kumjeruhi mumewe, Aminiel Njau (43) na kupora Sh 100,000.

Kenyela alisema dhumuni la watuhumiwa kufanya mauaji hayo, ilikuwa kupora bunduki inayomilikiwa kihalali na Njau ambayo hata hivyo hawakuipata.
 
Kamanda Kova kauli yako tunategemea itakuwa ya ukweli na ujambazi utapungua maeneo hayo na mengine ya jiji letu la DSM.Vituo vya polisi vinahitajika maeneo mengi mfano. Goba HAKUNA KITUO CHA POLISI na idadi ya watu wanaoishi huko ni kubwa mno hata km ni kuchangia kijengwe waambie watendaji wa mitaa/kata wapite kila nyumba kukusanya mchango kwa ajili ya ujenzi wa vituo kamanda wetu.
Suala la Goba lifanyie kazi tafadhali maana siku kukitokea uvamizi sijui utajitetea vipi wakati hakuna kituo chochote cha polisi huko
 
Huko kimara na temboni nasikia wakina meku wako kibao...duuu kama unga ltd
 
Back
Top Bottom