Polisi wetu tanzania.


taffu69

taffu69

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2007
Messages
2,089
Likes
1
Points
135
taffu69

taffu69

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2007
2,089 1 135
Vijana wetu wa jeshi la polisi mnausikitisha sana umma wa Watanzania. Hivi ni kwa nini mnakubali kutumika ndivyo sivyo. Mnapoamrishwa kuwapiga mabomu raia ambao wamekaa kwa amani na utulivu kwa minajili ya kudai haki ama kuangalia hatima ya kile walichokifanya mnajisikiaje.

Maisha ya polisi kuanzia mishahara, vitendea kazi, malezi ya familia pamoja na makazi vyote ni duni. Mnapata faraja gani mnapowapiga mabomu na virungu wale ambao wamejitolea kutetea haki za wanyonge ambao wengi wenu mnaangukia kwenye kundi hilo?

Mlichofanya Mwanza, Temeke, Arusha, Segerea na kwingineko ni kitendo cha kinyama na inafaa kilaaniwe na jamii nzima, ni lazima mtambue kile mnachofanya ama kutekeleza kina manufaa gani na kwa faida ya nani!
 

Forum statistics

Threads 1,238,812
Members 476,185
Posts 29,331,615