Polisi wetu sasa hii imekuwa too much!

Polisi wetu sasa hii imekuwa too much!

Sio tatizo la IGP bali ni tatizo la yule aliyesema anatamani angekuwa IGP

Sent using Jamii Forums mobile app
It is very true.

Yule jamaa aliyetamka hadharani kuwa I wish I could be IGP, ndiye anayeagiza hii kamatakamata ya wabunge wa Chadema.....

Refer kauli yake alipokuwa akimsifu Spika Ndugai kwa kazi "nzuri" anayofanya kule Bungeni ya kuwatimua wabunge wa upinzani wanaodaiwa ni wakorofi.......

Mkuu wa nchi akamhakikishia Spika Ndugai kuwa yeye Spika atakapomaliza "assignment" yake ya kuwatimua wabunge wa upinzani kule Bungeni, amwachie na yeye huku uraiani ambako atashughilika nao.......

Ukiunganisha dots hapo baada ya kushuhuhudia wabunge Halima Mdee na Esther Bulaya ambao wote walitimuliwa kule Bungeni na baadaye huku "uraiani" nako tayari Mkuu keshatekeleza ahadi yake kwa kuwa tayari wameshashughulikiwa.....
 
It is very true.

Yule jamaa aliyetamka hadharani kuwa I wish I could be IGP, ndiye anayeagiza hii kamatakamata ya wabunge wa Chadema.....

Refer kauli yake alipokuwa akimsifu Spika Ndugai kwa kazi "nzuri" anayofanya kule Bungeni ya kuwatimua wabunge wa upinzani wanaodaiwa ni wakorofi.......

Mkuu wa nchi akamhakikishia Spika Ndugai kuwa yeye Spika atakapomaliza "assignment" yake ya kuwatimua wabunge wa upinzani kule Bungeni, amwachie na yeye huku uraiani ambako atashughilika nao.......

Ukiunganisha dots hapo baada ya kushuhuhudia wabunge Halima Mdee na Esther Bulaya ambao wote walitimuliwa kule Bungeni na baadaye huku "uraiani" nako tayari Mkuu keshatekeleza ahadi yake kwa kuwa tayari wameshashughulikiwa.....
Hayo yanajulikana na kila mtu ila kuna mijitu inapinga hata kama wanaujua ukweli ulivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umaarufu wa kisiasa una gharama zake.

Sioni kama polisi wanafanya kitu cha kinyama sana,maana watu wenyewe huwa wanatoka na kuendelea na shughuli zao.

Au kuna lengo lingine tofauti na kutetea taifa.
 
Hivi sasa nchini kwetu imekuwa ni jambo la kawaida sana kusikia Polisi wamemkamata Mbunge fulani wa upinzani na kumweka ndani Polisi na baadaye kumpeleka mahakamani na kumfungulia mashitaka ya uchochezi.

Hata hivyo sisi wananchi tunaofuatilia kwa karibu siasa za nchi hii tumegundua kuwa kwa kweli Jeshi letu la Polisi linafanya uonevu wa hali ya juu kwa viongozi wa upinzani na tuseme kwa hakika kuwa kwenye nchi yetu kwa sasa viongozi wa vyama vya upinzani wanakuwa treated kama vile ni wahamiaji haramu wa nchi hii na ni kama hawatakiwi kuishi ndani ya nchi hii!

Katika kipindi kisichozidi wiki moja hadi hivi sasa tumeshuhudia wabunge wa upinzani wafuatao wa Chama cha Chadema wakikamatwa na Polisi. Mbunge Esther Bulaya wa Jimbo la Bunda. Mbunge John Heche wa Jimbo la Tarime. Mbunge Tundu Lissu na Mbunge Godbless Lema.

Inashangaza kuona kuwa Polisi wetu wanawawinda na kuwakamata wabunge wa Chadema pekee na kutotaka kabisa kuwagusa wabunge wa CCM katika hayo wanayoyaita makosa ya uchochezi.

Nitatoa mfano mmoja wa wazi kabisa kuonyesha namna gani Polisi wetu wanavyofanya ubaguzi wa hali ya juu katika hiyo kamata kamata yao.

Mbunge wa CCM Mheshimiwa Kingu alienda kwenye Jimbo la Singida Mashariki, Jimbo ambalo Mbunge wake ni Tundu Lissu wa Chadema na kufanya mkutano wa harambee wa kuchangia ujenzi wa shule, Mbunge huyo hakukamatwa na Polisi kwa uchochezi.

Lakini tumeshuhudia majuzi Mbunge wa Chadema wa Jimbo la Bunda, Mheshimiwa Esther Bulaya akifanya "the same thing" kama alichofanya mwenzake wa CCM Mheshimiwa Kingu na kwenda Jimbo la Mbunge mwenzake wa Chadema John Heche wa Jimbo la Tarime kwa lengo la kufanya harambee kwa ajili ya ujenzi wa shule, Polisi walimkamata Mbunge Esther Bulaya na kwenda kumlaza ndani kwenye sero zao za Polisi na wakati wowote kuanzia sasa anaweza kuburuzwa mahakamani na kusomewa mashitaka ya kufanya uchochezi!

Nipende tu kuwakumbusha Polisi wetu kuwa nchi yetu ipo kwenye mfumo wa vyama vingi na kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 3(1) inasema hivi "Nchi yetu itakuwa kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa na vyama hivyo katika uendeshaji wa shughuli zao hakutakuwa na chombo chochote kitakachokuwa na mamlaka ya kuingilia shughuli za vyama hivyo" mwisho wa kunukuu.

Sasa niwaulize Polisi wetu iwapo mnafanya kazi zenu kwa weledi na kwa namna taaluma zenu zimavyowahitaji kutekeleza majukumu yenu ni kwanini basi mnaivunja Katiba ya nchi yetu waziwazi inayosema nchi yetu ni ya vyama vingi na mnawatreat viongozi wa vyama vya upinzani kama siyo raia wa nchi hii na ni kama vile wahamiaji haramu?

Mkumbuke pia Polisi kuwa hata kama hayo mnayoyafanya ni maagizo toka juu lakini mkumbuke ule msemo unaosema ya kuambiwa changanya na akili yako......

In case mambo yataharibika hapa nchini huyo aliye juu anayewatuma kufanya maovu hayo hatapandishwa kizimbani kwa kuwa anayo kinga ya kutoshitakiwa, ni nyinyi wenyewe as individuals mtakaoburuzwa mahakamani na majaji watakaosikiliza kesi zenu haewatachukulia Kama utetezi mtakapowaambia kuwa huyo maovu mliyokuwa mnayafanya yalikuwa maelekezo toka juu.....

Mwenyezi masikio na ausikie ujumbe huu muhimu.
halafu wababe wa Kibiti wakiwafanyizia wanaanza kulialia!

nina hofu tunakoelekea tunaweza fika mahali kukawepo kuwindana kama nyau na panya kati ya raia na polisi!
 
Tumetumwa na nani?

Jibu hoja, je ni kwanini Jeshi letu la Polisi wamekuwa na kazi moja tu ya kuwawinda wabunge wa Chadema na kuwakamata na kuwafungulia mashitaka ya "kubambika"yasiyo na kichwa wala miguu?
Kwa sababu wabunge wa Chadema wanajifanya "Hamnazo"
 
Polisi waacheni maana watakufa tu kwani hawataishi milele
 
Sio wa kuwalaumu wao ni watii amri,unapokea amri unapiga saluti unageuka nyuma unatekeleza. Ila lawama ubebeshwa wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini Polisi wetu lazima wazingatie ule msemo wa la kuambiwa changanya na akili zako.....

Iwapo wataendelea kupokea maagizo toka juu hata yale ambayo siyo halali, wajue likitokea la kutokea, wasitegemee kuwa kwenye mahakama watatoa utetezi kuwa tulifanya maovu hayo kutokana na maagizo toka juu.......

Majaji/Mahakimu nao watawauliza maswali yafuatayo:-

1. Je nyinyi mnafanya kazi kwa mujibu wa Katiba ya nchi na sheria nyinginezo za nchi hii au kutokana na maelekezo toka juu?

2. Je nyinyi mnafanya kazi kwa mujibu wa taaluma na weledi wa kazi ya upolisi unavyotaka au mnafanya kazi kwa kupokea maagizo toka juu?

Kwa hayo maswali 2 tu hao Polisi watuhumiwa watakuwa wamemalizwa......
 
Kwa sababu wabunge wa Chadema wanajifanya "Hamnazo"
Humu JF tunajibizana kwa hoja na siyo utamaduni wa JF kujibizana kwa kejeli na matusi.....

Hizo tabia zipo kule kwenu mtaa wa Lumumba.....
 
IGP ndio atapelekwa mahakamani kwa matumizi mabovu ya madaraka. Hawa jamaa wanajidhalilisha sana yaani. Ndio maana saa nyingine wanasemwa ni maform 4 failures
Omari Mahita baada ya kustaafu aliburuzwa mahakamani kwa kumtia mimba house girl wake na kuruka matunzo ya mtoto .

Haikufahamika kama alimbaka kwa vitisho vya upolisi wake ama walikubaliana .

Kuna maisha mengine baada ya huu upolisi .
 
Back
Top Bottom