Polisi wetu sasa hii imekuwa too much!

Polisi wetu sasa hii imekuwa too much!

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,842
Reaction score
31,076
Hivi sasa nchini kwetu imekuwa ni jambo la kawaida sana kusikia Polisi wamemkamata Mbunge fulani wa upinzani na kumweka ndani Polisi na baadaye kumpeleka mahakamani na kumfungulia mashitaka ya uchochezi.

Hata hivyo sisi wananchi tunaofuatilia kwa karibu siasa za nchi hii tumegundua kuwa kwa kweli Jeshi letu la Polisi linafanya uonevu wa hali ya juu kwa viongozi wa upinzani na tuseme kwa hakika kuwa kwenye nchi yetu kwa sasa viongozi wa vyama vya upinzani wanakuwa treated kama vile ni wahamiaji haramu wa nchi hii na ni kama hawatakiwi kuishi ndani ya nchi hii!

Katika kipindi kisichozidi wiki moja hadi hivi sasa tumeshuhudia wabunge wa upinzani wafuatao wa Chama cha Chadema wakikamatwa na Polisi. Mbunge Esther Bulaya wa Jimbo la Bunda. Mbunge John Heche wa Jimbo la Tarime. Mbunge Tundu Lissu na Mbunge Godbless Lema.

Inashangaza kuona kuwa Polisi wetu wanawawinda na kuwakamata wabunge wa Chadema pekee na kutotaka kabisa kuwagusa wabunge wa CCM katika hayo wanayoyaita makosa ya uchochezi.

Nitatoa mfano mmoja wa wazi kabisa kuonyesha namna gani Polisi wetu wanavyofanya ubaguzi wa hali ya juu katika hiyo kamata kamata yao.

Mbunge wa CCM Mheshimiwa Kingu alienda kwenye Jimbo la Singida Mashariki, Jimbo ambalo Mbunge wake ni Tundu Lissu wa Chadema na kufanya mkutano wa harambee wa kuchangia ujenzi wa shule, Mbunge huyo hakukamatwa na Polisi kwa uchochezi.

Lakini tumeshuhudia majuzi Mbunge wa Chadema wa Jimbo la Bunda, Mheshimiwa Esther Bulaya akifanya "the same thing" kama alichofanya mwenzake wa CCM Mheshimiwa Kingu na kwenda Jimbo la Mbunge mwenzake wa Chadema John Heche wa Jimbo la Tarime kwa lengo la kufanya harambee kwa ajili ya ujenzi wa shule, Polisi walimkamata Mbunge Esther Bulaya na kwenda kumlaza ndani kwenye sero zao za Polisi na wakati wowote kuanzia sasa anaweza kuburuzwa mahakamani na kusomewa mashitaka ya kufanya uchochezi!

Nipende tu kuwakumbusha Polisi wetu kuwa nchi yetu ipo kwenye mfumo wa vyama vingi na kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 3(1) inasema hivi "Nchi yetu itakuwa kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa na vyama hivyo katika uendeshaji wa shughuli zao hakutakuwa na chombo chochote kitakachokuwa na mamlaka ya kuingilia shughuli za vyama hivyo" mwisho wa kunukuu.

Sasa niwaulize Polisi wetu iwapo mnafanya kazi zenu kwa weledi na kwa namna taaluma zenu zimavyowahitaji kutekeleza majukumu yenu ni kwanini basi mnaivunja Katiba ya nchi yetu waziwazi inayosema nchi yetu ni ya vyama vingi na mnawatreat viongozi wa vyama vya upinzani kama siyo raia wa nchi hii na ni kama vile wahamiaji haramu?

Polisi mkumbuke pia kuwa hata kama hayo mnayoyafanya ni maagizo toka juu lakini jikumbusheni ule msemo unaosema ya kuambiwa changanya na akili yako......

In case mambo yataharibika hapa nchini huyo aliye juu anayewatuma kufanya maovu hayo hatapandishwa kizimbani kwa kuwa anayo kinga ya kutoshitakiwa, ni nyinyi wenyewe as individuals mtakaoburuzwa mahakamani na majaji watakaosikiliza kesi zenu hawatachukulia Kama utetezi mtakapowaambia kuwa huyo maovu mliyokuwa mnayafanya yalikuwa maelekezo toka juu.....

Mwenye masikio na ausikie ujumbe huu muhimu.
 
Polisi wetu pia wanapaswa kujikumbusha wosia muhimu sana aliotuachia Baba wa Taifa letu Mwalimu Nyerere.

Katika moja ya hotuba zake alisema "Hatukuwaita wazungu wa Afrika Kusini makaburu kutokana na rangi yao, la hasha, tuliwaita wazungu wa Afrika Kusini makaburu kutokana na tabia zao za ubaguzi, kwa hiyo kwa yeyote anayefanya tabia za ubaguzi, whether awe mweupe au awe mweusi ni kaburu tuu" mwisho wa kunukuu

Kwa tabia zinazofanywa na Polisi wetu kwa hayo yanayoitwa ni makosa kwa wabunge kutotakiwa kwenye majimbo mengine, ni kwanini inapotokea wabunge wa CCM wamefanya hivyo iwe halali na wanapofanya hivyo wabunge wa Chadema iwe haramu?

Je huo siyo ubaguzi wa waziwazi kabisa na kwa wosia wa Mwalimu si alituusia kuwa nao tuwaite ni makaburu tuu?
 
Hivi sasa nchini kwetu imekuwa ni jambo la kawaida sana kusikia Polisi wamemkamata Mbunge fulani wa upinzani na kumweka ndani Polisi na baadaye kumpeleka mahakamani na kumfungilia mashitaka ya uchochezi.

Hata hivyo sisi wananchi tunaofuatilia kwa karibu siasa za nchi hii tumegundua kuwa kwa kweli Jeshi letu la Polisi linafanya uonevu wa hali ya juu kwa viongozi wa upinzani na tuseme kwa hakika kuwa kwenye nchi yetu kwa sasa viongozi wa vyama vya upinzani wanakuwa treated kama vile ni wahamiaji haramu wa nchi hii na ni kama hawatakiwi kuishi ndani ya nchi hii!

Katika kipindi kisichozidi wiki moja hadi hivi sasa tumeshuhudia wabunge wa upinzani wafuatao wa Chama cha Chadema wakikamatwa na Polisi. Mbunge Esther Bulaya wa Jimbo la Bunda. Mbunge John Heche wa Jimbo la Tarime. Mbunge Tundu Lissu na Mbunge Godbless Lema.

Inashangaza kuona kuwa Polisi wetu wanawawinda na kuwakamata wabunge wa Chadema pekee na kutotaka kabisa kuwagusa wabunge wa CCM katika hayo wanayoyaita makosa ya uchochezi.

Nitatoa mfano mmoja wa wazi kabisa kuonyesha namna gani Polisi wetu wanavyofanya ubaguzi wa hsli ya juu katika hiyo kamata kamata yao.

Mbunge wa CCM Mheshimiwa Kingu alienda kwenye Jimbo la Singida Mashariki, Jimbo ambalo Mbunge wake ni Tundu Lissu wa Chadema na kufanya mkutano wa harambee wa kuchangia ujenzi wa shule, Mbunge huyo hakukamatwa na Polisi kwa uchochezi.

Lakini tumeshuhudia majuzi Mbunge wa Chadema wa Jimbo la Bunda, Mheshimiwa Esther Bulaya akifanya "the same thing" kama alichofanya mwenzake wa CCM Mheshimiwa Kingu na kwenda Jimbo la Mbunge mwenzake wa Chadema John Heche wa Jimbo la Tarime kwa lengo la kufanya harambee kwa ajili ya ujenzi wa shule, Polisi walimkamata Mbunge Esther Bulaya na kwenda kumlaza ndani kwenye sero zao za Polisi na wakati wowote kuanzia sasa anaweza kuburuzwa mahakamani na kusomewa mashitaka ya kufanya uchochezi!

Nipende tu kuwakumbusha Polisi wetu kuwa nchi yetu ipo kwenye mfumo wa vyama vingi na kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 3(1) inasema hivi "Nchi yetu itakuwa kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa na vyama hivyo katika uendeshaji wa shughuli zao hakutakuwa na chombo chochote kitakachokuwa na mamlaka ya kuingilia shughuli za vyama hivyo" mwisho wa kunukuu.

Sasa niwaulize Polisi wetu iwapo mnafanya kazi zenu kwa weledi na kwa namna taaluma zenu zimavyowahitaji kutekeleza majukumu yenu ni kwanini basi mnaivunja Katiba ya nchi yetu waziwazi inayosema nchi yetu ni ya vyama vingi na mnawatreat viongozi wa vyama vya upinzani kama siyo raia wa nchi hii na ni kama vile wahamiaji haramu?

Mkumbuke pia Polisi kuwa hata kama hayo mnayoyafanya ni maagizo toka juu lakini mkumbuke ule msemo unaosema ya kuambiwa changanya na akili yako......

In case mambo yataharibika hapa nchini huyo aliye juu anayewatuma kufanya maovu hayo hatapanfishwa kizimbani kwa kuwa anayo kinga ya kutoshitakiwa, ni nyinyi wenyewe as individuals mtakaoburushwa mahakamani na majaji watakaosikiliza kesi zenu haewatachukulia Kama utetezi mtakapowaambia kuwa huyo maovu mliyokuwa mnayafanya yalikuwa maelekezo toka juu.....

Mwenyezi masikio na ausikie ujumbe huu muhimu.
hata kama mmetumwa jiongeZeni
 
hata kama mmetumwa jiongeZeni
Tumetumwa na nani?

Jibu hoja, je ni kwanini Jeshi letu la Polisi wamekuwa na kazi moja tu ya kuwawinda wabunge wa Chadema na kuwakamata na kuwafungulia mashitaka ya "kubambika"yasiyo na kichwa wala miguu?
 
Back
Top Bottom