Hamza kuua Polisi siyo hoja ya msingi kwenye hii mada. Mtu yeyote anaweza kuua kwani haya tumeyashuhudia sehemu mbalimbali hata huko Marekani. Hao Polisi wetu unaodai kuwa hawana mafunzo ya kutosha nao wanaweza kuua hata mara kumi ya hao.
Tunachozungumzia hapa ni Weledi na Uadilifu wa Polisi wetu. Polisi wetu kwa ujumla ni Waadilifu na ni Weledi ndo maana hata hayo matukio ya ajabu ajabu ni nadra sana kutokea hapa nchini ukilinganisha na nchi zingine. Kweli Nabii hathaminiwi kwao. Maana tukitilia maanani KAZI nzito na hatari wazifanyazo askari wetu kila siku katika mazingira magumu na hatari, ingetosha sana kukaa kimya tu kama tumeshindwa kuwapongeza na kuwaunga mkono.