Polisi wazima mapokezi ya Ndugulile | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wazima mapokezi ya Ndugulile

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 17, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Monday, 16 July 2012 13:51

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Elias Msuya

  MKUTANO ulioandaliwa na wakazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumpokea na kumsikiliza Mbunge wao, Faustine Ndugulile jana ulipigwa marufuku kwa kile kilichoelezwa kuwepo hatari ya kuvunjika kwa amani.


  Ndugulile alikuw aakirejea jimboni mwake jana, baada ya wiki iliyopita Naibu Spika, Job Ndugai kumpa adhabu ya kutohudhuria vikao vitatu vya Bunge alipodai kuwa baadhi ya madiwani wa Temeke walipewa rushwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ili kuruhusu mradi wa ujenzi wa Kigamboni.


  Hata hivyo hatua hiyo imeonekana kuwagusa wananchi wa Kigamboni na kumwandalia mkutano mbunge huyo, ambaye alipewa adhabu ya kutohudhuria vikao vitatu Bungeni wiki iliyopita.


  "Kesho saa nane mchana (jana) katika uwanja wa Machava uliopo Kigamboni Dar es Salaam, kutakuwa na mkutano wa wakazi wote wa Kigamboni kwa ajili ya kumpokea Mbunge wao aliyefukuzwa juzi Bungeni. Wananchi watasema yote aliyosema mbunge, wao ndiyo wamemtuma akayaseme Bungeni," ulisema ujumbe mfupi wa simu uliokuwa ukisambazwa kuwaalika watu.


  Mwandishi wa habari hizi alifika katika eneo la Machava ulipoandaliwa mkutano huo majira ya saa saba mchana na kukuta baadhi ya wananchi wakiondoa vyombo vya muziki na vipaza sauti na kusema kuwa mkutano huo umepigwa marufuku na polisi. Wakati huo magari ya doria ya polisi yalikuwa wakirandaranda eneo hilo la mkutano ambalo hata hivyo halikuwa na watu.


  Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, David Misime alikiri kupiga marufuku mkutano huo na kusema kuwa hakukuwa na njia nyingine ya kulinda amani ila kuchukua hatua hiyo.


  "Ni kweli tungeweza kuweka ulinzi lakini kwa hali ilivyojionyesha amani ingevunjika. Unaweza ukaulinda mkutano ndiyo ukasabaisha vurugu zaidi, ndiyo maana tumeamua kuupiga marufuku," alisema Misime.


  Naye Ndugulile akizungumza kwa simu na Mwananchi, alisema kuvunjwa kwa mkutano huo kunatokana na masuala ya siasa.


  "Hayo ni mambo ya siasa tu, mkutano huo uliandaliwa na wananchi wenyewe ili kutoa dyukuduku zao. Hata mimi nimejulishwa nikiwa najiandaa kwenda mkutanoni," alisema Ndugulile


  Kuhusu madai aliyotoa Bungeni, Ndugulile alisisitiza kuwa ni ya kweli. "Unajua, siyo kila kitu unaweza kuthibitisha Bungeni, lakini huo ni ukweli…," alisema Ndugulile.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Wow why he's CCM
   
 3. B

  Bob G JF Bronze Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hii ndo ccm bana, kila anae ongea ukweli ni CDM 2
   
 4. Dr F. Ndugulile

  Dr F. Ndugulile MP Kigamboni

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 248
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Sheria ya Mipango Miji no.8 ya 2007 inayosimamia mchakato wa Mji Mpya wa Kigamboni imekiukwa. Vipengele vinavyohitaji ushirikishwaji wa wananchi vimerukwa na hivyo kufanya mchakato huu hadi sasa kuwa batili.
  Suluhu ni kuanza upya mchakato huu kwa kufuata sheria.
   
 5. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,242
  Likes Received: 13,692
  Trophy Points: 280
  Naomba niulize huo mradi Uanze Upya Ili iweje wakati walishatangaza muda mrefu na picha na majina walipita kuangalia majengo.
   
 6. Dr F. Ndugulile

  Dr F. Ndugulile MP Kigamboni

  #6
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 248
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Ili kupata ufahamu ni vyema kuisoma na kuielewa sheria ninayoongelea ya Mipango Miji no.8 ya 2007. Kuna vipengele zaidi ya nane vya sheria havikufuatwa. Wananchi wanalalamika hawakushirikishwa kikamilifu na pia mchakato umekuwa ni wa muda mrefu kinyume ya kifungu na 24 cha sheria hii.
   
 7. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,242
  Likes Received: 13,692
  Trophy Points: 280
  Ungeweka hapa ingekuwa vzr sana, kumbukeni Serikali kipindi kile Mlitangaza kuwa kwa yeyote anayetaka kujenga basi asijenge na aliyejenga basi aishie hapo hapo.

  Watu kama hawa wachache ambao walikiuka kwa nn wapewe ushindi juu ya madai yao? Tulitarajia Mbunge wetu ututee juu ya malipo mazur na maslahi mengine maana watu wa juu walishaiuza Kigamboni yetu na ww hauna Nguvu kubwa sana kupinga juu ya hili suala. We si unakumbuka ulikuwa Mstari wa mbele kututetea juu ya kivuko kupanda?

  Lakini mpaka sasa kiko wapi??? Imebadilishwa kama ulivyotaka!!!???
   
 8. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,600
  Likes Received: 1,678
  Trophy Points: 280
  Kigamboni imekufa kabla ya kuanza


  [​IMG] Na Nyaronyo Kicheere - Imechapwa 25 May 2011

  Jamvi la Weledi  KASHFA nzito ya ardhi imeibuka Kigamboni jijini Dar es Salaam inayothibitisha usemi kwamba "penye fedha na ardhi viongozi wa chama tawala (CCM) na watendaji wake serikalini hawana haya."

  Tulikiona kilichotokea kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania. Kila mwenye jina katika CCM, alijichotea.
  Uhuni wa kupora fedha za EPA sasa unajirudia na unatekelezwa Kigamboni wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam. Tofauti na huko nyuma walipokuwa wanapora fedha, sasa wanapora ardhi ya wakazi wa Kigamboni kwa kisingizio cha kujenga mji mpya.

  Mgogoro uliopo ni kwamba watawala hawataki kabisa kufuata sheria zilizowekwa katika utekelezaji wa mradi huo. Hapa sheria zinazohusika ni Sheria ya Utwaaji wa Ardhi Na. 47 ya mwaka 1967 na Sheria ya Mipango Miji Na. 8 ya mwaka 2007.
  Walianza kwa kuutangazia umma mwaka 2008 kuwa kungejengwa mji mpya Kigamboni na wakazi wake wakazuiwa kuendeleza, kwa namna yoyote, ardhi yao hadi hapo watakapolipwa fidia ili kupisha ujenzi wa mji huo.

  Tangazo la serikali la 24 Oktoba 2008 kwenye gazeti la Serikali Na. 43 Vol. 89 lilikuwa na taarifa ya amri ambayo ilianisha mipaka ya eneo litakalokumbwa na ujenzi wa mji mpya kuwa ni kata tano za Somangila, Kigamboni, Vijibweni, Kibada na Mji Mwema.
  Amri ya serikali ilionyesha waziwazi kuwa ilifanyika chini ya kifungu cha 34 cha Sheria ya Utwaaji Ardhi sura ya 118 ambayo inahusu upangaji vizuri na ujenzi wa makazi tu na siyo viwanda, maofisi na maghorofa ya taasisi za umma.

  Sheria hii ya utwaaji wa ardhi inarahisisha sana utwaaji ardhi kwa ajili ya kuwapanga vizuri wakazi wanaoishi katika makazi holela, yasiyo na miundombinu mizuri kama barabara, maji, umeme, vituo vya afya, shule na majumba ya maendeleo.

  Sheria hii hairuhusu watawala kuleta watu wengine ili kuwaendeleza kwa kisingizio chochote kile hata cha uwekezaji. Ardhi ikitwaliwa chini ya sheria hii itagawanywa kwa wakazi walewale waliokuwapo baada ya kutenga maeneo ya ardhi kwa ajili ya miundombinu.

  Lakini kama lengo la kutwaa ardhi ni kwa ajili ya maendeleo, basi sheria husika inayotakiwa kutumika ni Sheria ya Mipango Miji namba 8 ya mwaka 2007. Sheria hiyo inawapa mwanya wa kuchukua maeneo na kugawa inayobaki au kuwaleta marafiki, wawekezaji na wengi wengine.

  Watawala wa CCM hawataki kutwaa ardhi chini ya sheria hii kwa sababu ina masharti magumu. Masharti hayo ni pamoja na kulazimisha uwazi na ushirikishwaji wananchi katika kuendeleza ardhi husika.

  Kifungu cha 8 cha sheria hiyo kinataka kabla ya kutangazwa eneo kuwa eneo la kuendelezwa, kwanza wananchi waelezwe na waukubali mpango/ mradi huo.

  Jambo hili halikufanyika Kigamboni kwa sababu sheria iliyotumika kutwaa ardhi yao siyo ya kutaka kuendeleza, bali ya kutaka kuwapanga wakazi waliojenga holela ili sasa nyumba zipangwe kwa mitaa na miundombinu iwekwe.

  Kifungu cha 11 cha Sheria ya Mipango Miji kinataka mamlaka husika kutayarisha rasimu ya uendelezaji huo ndani ya miezi sita kwa ushirikiano na wadau wote wakiwamo wamiliki wa ardhi kwa maana ya wananchi hasa wakazi wanaomiliki nyumba Kigamboni. Hili halikufanyika kabisa.

  Kifungu cha 19(3) kinazuia uendelezaji wa eneo lolote chini ya Sheria ya Mipango Miji kama utaratibu uliowekwa na sheria hiyo (kuanzia kwenye tangazo, uandaaji rasimu na upitishaji rasimu ulioainishwa katika vifungu 8 – 18) haukufuatwa.

  Pamoja na kwamba watawala wamekiuka sheria kwa kutwaa ardhi wakitumia sheria tofauti na sheria inayotakiwa kwa ajili ya uendelezaji wa ardhi ya Kigamboni, bado wamepanga awamu tatu za uendelezaji ardhi hiyo utakaotekelezwa katika miaka 20 tangu 2011 hadi 2030.

  Awamu ya kwanza imepangwa kuanza 2011 hadi 2020 ambapo yatajengwa madaraja na barabara na ujenzi wa nyumba 16,000 kutosheleza watu 100,000 kabla ya mwaka 2014; awamu ya pili 2021 hadi 2025 na awamu ya tatu ni 2026 hadi 2030.

  Maswali yanayokuja ni mengi. Kwanza mbona mpango huo haukufuata Sheria ya Mipango Miji ya mwaka 2007? Mbona utekelezaji wake umeanza kabla ya kupitishwa mpango kamambe (master plan)?

  Je, wananchi watakaaje tangu 2011 hadi 2030 bila fidia, bila kutumia ardhi yao kama dhamana kukopa, bila kuendeleza nyumba zao? Mbona mbunge wa Kigamboni Faustine Ndugulile yeye amejenga bila kuhojiwa? Mbona orodha ya wakazi haitangazwi wakati tunajua wameorodheshwa wasiokuwapo Kigamboni?

  Kwa nini wananchi wa Vijibweni wanahamishwa eti ili kupisha upanuzi wa bandari wakati eneo hilo lipo ndani ya mradi? Je, mamlaka ya uendelezaji mradi wa mji mpya Kigamboni (Kigamboni Development Authority) ndiyo inayowahamisha?

  Kama ni KDA mbona utaratibu tulioahidiwa wa kujengwa maghorofa ili wananchi wakihamishwa wakae haufuatwi? Maghorofa tuliyoahidiwa na Waziri wa Ardhi na Makazi, Anna Tibaijuka, hayajajengwa sasa hawa wananchi watakwenda wapi?

  Kumbukeni KDA ndiyo yenye jukumu la kuhamisha na kutoa makazi kwa wananchi wakati ahadi ya Rais Jakaya Kikwete alipotembelea Kigamboni kabla ya uchaguzi ilikuwa "hakuna mtu atakayehamishwa bali mtasogezwa kupisha miundombinu."

  Mbaya zaidi serikali inatangaza kwamba eti itawavunjia wale waliojenga baada ya amri ya zuio wakati yenyewe haisemi kuhusu jinsi ilivyokiuka sheria yenyewe na kitu gani kitafanywa kwa wakubwa waliokiuka sheria makusudi kuhakikisha wanapata ardhi Kigamboni.

  Historia ya mradi huu ni ndefu tangu tulipotangaziwa 2008 kuwa mji huo mpya wa Kingamboni ungekuwa wa kisasa wenye maghorofa kedekede, barabara pana kama Ulaya, madaraja mawili moja Kurasini na jingine Magogoni usawa wa ikulu pamoja na maeneo ya viwanda, burudani na mahoteli ya kitalii.

  Kwa kufahamu tabia za viongozi na watawala wetu kila mahali penye fedha na ardhi wananchi wa Kigamboni walianza mara moja kupiga kelele wakidai Kigamboni imeuzwa ili CCM wapate fedha za uchaguzi wa 2010. Wananchi hawakusema Kigamboni ilikuwa imeuzwa kwa nani.

  Wa kwanza kufika Kigamboni kuwatoa shaka wananchi ni aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi ambaye pia alikuwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati akisema wananchi hawatahamishwa bali watajengewa maghorofa ndani ya Kigamboni wakae.

  Chiligati alifuatiwa na Rais Kikwete ambaye alihutubia umati akikana Kigamboni kuuzwa na kusema ni mradi wa kuboresha makazi huku akisisitiza "hamtahamishwa ila mtasogea tu kupisha ujenzi wa miundo mbinu basi." Kikwete alitangaza pia kujengwa barabara ya Feri – Tungi kwa kiwango cha lami.

  Walipotembelewa na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi wa sasa, Anna Tibaijuka, wenye mabango ya kuonya uchakuachuaji ardhi yao wakakamatwa na polisi kwa amri ya diwani wa Kigamboni, Doto Masawani. Haya yote ni ushahidi tosha mradi haupo au umekufa.


  0785788727, kicheere@yahoo.com
   
 9. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu nafikiri wewe umesha jisahau unafikiri maeneo ya mbagala siyo mbunge wao barabara ni mbovu lakini wewe unatafuta umaarufu wa mji mpya acha ujengwe
   
 10. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Usitu karirishe vifungu vya sheria Kama magufuli hapa baada ya kunyimwa uwaziri ndio unaibuka kipindi chote ulikuwa kimya baada ya baraza la juzi kutokuwepo unajifanya unafunguka mnafiki mkubwa wewe. Hii ni serikali ya Chama chako ukitaka jivue gamba lakini si kutafuta umaarufu kimagumashi hapa
   
 11. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,906
  Likes Received: 5,367
  Trophy Points: 280
  mbunge wangu faustine tuambie tibaijuka kakulipa fidia shilingi ngapi?kwa nini peke yako?kama si usaliti ni nini?
   
 12. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  CCM ni CCM tu maana imeandikwa panya ni panya hakosi mkia. Hakuna jipya hapa huyu ni CCM na CCM ni wale wale yeye kama mbunge angegoma kulipwa fidia yeye kwanza na ahakikishe wanananchi wake wamelipwa swali la kujiuliza kwanini aliongelee hili sasa wakati lilikuwepo siku nyingi
   
 13. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Bw. Andungulile (samahani kwa kutokuanza na Mhe.) ebu tueleze hapa jamvini, kabla ya kutamka hadharani kwa maana ya bungeni maneno makali kwamba waziri alitoa mulungula kwa baadhi ya madiwani, kuna consultations zozote ulifanya kwa viongozi wa ngazi za juu ili kuwa-prompt na ikiwezekana wasitishe mchakato mzima au uliamua kujitoa kimasomaso kumwaga unga hadharani tu?

  Je, una data za kutosha kudhhirisha hicho ulichosema ambacho ni tuhuma nzito sana dhidi ya serikali inayoongozwa na chama chako tawala?

  Je, una maoni gani kwa kitendo cha polisi kuzuia mkutano uliopanga kuwapa wapiga kura wako feedback ya kilichojiri mjengoni? Marufuku hiyo ya polisi ni halali kisheria?
   
 14. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 738
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ni wao kwa wao, wenyewe kwa wenyewe. Ni ndugu na nduguye.
   
 15. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #15
  Jul 17, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  [​IMG]

  [​IMG]
  Kiagamboni city itakavyoonekana baada ya ujenzi kukamilika
   
 16. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #16
  Jul 17, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,076
  Likes Received: 7,566
  Trophy Points: 280
  Umezikimbia Changamoto za Mbagala ambao ndiyo walikupa kura nyingi zaidi na sasa umejikita zaidi kigamboni.

  Pia wewe ndiye uliyekuwa ukisimamia na kuratibu mchakato wa kamati ya wenye mali (nyumba) za Kigamboni kwa lengo la kuhakikisha wanalipwa stahili zao, na ndiye ambaye ulimualika waziri wa ardhi kuhudhuria vikao vyenu, na kikao chake cha kwanza kuhudhuria kilifanyika maeneo ya kwa Mwingila na msisitizo wake ulikuwa hili jambo lisirahisishwe kwa hoja za kisiasa kwani linaweza lika mislead watu na kujikuta wakitumia muda mwingi kupigania kitu ambacho haki exist ni na akashauri ni vizuri kusimamia mali za watu lakini ni vyema wakitumia washauri ambao ni wataalam kuliko majukwaa ya kisiasa.

  But all over sudden inashangaza kuona wewe ambaye ni mbunge wao ukiwa wa kwanza kutoulewa ushauri wa kitaalam uliopewa na sasa upo mstari wa mbili ukiwa mislead watu, ulitakiwa kwanza uuelewe mradi wenyewe wa Kigamboni una demand nini na ni mazingira yapi yanayoweza kuupelekea existence yake.

  Stop order iliyotolewa kwa watu kutojenga katika mji wa Kigambni ilisha expire bila chochote kufanyika na hapo ndiyo palikuwa pa kuanzia kutumia ushauri wa Prof. Tibaijuka, lakini wewe unataka kulikuza tofauti na lilivyo ili likupandishe chat. Tatizo kubwa la Kigamboni ni ugawaji holela na wa kimkakati wa viwanja kwa watu fulani huko maeneo ya Gezauolole n.k.

  Ifikirie Kigamboni kwa ukubwa na jigrafia yake ,watu wake na tofauti za matatizo wanazokabiliana nazo kulingana na maeneo yao, na siyo zile nyumba za pale kata, za mjimwema, kigamboni na Tungi tu, ambazo mnatengenezea stori kila uchao huku zikibadilika badilka. na kama stori zenu zingekuwa na ukweli wasingeongeza kata mpya pale.

  Anyways, Naweza nisikulaumu sana kwani katika kampeni zako hukuwa na mkakati wowote kushughulikia kero za watu, wala hukuwahi kuzifahamu kero zao kabla na thats why uliishia kujitambulisha jina, na elimu yako basi.

  Ni wakati sasa wa kujiimarisha na kujua namna ya kusimamia kero za watu ili kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya wapiga kura wako. Ulikuwa na timu nzuri ambayo ilikuwa tayari kukupa ushirikiano ili kuleta maendeleo jimboni kwako.

  Nashangaa unashindwa vipi wakati ungeweza kushirikiana na watu kama Masaga Kiboko, Thaddeus Musembi, Phares Magesa, Kazimbaya Makwega, Tesha n.k. ambao tofauti na wewe, wao tayari walikuwa na papers za utafiti wao ndani ya jimbo na wayfowards walizokuwa nazo, pia walikuwa tayari kukukabidhi plans zao na wao kukusaidia katika implementation yake, lakini ukawakwepa ukihofu watapa credits na kuwa threat kwako.
  Son, you have to change now.
   
 17. mwagavumbi 11

  mwagavumbi 11 JF-Expert Member

  #17
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Ndugulile hajui analoliongea na siamini kama wapiga kura wake watamuunga mkono katika hili. Lazima atambue kuwa mama Tibaijuka japo yuko CCM ni mtu mabye anakubalika sana katika jamii nzima ya Tanzania na dunia kwa ujumula. Sioni mantiki ya kuzuia mradi ambao umedumu miaka zaidi ya 4 na sas tumepata Jembe, mama Tibaijuka ambaye katumia kila mbinu kukoa mradi ambao ulikuwa unaelekea kufa.

  Nina mashaka kwamba huenda Mr.Ndugulile ametumwa na baadhi ya mafisadi wachache walioko huko kigamboni ili waendelee kuuteka na kuutawala mji huu wa Kigamboni kwan wao wameshajinyakulia maeneo kadhaa kwa njia isiyohalali ya kuwaonea wanyonge.
   
 18. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #18
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,242
  Likes Received: 13,692
  Trophy Points: 280
  au kuna plan za kutaka kugombea tena?
   
 19. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #19
  Jul 17, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Yaani maneno mazito mnamtupia mbunge wetu kwa kuwa ni CCM , hivi angekuwa wa chama cha wachaga leo naona angekuwa ni mshindi mkubwa! acheni ujinga nyie !
   
 20. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #20
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,242
  Likes Received: 13,692
  Trophy Points: 280
  ngoja aje.
   
Loading...