Polisi wazima maandamano Lindi, Mtwara... Hakukaliki!

Polisi wazima maandamano Lindi, Mtwara... Hakukaliki!

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
3,295
Reaction score
2,505
Polisi wazima maandamano Lindi, Mtwara hakukaliki

HALI ya usalama mkoani Mtwara bado tete baada ya jana Jeshi la Polisi kuwahamishia mkoani Lindi waandishi wa habari 150, waliokuwa katika mkutano wa siku tatu wa Kongamano la Nane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), uliofanyika Mtwara.

Waandishi hao walitoroshwa na polisi jana saa 11:00 alfajiri kwenda mkoani Lindi ambapo pia polisi walifanikiwa kusitisha maandamano yaliyokuwa yameandaliwa na Chama cha Wananchi (CUF), kwa lengo la kutaka kupata tathmini ya mwendelezo wa miradi ya gesi na maji.

Habari zinasema wananchi hao walitaka kuwateka waandishi wa habari kwa madai kuwa waliandika habari za kuzimwa kwa uasi wao kuhusu gesi na Waziri Mkuu Mizengo Pinda jambo wanalodai siyo kweli.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Wilman Ndile alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Hata hivyo, alisema kuwa taarifa hizo zilikuwa ni tetesi tu, akiongeza kwamba katika Mkoa wa Lindi kulikuwa na taarifa kwamba yangefanyika maandamano makubwa, lakini hakuna kilichotokea.

"Ulikuwa ni uvumi wa watu, unajua hivi sasa anaweza kuibuka mtu na kutuma ujumbe mfupi wa maneno kuhusu jambo lolote tu, ila suala hilo la waandishi wa habari ni kweli na asubuhi niliambiwa na OCD, lakini hali ni shwari sasa," alisema.

Mgogoro wa gesi uliibuka mwishoni mwa mwaka jana, baada ya Serikali kutangaza mpango wake wa kutandaza bomba la gesi kutoka mkoani humo kwenda Dar es Salaam.

Source: Mwananchi Jpili

MY Take:
Huu moto wa Mtwara unazimwa kwa mafuta ya Petroli na Waziri Mkuu Pinda

Kongamano la Mfuko wa Bima ya Taifa linafanyikia Mtwara, waandishi wa habari 150 wanaenda huko, then wananchi wanataka kuwateka? Hii hadithi ya Bulicheka imefikaje hapa? Wananache watake kuwateka waandishi wa habari?
 
Mkuu FJM, watu wa Mtwara wamechoka, wamezuiwa kupata taarifa zozote kuhusu maendeleo ya sakata la gesi, what else shuld they do? Pinda kazuia mikutano yao, iko wapi haki ya kupata habari kwao?

Hope wangefanikiw akuwateka wanahabari, wangekuwa wameandika historia katika sakata la kupigania haki zao. Nasikitika sana wameshindwa katika dakika za mwisho baada ya Polisi kuwatorosha wanahabari hao
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: FJM
hapo kazi ipo jamaa wamejitenga na dhambi ya kudanganywa na kusadiki upuuzi kazi kwa mawaziri wanaotoka huko.membe.chikawe.ghasia .mkuchika na shemeji yao
 
Kweli haki imefikia kupiganiwa kiasi hii hata kwa nchi yenye imani kama Tanzania?
 
Mkuu The Big Show tunakusubiri umepotelea wapi? Tujuze ya ndg zetu wa Ntwara.
 
Mkuu FJM, watu wa Mtwara wamechoka, wamezuiwa kupata taarifa zozote kuhusu maendeleo ya sakata la gesi, what else shuld they do? Pinda kazuia mikutano yao, iko wapi haki ya kupata habari kwao?

Hope wangefanikiw akuwateka wanahabari, wangekuwa wameandika historia katika sakata la kupigania haki zao. Nasikitika sana wameshindwa katika dakika za mwisho baada ya Polisi kuwatorosha wanahabari hao

JF,
Mie napita tu! Ukipita kwenye barabara kuna bill boards( mabango) makubwa ya CCM yameandikwa " CCM Dhaifu Nchi itayumba" siyo maneno yangu kama sijakosea haya maneno yalitamkwa na Hayati Mwl. Nyerere! I didn't always believe whether watu wa CCM walimwelewa Mwalimu . This is what is taking place sasa ilaumiwe Chadema au CUF wakati haya mambo aliyaona Nyerere kabla hajafa. Vijana tumieni the grey matter msifikirie Masaburi?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu FJM, watu wa Mtwara wamechoka, wamezuiwa kupata taarifa zozote kuhusu maendeleo ya sakata la gesi, what else shuld they do? Pinda kazuia mikutano yao, iko wapi haki ya kupata habari kwao?

Hope wangefanikiw akuwateka wanahabari, wangekuwa wameandika historia katika sakata la kupigania haki zao. Nasikitika sana wameshindwa katika dakika za mwisho baada ya Polisi kuwatorosha wanahabari hao

Tumwombe Mola tusifike huko kwenye red tena afadhali wameshindwa. Haya mambo ya kuteka hayafai na sio ya kuendekeza; watumie njia nyingine kudai haki zao na sio kuanzisha magenge ya kuteka watu.
 
Hii mbona kama habari ya udaku, hivi kwa Tanzania hii ninayoifahamu mkutano wa NHIF uwe na waandisi 150?
 
Mkuu The Big Show tunakusubiri umepotelea wapi? Tujuze ya ndg zetu wa Ntwara.
nilishamwambia bigshow alikua akitafuta kutoka.nadhani lengo limetimia,na huo ndo ubunifu wenyewe.
 
Kweli haki imefikia kupiganiwa kiasi hii hata kwa nchi yenye imani kama Tanzania?

Tofautisha Amani na Utulivu unaotokana na woga wa wananchi na unafiki wa wanaofaidika na huu ujingaujinga unaoendelea.
 
natamani watanzania wote tungekuwa kama wanatwara hii nchi ingekuwa zaidi ya dubai .kila kona ya nchi imejamaa maliasili na shangaa sasa sisi ndio tunaongoza kwa kukopa na kupewa misaada na ni masikini wa kudumu
 
Tumwombe Mola tusifike huko kwenye red tena afadhali wameshindwa. Haya mambo ya kuteka hayafai na sio ya kuendekeza; watumie njia nyingine kudai haki zao na sio kuanzisha magenge ya kuteka watu.

Ipi? Unbaweza kuwashahuri?
Kumbuka haki aiombwi!
 
Back
Top Bottom