POLISI : Wazazi wa watoto watakaopotea wakati wa sikukuu kushtakiwa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
4d9fb64546926d28c2cd7c2d4003c87b.jpg
Jeshi la Polisi limesema litawakamata wazazi wa watoto watakaopotea wakati wa sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao

Hatua inadaiwa ni kushindwa kutekeleza majukumu yao huku watoto wakijaa katika vituo vya polisi kutokana na kupotea

Akizungumza jana Dar es salaam, Msemaji wa jeshi la polisi nchini, Advera Bulimba alisema jeshi hilo halitawavumilia wazazi wa watoto watakaopotea nyakati hizi za sikukuu

"Utakuta watoto wanajaa kwenye vituo vya polisi kwamba wamepotea... sasa tunajiuliza amepotea mzazi wake alikuwa wapi? lazima mzazi awajibike na tutamchukua mzazi aweze kuisaidia polisi kutuambia kwanini mtoto wake amefika kituo cha polisi yeye alikuwa wapi"? alisema

Bulimba ambaye pia ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi hilo, alisema katika sikukuu hizi wazazi wanakuwa na tabia ya kuacha watoto wao na kwamba wanakwenda starehe kama fukweni na kutembea wenyewe jambo ambalo hawatakubaliana nalo

Alisema wazazi hao wataisadia polisi kufanya uchunguzi kwani kupotea kwa watoto ni uzembe

Bulimba aliwataka wananchi kuwa makini katika kipindi hiki, kwani kuna matapeli wanatumia majina ya viongozi kutaka taarifa zao au fedha, kutoa taarifa polisi
"Hatutawavumilia wanakunywa pombe na kuendesha magari tutawachukulia hatua za kisheria, wamiliki wa kumbi za starehe wazingatie uhalali wa leseni zao katika uingizaji wa watu"alisema

Bulimba aliongeza kuwa ni vema wamiliki wa maduka na hoteli kufunga vifaa vya kufuatilia taarifa za wateja wao (Kamera) ili kufuatilia nyendo zao

Alitaka wananchi wanapoona tofauti na mazingira wanamoishi watoe taarifa polisi au kumtambua mhusika asiyefahamika

Alisema "wananchi wakishirikiana tunaweza kupata taarifa za kiharifu mapema na kudhibiti, na hata wafanyabiashara wa maduka hufanya hivyo"

Alitaka wananchi kuwa makini na hata kuota taarifa za askari wazembe wanaochelewesha kutoa huduma kwa wananchi kwani zipo taratibu za kuwajibisha kwa wasiofanya kazi kwa weledi

"Kuna vituo vinahamishika hivyo ni kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma haraka na kwa wepesi kama kuna taarifa zozote waseme"alisema

Chanzo : JamboLeo
 
Itasaidia maana mzazi anaogesha mtoto na kumvalisha nguo halafu anamwachia aende atakako hii si sawa kabisa
 
Nauliza watawashtaki kwa Sheria gani, ufafanuzi.
 
Back
Top Bottom