Polisi wawakomesha wapinzani Kigoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wawakomesha wapinzani Kigoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Habarindiyohiyo, Apr 17, 2009.

 1. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jeshi la polisi mkoani Kigoma wilayani Kibondo limewakomesha wachama wa upinzani waliokuwa wakileta vurugu kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa marudio katika kata ya Kitahana. Hatua hiyo ya polisi imefuatia wafuasi wa upinzani katika kata hiyo kubandika bango katika kata hiyo lenye maandishi ya kumwelezea mgombea aliyeteuliwa na CCM kwenye kampeni za uchaguzi katika kata hiyo. Mgombea huyo mteule ameelezwa wasifu wake kuwa ni mjumbe wa mkutano mkuu wa wilaya wa chama hicho, katibu wa mbunge na mhasibu wa CCM wilaya ambaye anataka pia udiwani kupitia chama hicho. Pia wamemwelezea kuwa katika uchaguzi wa CCM wa mwaka 2008 alikamatwa na TAKUKURU kwa tuhuma za kutoa rushwa kwenye kura za maoni za CCM. Polisi hao sita waliokuwa na silaha na gari walifika na kulibeba bango hilo na kuondoka nalo pamoja na kuwatanya vijana kwa bakora katika kijiji hicho kutokana na uchochezi.

  CCM wanamtuhumu Mwenyekiti wa Kijiji Rusohoko kwa tiketi ya CHADEMA kuwa ndio chanzo cha uchochezi huo. Mgombea huyo wa CCM alishinda kwa kura za maoni kwa udhamini wa mfanyabiashara maarufu Kigoma anayemiliki Hoteli ya Hill Top bwana Sheni pamoja na mfanyabiashara mwingine anayefahamika zaidi kama DC wa Kibondo. Wafanyabiashara hawa pamoja na mfanyabiashara mwenzao Bwana Rajabu Maranda ambaye ni mweka hazina wa CCM Mkoa wa Kigoma wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha chama kinapata ushindi katika chaguzi. Baadhi ya wananchi waliohojiwa wameonyesha kusikitishwa na siasa za uchochezi zinazofanywa na wapinzani na kulipongeza jeshi la polisi kwa kuchukua hatua za haraka kukabiliana na hali hiyo

  .......ndiyohiyo
   
 2. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huyu Sheni na Maranda si ndio wale wa EPA? Hawa polisi badala ya kuchukua hatua juu ya tuhuma za rushwa kazi yao ni kupiga raia tu!

  Asha
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Polisi ni wa wafuasi wa Sultani CCM ambae anaitumia Katiba ya Chama Chake kushika hatamu ,ndio maana ya kushika hatamu hiyo ,polisi jeshi usalama wa Taifa wote wanakuwa kama mifugo yake.
   
Loading...