Polisi Wauana Kwa Risasi Jijini Mwanza Wakiwa Lindoni

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
ASKARI Polisi wa Kituo cha Polisi Nyamagana jijini Mwanza, Konstebo Daud Masunga Elisha, amemuua askari mwenzake, Konstebo Petro Saimon Matiko kwa risasi na baadaye kujiua kwa risasi na kufa papo hapo.

Tukio hilo lilitokea jana saa 8.30 mchana jijini Mwanza katika eneo la Benki ya Posta Tawi la Pamba wilayani Nyamagana huku chanzo cha mauaji hayo kikiwa hakijulikani.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha alisema kitendo hicho si cha kawaida ndani ya jeshi hilo, na kufafanua jinsi mazingira ya tukio lilivyotokea na kusababisha taharuki kwa wananchi na wateja waliokuwa ndani na nje ya benki hiyo.

Ni kweli kuna askari wawili wamefariki eneo la Benki ya Posta. Katika eneo la benki hiyo kulikuwa na askari wawili waliokuwa lindoni ambao ni PC Elisha na PC Remigius Alphonce mwenye namba H 4291, wakiwa wanaendelea na lindo alifika askari mwingine aliyekuwa amevaa kiraia PC Matiko na kuwasalimia kisha kuingia ndani ya benki kuchukua fedha, alieleza Kamanda Kamugisha na kuongeza:

Baada ya dakika tano, Matiko alitoka nje na kuwaeleza askari wenzake kwamba mtandao unasumbua, wakati akieleza hivyo, ghafla askari PC Elisha aliweka chemba risasi ambapo mwenzake PC Alphonce alimhoji mbona unaweka risasi katika hali ya utayari wa kutumika na alijibiwa kwa ufupi kwamba achana na mimi.

Ghafla alimfyatulia risasi PC Matiko na kumpiga eneo la bega la kushoto na kutokeza mgongoni na kuanguka chini, kitendo hicho kilimfanya PC Alphonce kukimbilia Benki ya Barclays ili kuomba msaada kwa askari wenzake waliokuwapo lindoni hapo.

Kabla ya askari hao kufika, ilisikika sauti ya mlio wa risasi na baada ya kurudi alimkuta PC Elisha akiwa amejipiga risasi kwenye paji la uso na kutokea nyuma ya kisogo, tayari akiwa amepoteza maisha.
 
Duh! Hii hatari sana. Viongoz wa polis jaribuni kuwa makini na askari ili kujua tofauti zao na mafadhaiko yao. Lakn tofauti na hapo nyinyi mnawatumia askar wadogo kama toilet paper.

Hebu chukulia kama hyo gadhabu angekuja nayo kituon na kuingia ofisin kwa Ocd au RPC ingekuwaje?
 
Au alidhan jambazii ktk nafs kumsuta akaijikuata kafanya ivoo_tathimin yangu tu
 
ASKARI Polisi wa Kituo cha Polisi Nyamagana jijini Mwanza, Konstebo Daud Masunga Elisha, amemuua askari mwenzake, Konstebo Petro Saimon Matiko kwa risasi na baadaye kujiua kwa risasi na kufa papo hapo.

Tukio hilo lilitokea jana saa 8.30 mchana jijini Mwanza katika eneo la Benki ya Posta Tawi la Pamba wilayani Nyamagana huku chanzo cha mauaji hayo kikiwa hakijulikani.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha alisema kitendo hicho si cha kawaida ndani ya jeshi hilo, na kufafanua jinsi mazingira ya tukio lilivyotokea na kusababisha taharuki kwa wananchi na wateja waliokuwa ndani na nje ya benki hiyo.

?Ni kweli kuna askari wawili wamefariki eneo la Benki ya Posta. Katika eneo la benki hiyo kulikuwa na askari wawili waliokuwa lindoni ambao ni PC Elisha na PC Remigius Alphonce mwenye namba H 4291, wakiwa wanaendelea na lindo alifika askari mwingine aliyekuwa amevaa kiraia PC Matiko na kuwasalimia kisha kuingia ndani ya benki kuchukua fedha,? alieleza Kamanda Kamugisha na kuongeza:

?Baada ya dakika tano, Matiko alitoka nje na kuwaeleza askari wenzake kwamba mtandao unasumbua, wakati akieleza hivyo, ghafla askari PC Elisha aliweka chemba risasi ambapo mwenzake PC Alphonce alimhoji mbona unaweka risasi katika hali ya utayari wa kutumika na alijibiwa kwa ufupi kwamba ?achana na mimi.?

?Ghafla alimfyatulia risasi PC Matiko na kumpiga eneo la bega la kushoto na kutokeza mgongoni na kuanguka chini, kitendo hicho kilimfanya PC Alphonce kukimbilia Benki ya Barclays ili kuomba msaada kwa askari wenzake waliokuwapo lindoni hapo.

?Kabla ya askari hao kufika, ilisikika sauti ya mlio wa risasi na baada ya kurudi alimkuta PC Elisha akiwa amejipiga risasi kwenye paji la uso na kutokea nyuma ya kisogo, tayari akiwa amepoteza maisha.?

99.999% Ya Mauaji Ya WAJEDA Kwa WAJEDA au MANDATA Kwa MANDATA Huwa Ni Wivu Wa KIMAPENZI Na Mara Nyingi Hali Hii Hutokea Pale Ambapo Mmoja Wao Anakuwa Ameenda KOZI Ile Fupi Ya Miezi 3 au Ile Ya Miezi 6 au 9 Halafu Ukute Kule Ktk Makazi Yao Wanaishi Jirani au Karibu Hapo Ni Lazima Tu Mmoja Wao ( Hasa Yule Anayebaki ) Atambandulia au Kumkanyagia Mwenzake Mke Wake. Wanajeshi ( Wajeda ) au Mapolisi ( Mandata ) Huwa Hawana BIFU Za Kudhulumiana Pesa Ila Ukitaka Uone UKATILI Wao Mmoja Wapo AGONGEWE Ndipo Utawajua.
 
Uamuzi wa kijinga kabisa wa kuua na kujiua

Na Ujinga Zaidi Unakuja Pale Ambapo Nyie ( Wao ) MAPOPOMA Wawili Wamejiua Labda Kwa WIVU Wa Kimapenzi Halafu Huyo Demu Wanaomgombania Sasa ANAUKESHEA Tu IKUPILIPA NKOBA Lodge au KYAKA NKUNDE Guest House Na MASELA Wengine. Hapa Ndipo Naona Kiwango Chetu Kidogo Cha KUFIKIRI Kwa Baadhi Ya Wanaume Wenzetu. Yaani MBUNYE Tu Inakufanya Ujitawanye UBONGO Wako Na Umtungunyue Mwenzio Kweli? Mbona Mademu Wamejaa Kibao Hata Wa Buku Buku Na Mkopo?
 
Kwa vyovyote vile mchokozi ni huyo askari aliyekuwa kiraia, kamfuata mwenzake kwenye lindo ili kumlingishia kuwa anataka kutoa ela ili akaitumie kumgegedea demu wake
lkn jamaa (muuaji) alikuwa ameshapata infor
 
Na Ujinga Zaidi Unakuja Pale Ambapo Nyie ( Wao ) MAPOPOMA Wawili Wamejiua Labda Kwa WIVU Wa Kimapenzi Halafu Huyo Demu Wanaomgombania Sasa ANAUKESHEA Tu IKUPILIPA NKOBA Lodge au KYAKA NKUNDE Guest House Na MASELA Wengine. Hapa Ndipo Naona Kiwango Chetu Kidogo Cha KUFIKIRI Kwa Baadhi Ya Wanaume Wenzetu. Yaani MBUNYE Tu Inakufanya Ujitawanye UBONGO Wako Na Umtungunyue Mwenzio Kweli? Mbona Mademu Wamejaa Kibao Hata Wa Buku Buku Na Mkopo?

Fedheha ya kiwango cha mwisho kabisa, au dharau ya kiwango cha juu kabisa kutoka kwa mwanaume mwenzako hasa anayekufahamu ni kukuchukulia demu wako. Na wewe subiri siku moja ukafume kademu kako kanagalagazwa, tuonane kama utapiga mapambio ya kumsifu jamaa.
 
Maamuz ya kipuuzi hayo ila naamini constable za pale nyamagana zinajua chanzo cha tukio
 
Back
Top Bottom