Polisi waua tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi waua tena

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Oct 5, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Paulo Kasabago


  Jeshi la Polisi limeendelea kuandamwa na matukio ya kuua raia baada ya askari wake wanne, akiwamo Mkuu wa Kituo (OCS) kukamatwa kwa tuhuma za kuvamia nyumba ya kulala wageni, kujeruhi, kupora mali na kumuua mchimbaji wa madini.

  Tukio hilo limetokea katika Wilaya ya Chato, mkoani Geita baada ya askari hao kutuhumiwa kuwavamia wafanyabiashara wawili waliokuwa kwenye nyumba hiyo, kuwapora fedha, mawe yanayosadikiwa kuwa dhahabu na kuwajeruhi kwa vipigo ambavyo vilisababisha kifo cha mmoja wao.

  Askari wanaotuhumiwa kuhusika katika tukio hilo ni wa kituo cha polisi cha Buziku wilayani Chato ambao waliwavamia David Gilles Vyamana na Gilbert Ntabonwa, wakazi wa kijiji cha Kakeneno wilayani humo na wazaliwa wa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.

  Tukio hilo lilitokea usiku wa Agosti 30, mwaka huu wakati watu hao wakiwa kwenye nyumba ya wageni ya Buziku Inn.

  Watu hao wanaosadikiwa kuwa ni wachimbaji wadogo wa dhahabu, kabla ya kukumbwa na mkasa huo, walitokea kijijini kwao Kakeneno na kuelekea kijiji cha Buziku kwa ajili ya kuburudika na kwamba baada ya kupanga vyumba katika nyumba hiyo mmoja akiwa chumba namba mbili na mwingine namba tatu, walimuomba mhudumu kuendelea kuwahudumia vinywaji wakiwa vyumbani.

  Habari zinasema kuwa saa 5:30 usiku, polisi walivamia eneo hilo na kuwaamuru wachimbaji hao kufungua milango ya vyumba vyao.

  Kwa mujibu wa chanzo chetu, baada ya watu hao kukataa kutii amri hiyo huku wakihoji uhalali wa kuwaamuru kufungua milango wakati wamelala, askari hao walitumia nguvu kubwa na kufanikiwa kuvunja milango kisha kuanza kuwaadhibu kwa vipigo vikali.

  Habari zinadai kuwa katika chumba cha kwanza askari hao walichukua kiasi cha Sh. 500,000 na mawe yanayosadikiwa kuwa ni dhahabu yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye mfuko mdogo katika chumba cha pili.

  Baada ya kuwapa kichapo, waliwachukua na kuwapeleka kwenye kituo cha polisi na kushikiliwa kwa muda na baadaye baada ya kubaini kuwa hali zao zinaendelea kuwa mbaya kutokana na majeraha, walilazimika kuwaondoa haraka na kuwapeleka kwenye Kituo cha Afya cha Bwanga kabla ya kuwahamishia Hospitali ya Wilaya ya Chato kwa matibabu zaidi.

  Shuhuda mwingine, alidai kuwa baada ya wachimbaji hao kukaidi kufungua milango licha ya mhudumu wa nyumba hiyo, Godesiliva Paulo, kuwataarifu kuwa wanaowahitaji ni askari polisi, polisi walilazimika kutumia nguvu kuingia ndani, lakini katika hali ya kushangaza wachimbaji hao walikutwa ndani ya chumba kimoja wakiendelea kunywa pombe na ghafla mmoja wao alimkwida koo PC Mwidin, hali iliyowalazimu kutumia nguvu kubwa kuwaondoa vyumbani vyao kwa lengo la kuwapeleka kituo cha polisi.

  Aliongeza kuwa baada ya askari hao kufanikiwa kuwatoa ndani ya chumba wachimbaji hao walikaidi kwenda kituo cha polisi na kuanza kupiga yowe wakiomba msaada kwa wananchi na baada ya muda mfupi, watu wengi walikusanyika eneo hilo na kuanza kuwashambulia na kuwajeruhi.

  Alisema kuwa baada ya kutambua hali zao siyo nzuri walilazimika kuwapeleka kupata matibabu, lakini wakati wakiendela kuhudumiwa, mmoja wao aliyefahamika kwa jina la Gilbert Ntabonwa (40) alifariki dunia akiwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Chato.

  KAULI YA KAIMU RPC

  Akizungumza na NIPASHE, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Paulo Kasabago, mbali na kuthibitisha kuwapo kwa tukio hilo, alisema kuwa uchunguzi wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa askari wake walienda kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusiana na kuwepo kwa watu wanaohofiwa kuwa ni wahalifu kutokana na mazungumzo yao wakati wakinywa pombe kabla ya kuingia ndani ya vyumba vyao.

  “Askari wetu walikwenda eneo hilo baada ya kupigiwa simu na raia mwema kuwa watu waliokuwa wakinywa pombe kwenye gesti hiyo siyo wema kutokana na mazungumzo mbalimbali waliyokuwa wakiyazungumza kabla ya kuhama nje na kuingia ndani ya vyumba vyao,” alisema Kasabago.

  Kufuatia hali hiyo jeshi hilo linawashikilia askari wake wanne akiwemo mkuu wa kituo hicho, Sajenti Raulens Bendera, kwa ajili ya uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo la mauaji na kwamba itakapothibitika kuhusika, hatua za kisheria zitashika mkondo wake.

  ASKARI WANAOSHIKILIWA

  Kamanda Kasabago aliowataja wengine wanaoshikiliwa kuwa ni PC Mwidini, PC abdallah na PC Yusuph, wote wakiwa ni askari wa kituo kidogo cha Buziku wilayani Chato.

  Kamanda Kasabago aliongeza kuwa baada ya upekuzi uliofanywa na askari hao, waliwakuta wachimbaji hao wakiwa na fedha taslimu Sh. 500,500, kiroba cha mfuko unaosadikiwa kuwa na mawe ya dhahabu na chupa moja ya bia.

  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Chato, Dk. Pius Buchukundi, alithibitisha kupokea majeruhi wawili waliopelekwa hospitalini hapo kutoka Kituo cha Afya cha Bwanga na kwamba wakati wakiendelea kuwatibu, mmoja wao alifariki dunia na kwamba Vyamana anaendelea vizuri.

  Dk. Buchukundi alisema kuwa uchunguzi wao ulibaini kuwa marehemu alijeruhiwa kutokana na kipigo kilichosababisha damu kuvujia ndani ya mwili.

  Kwa mujibu wa Dk. Buchukundi, tayari ndugu na jamaa wa marehemu huyo wamefika na kuchukua mwili wake kwa ajili ya kuusafirisha kwenda nyumbani kwao Kibondo, mkoani Kigoma kwa ya maziko.

  Septemba 2, mwaka huu, polisi walimuua aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, mkoani Iringa, Daudi Mwangosi, katika kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa wakati viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakifungua tawi la chama chao.

  Askari mmoja, Pacificus Cleophace Simon (23), alifikishwa mahakamni mjini Iringa akikabiliwa na kosa la kumua Mwangosi.

  Jumapili iliyopita Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi wa Septemba pamoja na mambo mengine aliwataka polisi kuacha kutumia nguvu kupita kiasi wanapokabilina na vikundi na raia.
  CHANZO: NIPASHE

   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  kawaida yao kupora na kuua
   
 3. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,351
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Tukimbilie wapi jamani endapo wale tunaotegemea kuwakimbilia kwao wamegeuka wauaji na wanyang'anyi? Kwa nini serikali isiwalipe mshahara wa kutosha ili wasitishe zoezi hilo?What a pitty country?
   
 4. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,096
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Hawa jamaa kweli ni noma. Walishawahi kunibeba pale Morogoro (Msamvu) kisa nililipia chumba guest, nikaregister then nikatoka. Kurudi nikakuta chumba kina mtu mwingine, nilipokuja juu nikashangaa nabebwa kwa mabuti nikatupiwa kwenye defender. Iliniokoa guest register.
   
 5. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  U-Askari ni kazi ya laana na ndo maana maaskari wengi HAWATUMII busara ktk maamuzi yao........... kwa maono yao
  wanajiona kama miungu watu na wako juu sheria!!!!!!:confused2:
   
 6. T

  Teko JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 3, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Ni kweli mkuu! Unajua kwa mtu asiye kumbana bado na vitimbwi vya polisi hawezi amini wanayosema watu kuwa baadhi ya polisi sio watu wanaotumia kabisa busara ktk maamuzi yao,wao daima ni kukurupuka tu,hawana muda wa kuchunguza issue kabisa japo kwa muda mfupi.Na matokeo yake ndo haya tunayoyaona.Binafsi nilishawahi vamiwa na kundi la polisi nyumbani kwangu kwasababu tu ya kusikia maneno ya watu, na kwa vile wao ni wakurupukaji hawachunguzi jambo kwanza,wakajikuta wamewinda denge lisilo liwa!
   
 7. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,802
  Likes Received: 2,575
  Trophy Points: 280
  You do not lead by hitting people over the head-that is assault not leadership. Qoute US president Dwight Eisenhower alipokosowa tawala kandamizi.
   
 8. sindano butu

  sindano butu JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 20, 2012
  Messages: 478
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 45
  shida zote wanazozipata wananchi ni kwasababu ya sheria mbovu na matakwa ya watawala. POLISI- watawala power!!
   
 9. Dogo1

  Dogo1 JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,102
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Mawazo yenu juu ya polisi yanaweza kuwa mazuri but mnayatoa @ wrong place, pelekeni kwenye kamati ya maoni ya katiba mpya!
   
 10. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,096
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Umekutana nao mkuu hao watu wa tume? Unaweza fikiri uko kizimbani. Na hivi watz walivo waoga, hiyo katiba wataibadilisha rangi tu.
   
 11. k

  kilaki Member

  #11
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 27, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yale,yale tuliyozoea.mnaua nyie,mnachunguza nyie kwa tume yenu na mnatoa hukumu nyia na zaidi ya hayo nyie ndio watekelezaji wa hukumu.kichekesho kweli kweli.:A S embarassed:
   
 12. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,548
  Likes Received: 1,593
  Trophy Points: 280
  upo umuhimu mkubwa kwa jeshi la polisi watendaji wake kupatiwa elimu ya haki na wajibu wa raia pamoja
  na wao kupatiwa elimu ya kujua mipaka ya kufanyia kazi
  lakini kwa kuwa ni kasumba au ni jeuri tu ya kujiona wapo juu ya sheria
  sidhani kama watazingatia elimu watakayo patiwa kuhusu wajibu na haki na taratibu na sheria zinazotumika
  katika kazi
   
Loading...