Polisi watakiwa walipe gharama za umeme wenyewe

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Machungu ya Serikali ya awamu ya tano ya Rais Magufuli kudhibiti mapato na matumizi ya fedha za umma yamegusa masilahi ya polisi na kuwaacha na maumivu.

Kutokana na hali hiyo Serikali ya Dr Magufuli imeamua kuwa askari walipe gharama za umeme wao wenyewe tofauti na ilivyokuwa katika Serikali za awamu zilizopita ambapo gharama za umeme zilikuwa zikilipwa na Serikali.

Chanzo: Tanzania Daima
 
Machungu ya serekali ya awamu ya tano ya Rais Magufuli kudhibiti mapato na matumizi ya fedha za umma,Yamegusa masilahi ya polisi na kuwaacha na maumivu.
Kutokana na hali hiyo serekali ya Dr Magufuli imeamua kuwa askari walipe gharama za umeme wao wenyewe tofauti na ilinyokuwa katikati serekali za awamu zilizopita ambapo gharama za umeme zilikuwa zikilipwa na serakali.
Source Tanzania Daima
Wametupiga mabomu weeee Sasa wanasoma plate number.Ccm ni ile ile

Tatizo liko wapi wanapewa posho ulitaka wapewe posho halafu tena walipiwe?.Wenzao waliopanga uswahilini umeme wanalipiwa na nani?
 
Waboreshe mishahara yao sasa maana wasije kutuletea tatizo sisi wananchi la kuwalipia kupitia rushwa na uhalifu wa aina mbalimbali
 
Hilo ni kweli kwa sasa wanajilipia umeme tofauti na ilivyokuwa zamana kila floor ina mita yake
 
Uwiiiiii mzee wangu JPM naomba uku kwetu usije nahisi hata mijengo utasema tulipie.
 
Machungu ya serekali ya awamu ya tano ya Rais Magufuli kudhibiti mapato na matumizi ya fedha za umma,Yamegusa masilahi ya polisi na kuwaacha na maumivu.
Kutokana na hali hiyo serekali ya Dr Magufuli imeamua kuwa askari walipe gharama za umeme wao wenyewe tofauti na ilinyokuwa katikati serekali za awamu zilizopita ambapo gharama za umeme zilikuwa zikilipwa na serakali.
Source Tanzania Daima
Wametupiga mabomu weeee Sasa wanasoma plate number.Ccm ni ile ile
Kuna upotoshwaji mkubwa sana kwenye hii habari .na ndio maana kuna mambo hayajaandikwa! Sasa hivi utaratibu ni kufunga ruku na kila mtu atalipa anacho tumia na posho za umeme na mambo mengine zinawekwa kwenye mshahara.....! Tanzania Daima lengo lao ni kuonesha polisi wamekomolewa kumbe wamepunguziwa mzigo....
 
SI WAALIPE TU KWANI SHIDA NI NINI MPAKA WASILIPE ?ZILE RUSHWA WANAZOKAMUA WANANJI KWANINI WASILIPEUMEME NA NAULI ? SI WANAPEWA MISHAHARA NASHANGAA HATA KWENYE MABUS HAWALIPI WAKATI HUDUMA ZAO NI MBOVU VITUONI UNAENDA KITUONI UNAJIBIWA UTUMBO WAKATI ILE NI KAZI YAO NA WAMECHAGUA WENYEWE

WALIPEEEEEEEEEEEEEEE

UMEME
NAULI NA MENGINEYO VINGINEVTO WAPANDE MAKALANDINGA YAO
 
Yaani Watanzania tunapenda ubwete sana....yaani jitu linaonaje ugumu wa kulipia kitu ulichotumia....??
 
Kuna upotoshwaji mkubwa sana kwenye hii habari ... Tanzania Daima lengo lao ni kuonesha polisi wamekomolewa kumbe wamepunguziwa mzigo....
Hapo kwenye bold & red. Huduma ya LUKU ni pre-paid, yaani unalipa kwanza halafu unaendelea kutumia kwa kusikilizia. Huko kupunguziwa mzigo, ina maana posho watakayokuwa wanalipwa ni kubwa kuliko matumizi halisi ya umeme? Umejuaje kama mzigo utapungua wakati matumizi ya kila kaya ya askari yanatofautiana na malipo halisi yanakuja kujulikana kadri atumiavyo?
 
Kumbe walikuwa wanalipiwa umeme!! kwanini walipiwe wakati wafanyakazi wengine wanalipa wenyewe?
 
Kuna upotoshwaji mkubwa sana kwenye hii habari .na ndio maana kuna mambo hayajaandikwa! Sasa hivi utaratibu ni kufunga ruku na kila mtu atalipa anacho tumia na posho za umeme na mambo mengine zinawekwa kwenye mshahara.....! Tanzania Daima lengo lao ni kuonesha polisi wamekomolewa kumbe wamepunguziwa mzigo....
Kweli mkuu, hawa waandishi wa magazeti ya wafuasi wa iliyokuwa Ukawa kazi yao ni kuponda tu na kupotosha.
 
Back
Top Bottom