Polisi wasuasua kujibu madai ya Mwakyembe

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
Manumba(10).jpg

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba



Jeshi la Polisi linakwepa kutoa tamko la kukataa au kuthibitisha madai yaliyotolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kwamba linatumiwa na mafisadi kutokana na taarifa iliyotoa kuwa ugonjwa unaomsumbua waziri huo hautokani na kulishwa sumu.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, hivi karibuni alisema uchunguzi uliofanywa na jeshi hilo na kupata taarifa toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ugonjwa unaomsumbua Dk. Mwakyembe hautokani na kulishwa sumu.

Hata hivyo siku moja baada ya tamko hilo, lDk. Mwakyembe aliibuka na kueleza kuwa Jeshi hilo lina ufinyu wa uelewa unaojitokeza kwenye tamko lake unaosisitiza kuwa hakunywesha.

Dk. Mwakyembe alieleza kuwa vyombo vya dola likiwemo Jeshi la Polisi vinapelekeshwa na mafisadi ndiyo maana vimetoa taarifa kwamba hakulishwa sumu ambayo inatofautiana na ile iliyotolewa na madaktari waliokuwa wakimtibu nchini India.

Msemaji wa Polisii, Advera Senso, alipopigiwa Ijumaa ya wiki iliyopita alimtaka mwandishi kuwasilisha maswali ya mambo anayotaka kuyauliza kwa maandishi ili yajibiwe. Jumanne wiki hii NIPASHE iliwasilisha maswali, lakini

tangu juzi hadi jana Senso amekuwa akipiga danadana kutoa majibu ya maswali hayo.
Juzi alipofuatwa ofisini kwake, alisema maswali ameyapokea, lakini yapo katika ofisi ya utawala na kuahidi jana kufuatilia ili yaweze kujibiwa lakini kinyume chake amedai kuwa bado hayajajibiwa.

Jeshi la Polisi limeanza kumsaka mchawi aliyeibua madai hayo ili ashtakiwe mahakamani kutokana na uamuzi wa kupeleka jalada la mashtaka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP). Senso, alisema jalada hilo limeshapelekwa kwa DPP ingawa hakuwa tayari kueleza kwa kina wanaotuhumiwa katika jalada hilo.




CHANZO: NIPASHE


kipanya_23-_02-_2012_20120223_1036903633.jpg
?????
 
Nipashe vp?mbona wanairudia rudia habari hii kwa mwelekeo ule ule?au kule kukumbushia inshu ya mtoto wa Mengi kubambikiwa madawa na kina Mkumbo,Nzowa kajipatia credit tosha IPP?
 
Kumbe picha linaendelea now liko kwa DPP,jamani series nyingine ikitoka mtujuze.
 
hii controversy ya mwakyembe na kulishwa sumu sijui itaishia wapi... it is aserious matter that needs to be seriously addressed badala ya kupigwa danadana za kisiasa
 
Wajibu tena nini wakati majibu tulishayapata kuwa wao ni waongo na hatutakuja kuwaamini tena na wanavyozidi kutuuwa hivi
 
Tatizo Polisi wameruhusu kutumiwa na wasiasa kwa manufaa yao binafsi, na hii itacost their integrity!!!!!
 
Nipashe vp?mbona wanairudia rudia habari hii kwa mwelekeo ule ule?au kule kukumbushia inshu ya mtoto wa Mengi kubambikiwa madawa na kina Mkumbo,Nzowa kajipatia credit tosha IPP?

Mkuu hii habari imerudiwa kivipi?wao walitegemea kupata majibu kwa huyo Senso ijumaha ya juzi kama walivyoahidiwa,wamerudi ijumaha hakuna kilichoendelea zaidi ya danadana
 
Back
Top Bottom