Polisi wasaka mchawi sakata la Mwakyembe

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,957
Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe

Baada ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, kusema ugonjwa unaomsumbua Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, hautokani na kulishwa sumu, Jeshi la Polisi limeanza kumsaka mchawi aliyeibua madai hayo ili ashtakiwe mahakamani.

Kati ya wanaohofiwa kwamba wanaweza kukumbwa kushtakiwa kwa tuhuma hiyo, ni ama Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, au Dk. Mwakyembe mwenyewe. Mchakato wa kumtafuta mchawi katika suala hilo unatokana na uamuzi uliochukuliwa na

Jeshi la Polisi kukamilisha upelelezi wa suala hilo na kupeleka jalada la mashtaka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP).DPP amepelekewa jalada hilo ili aamue kama wanaotoa taarifa kwamba Dk. Mwakyembe alilishwa sumu washtakiwe mahakamani au la.Hatua hiyo imechukuliwa na Jeshi hilo zikiwa zimepita siku chache tangu DCI Manumba, kueleza kuwa ugonjwa unaomsumbua Dk.

Mwakyembe hautokani na kulishwa sumu. Msemaji wa Polisi nchini, Mrakibu Msaidizi wa Jeshi hilo (ASP), Advera Senso, akizungumza na NIPASHE jana ofisini kwake, alithibitisha kupelekwa kwa jalada hilo kwa DPP. Hata hivyo, Senso hakuwa tayari kueleza kwa kina

wanaotuhumiwa katika jalada hilo kutoa taarifa kuhusu Dk. Mwakyembe kulishwa sumu. Wakati Senso akisita kutaja wanaotuhumiwa katika jalada hilo, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amekuwa akitamka hadharani kuwa ugonjwa unaomsumbua

Dk. Mwakyembe, unatokana na kulishwa sumu. Kutokana na kauli hiyo ya Waziri Sitta, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, pamoja Jeshi la Polisi mara kadhaa wamekuwa wakinukuliwa na vyombo vya habari wakimtaka Sitta kupeleka ushahidi

unaoonyesha kuwa Dk. Mwakyembe amelishwa sumu. Sitta amekuwa akieleza hivyo katika mikutano yake kadhaa ikiwemo anayoalikwa makanisani. Siku moja baada ya Manumba kukanusha madai juu ya Dk. Mwakyembe kulishwa sumu, Naibu Waziri huyo alilishambulia Jeshi la Polisi kwa kueleza kuwa lina ufinyu wa uelewa. Dk. Mwakyembe alisema kulishwa sumu si lazima mtu anyweshwe ili imdhuru

wakati inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa tu. Alisema Jeshi la Polisi limejiingiza kwenye suala ambalo kwa takriban mwaka mzima halijawahi kuwa na dhamira ya dhati ya kulielewa au kulichunguza mbali na kulifanyia mzaha kupitia magazetini.

CHANZO: NIPASHE
 
Hili Jeshi la polisi linafurahisha sana, hivi Dr. Mwakyembe aliishutumu serikali au anatuhumu kikundi cha watu kumlisha sumu? Inakuwaje linashupalia kufungua kesi kwa nini watuhumiwa wasifungue wao kesi ya madai? Kama ni hoja ya watu kuwatuhumu wengine zipo tuhuma nyingi tu mitaani na wafikirie kufungua kesi pia.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
As I have been always telling my JF members there is strong commitment of these two police speakers they both aim at maintaining some status ahead of the time. I could call it as corruptiob of office responsibilies. Both deserved persecution in serious government but not this corrupt country.
 
Inshu ya Dr mwakyembe imekuwa ndo ya kuuzia magazeti sasa. Hakuna kipya ktk habari hii. shame on you Nipashe ktk hili! matokeo ya waandishi wavivu
 
Ndo akome kuwa na nyumba ndogo tabata.....network search.....
 
Wachawi wao wenyewe!! Kutuletea statement za uongo....washazoea kuburuzwa watu na mambo yao Yale ya kubambikia kesi....sasa wakaonelea waje na uzushi Huu. Timing imekataa safari hii
 
Kuna polisi majambazi - Samuel Sitta ..... Nakubaliana nawe,kwa kubambikia kesi jamaha awajambo
 
Yeaaah! The source is reliable, but why the investigation do not start from the source too?
 
Kinachofurahisha mpaka hapa ni ukweli kuwa mchezo huu sasa unawarudi waliouasisi. Dr. Mwakyembe alipoongoza kamati teule ya bunge kuandaa ripoti ya nusu-ukweli alidhani anaisaidia serikali. Lakini sasa imemgeuka.
Aliyekuwa spika wa bunge. Samwel sitta alipozima mjadala wa richmond kwa rungu lake kuu alhdhani anaisaidia serikali. Kumbe sivyo leo inamwona mwongo na mzushi. Naona sasa yanatimia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…