Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,743
- 2,601
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara limewataka viongozi wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) kusitisha mpango wao wa kufanya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2026 mjini Musoma.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 1, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Pius Lutumo, amesema Jeshi la Polisi limeridhia kuendelea kutekeleza amri ya mahakama inayokataza chama hicho kufanya shughuli za kisiasa hadi kesi ya msingi inayowakabili itakapomalizika mahakamani.
Amesema kupitia mitandao ya kijamii, Jeshi la Polisi limebaini picha na taarifa za BAWACHA zikihamasisha kufanyika kwa maadhimisho hayo, hatua ambayo ameieleza kuwa ni ukiukwaji wa makusudi wa amri ya mahakama.
Kutokana na hali hiyo, Jeshi la Polisi limewataka viongozi wa BAWACHA waliohusika na kikao cha maandalizi kufika Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Mara (Makosa ya Jinai) Machi 2, 2026 kwa ajili ya mahojiano.
“Jeshi la Polisi linaendelea kutambua amri hiyo kwani haijatenguliwa. Tunawashauri CHADEMA kurejea mahakamani kumaliza shauri lao badala ya kukaidi amri ya mahakama, jambo ambalo kimsingi ni dharau kwa mahakama (contempt of court),” amesema Lutumo.
Chanzo: Jambo TV
Soma Kimenuka: Pamoja na Katazo Batili la Polisi BAWACHA yatangaza kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani bila kuogopa chochote