Polisi wamtosa Kibanda

Polisi wamtosa Kibanda

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803


JUMAPILI, MACHI 24, 2013 08:55 NA WAANDISHI WETU


​
SIKU 19 zikiwa zimepita baada ya tukio la kutekwa na kuteswa kinyama kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, Jeshi la Polisi limeshindwa kutoa taarifa ya mwenendo wa uchunguzi linaoufanya kuhusu sakata hilo kama lilivyoahidi awali.

Makamanda wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi, kwa nyakati tofauti walipoulizwa na MTANZANIA Jumapili kuhusu mwenendo wa uchunguzi huo unaofanywa na makachero 12, wamekuwa wakipiga danadana kueleza ukweli.
Sambamba na hilo, uchunguzi wa MTANZANIA Jumapili umebaini kuwa uchunguzi wa makachero hao hadi sasa haujawagusa majirani wa Kibanda na hata watu waliomuokota na kumpeleka hospitali akiwa mahututi nao hawajaitwa kuhojiwa na polisi.

Uchunguzi huo wa polisi pia haujawagusa wafanyakazi wenzake wala simu zake za mkononi zinazoaminika kuwa zinaweza kusaidia katika uchunguzi huo, nazo polisi hawajataka kuzikagua.

Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ACP Ahmed Msangi, ambaye ni mmoja wa makachero wanaounda timu ya watu 12 wanaochunguza mkasa wa kutekwa na kuteswa kwa Kibanda, alipotafutwa na gazeti hili jana kupitia simu yake ya kiganjani ili kujua uchunguzi huo ulipofikia, baada ya kupokea simu alianza kufanya vituko.

ACP Msangi baada ya kupokea simu na kujuliana hali na mwandishi kujitambulisha, alipotakiwa kuthibitisha uwepo wake ndani ya timu hiyo na hatua ambazo timu hiyo imefikia katika uchunguzi wake, alianza kuita kwenye simu haloo, halooo, na hata mwandishi alipomwambia kuwa anamsikia ajibu kwa sauti ya taratibu, alizidi kupayuka kwenye simu neno haloo kisha akakata simu.

Alipopigiwa tena na tena, simu yake ilikuwa haipatikani, jambo lilioonyesha kuwa aliizima kabisa.

ACP Msangi ndiye aliyeongoza tume iliyoundwa kuchunguza tukio la kutekwa na kuteswa kinyama kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka, ambayo hadi sasa majibu yake hayafahamiki.

MTANZANIA Jumapili lilimtafuta pia Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, kupitia simu yake ya kiganjani na alipoulizwa kuhusu mwenendo wa uchunguzi wa sakata hilo, alieleza kuwa hana la kusema, kwa sababu anasubiri majibu ya tume hiyo.

"Tume ikishaundwa huwezi ukatoa taarifa mpaka wao waje na majibu na ndiyo tunasubiri, bado tunategemea baada ya muda muafaka tutatoa taarifa," alisema Kamanda Kova.

Hata hivyo, wiki iliyopita, Kamanda Kova alipoulizwa na gazeti hili kuhusu mwenendo wa uchunguzi huo, alisema kuwa suala hilo limekwishapita uwezo wake kwa sababu linashughulikiwa na ngazi ya makao makuu, hivyo wenye uwezo wa kulizungumzia ni maofisa wa makao makuu.

Siku moja baadaye, Kamanda Kova alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akieleza kuwa taarifa ya mwenendo wa uchunguzi wa tukio la kutekwa na kuteswa kwa Kibanda ingetolewa na tume wiki iliyopita, jambo ambalo halikufanyika.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emanuel Nchimbi, naye ni mmoja wa viongozi waandamizi wa serikali waliokataa kuzungumzia sakata la Kibanda.

Nchimbi alikataa kuzungumzia kutekwa kwa Kibanda Machi 12, baada ya waandishi wa habari kumtaka afanye hivyo katika mkutano aliouitisha kutangaza uamuzi wa serikali kuwafukuza kazi polisi watano kwa kosa la wizi, kwa kile alichodai kuwa suala hilo ni dogo sana linashughulikiwa na Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, naye alipoulizwa sakata hili kupitia simu yake ya kiganjani, yeye alilihamisha kutoka makao makuu na kuelekeza Kanda Maalumu ya kipolisi ya Dar es Salaam kwa kueleza kuwa suala la Kibanda haliko mikononi mwa makao makuu, bali limekabidhiwa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kulichunguza.

Tangu tukio hilo lilipotokea, Jeshi la Polisi na viongozi waandamizi serikalini wamekuwa wakipiga danadada kuweka wazi ukweli wa waliohusika kumteka na kumjeruhi Kibanda, jambo ambalo limemsababisha kuibuka kwa hisia mchanganyiko kwa jamii kuhusiana na unyama huo.

Wachambuzi na wafuatiliaji wa mambo wanaeleza kuwa huenda suala hilo likachukua mwelekeo unaofanana na ule wa tukio la Dk. Ulimboka, ambapo ni takribani miezi tisa sasa hakuna uhalisia wa aliyekamatwa akihusishwa na kutekwa kwake.

Licha ya Dk. Ulimboka kumtaja katika hati ya kiapo, Ofisa wa Ikulu, Ramadhani Ighondu, kuwa ndiye mhusika mkuu wa kutekwa na kuteswa kwake, hakuna taarifa zinazoonyesha hatua alizochukuliwa Ofisa huyo, tofauti na ambavyo imekuwa ikichukuliwa katika matukio mengine ya kihalifu.

Kumekuwa na maswali mengi kuhusu utendaji kazi wa Jeshi la Polisi na wengi wa waliohojiwa kuhusiana na hilo wamehoji nguvu iliyotumika kuwasaka na kuwatia nguvuni watuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Marehemu Liberatus Barlow, ambao walikamatwa siku 12 tu baada ya tukio.

Kamanda Barlow aliuawa Oktoba 13 mwaka jana, saa 8 usiku, kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika eneo la Minazi Mitatu, huko Kitangiri Mwanza, wakati akimsindikiza Mwalimu Dorothy Moses nyumbani kwake, kutoka katika kikao cha harusi.

Baada ya tukio hilo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba, aliongoza uchunguzi uliofanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa na katika taarifa yake kwa IGP Mwema, alisema makachero walitumia mbinu mbalimbali kwa kuunda kikosi cha nguvu kazi kilichokua chini yake kilichojigawa kwenye makundi matatu, moja likiwa la ukamataji, la pili la mahojiano na tatu la intelijensia na makundi yote yalitumia njia za kisayansi, ikiwa ni pamoja na kufuatilia mitandao ya simu.

Tayari watu mbalimbali wamekwishaanza kuonyesha mashaka kuhusu uchunguzi unaofanywa na Jeshi la Polisi kuhusu tukio la kutekwa na kuteswa kwa Kibanda.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Haki za Binadamu ( LHRC), Dk Helen Kijo Bisimba, alipozungumza na MTANZANIA Jumapili, alisema Jeshi la Polisi lina mambo ambayo halitaki kuyafanyia kazi, hivyo upo umuhimu wa kutafuta nguvu ya ziada ili ukweli uweze kubainika.

Bisimba alisema kuwa kuna masuala ambayo jeshi hilo linakwepa kujihusisha nayo kwa karibu na kutolea mfano tukio la Dk. Ulimboka kutokuwa na taarifa kamili hadi leo.

Makamu wa Rais wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani (IAWT) na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), Jaji Eusebia Munuo, alisema kuwa hiyo ni kazi ya polisi kuchunguza na kutoa taarifa hivyo waachiwe jukumu hilo.

Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Azaveli Lwaitama, alisema anashangazwa kuona polisi wakitumika kisiasa katika suala la msingi.

"Mbele ya safari itatugeuka, kwani tunajenga siasa kuwa ni kuteka, kuua watu na hata gazeti lililokuwa likiripoti kwa kina kutekwa kwa Dk. Ulimboka limefungiwa, hivyo ni mchezo wa kuigiza na hali hii ni mbaya kisiasa," alisema Dk. Lwaitama.


 
Time will tell...yetu macho..wasipoziba ufa waandae matofali ya kujenga ukuta.
 
wamchunguze nani? wakati wao ndio wahusika! binadamu kaumbwa na asili ya aibu, hapo walipo dhamiri zao zinawahukumu, yaani hawana amani kabisa.
 
Polisi wanapata wakati mgumu ku deal na kesi za ugoni kwasababu walioteswa aidha hawataki kutoa ushirikiano kwa kuogopa aibu na kuharibu ndoa zao au wanaomba polisi waache kuchunguza.

Matokeo yake wanatumia mwavuli wa siasa kuficha ukweli kwamba mateso yao ni vita binafsi. Haiji akilini kwamba mtu anapigwa halafu anakimbia kutoa ushahidi wa waliompiga au a atoa ushahidi nusunusu.

Bora hata mteswa moja amesema kwamba sakata lake sio lakisiasa kuliko jamaa wa Mabwepande asiyesomeka kabisa. Ugoni noma!!
 
Polisi wanapata wakati mgumu ku deal na kesi za ugoni kwasababu walioteswa aidha hawataki kutoa ushirikiano kwa kuogopa aibu na kuharibu ndoa zao au wanaomba polisi waache kuchunguza. Matokeo yake wanatumia mwavuli wa siasa kuficha ukweli kwamba mateso yao ni vita binafsi. Haiji akilini kwamba mtu anapigwa halafu anakimbia kutoa ushahidi wa waliompiga au a atoa ushahidi nusunusu. Bora hata mteswa moja amesema kwamba sakata lake sio lakisiasa kuliko jamaa wa Mabwepande asiyesomeka kabisa. Ugoni noma!!

Mkuu wewe ni mkongwe,unayeheshimika hapa JF hebu nyoosha hii habari yako!
 
Mkuu wewe ni mkongwe,unayeheshimika hapa JF hebu nyoosha hii habari yako!

Mkuu, mara nyingi sikurupuki. Na habari hii haijapinda hata kidogo. Utaona kesi hizi mbili zitakavyoisha kwa ajabu ajabu kwasababu sio kesi za kisiasa. Ni kesi binafsi ambazo wanasiasa wamezibatiza kuwa za kisiasa kwa faida za kisiasa.

Watanzania tunadhani wahariri na public figures hawana maisha binafsi wala ugomvi binafsi unaoweza kuhatarisha maisha yao na inapotokea wamepigwa basi moja kwa moja tunahusisha taaluma au position zao na hivyo kuingiza siasa.

Tuna tatizo endapo tunadhani wahariri au waandishi kama ilivyo mdokta au walimu kwamba hawana maadui binafsi. Ajabu tunalazimisha kila kesi kuwa ya kisiasa ata kama aliyepigwa anasema sio hivyo.

Kibanda kasema kwa mdomo wake kwamba sakata lake halihusiani na siasa lakini bado JF tunataka liwe la kisiasa!!! Ifike muda tuambizane ukweli kwamba kesi fulani sio za kisiasa. Hili ni gumu kwasababu mazingira ya mateso yanaweza kuwa ya aibu kwa mteswa kuyasema. Yule kiongozi aliyeibiwa simu na ela Morogoro alikubali kwamba ilikuwa kazi nzuri ya changudoa? Polisi walisema hivyo? Kwanini leo walioteswa kwa ugoni waseme chanzo au polisi waseme chanzo?

Kesi hizi zitaishia hivi hivi na werevu eatajuwa kwamba polisi waki report ukweli watakuwa wanafanya kile wazungu wanaita blaming the victim.
 
Hivi kweli mtu na akili zake timamu anaweza akahusisha tukio la Ulimboka na Kibanda kuwa ni matukio ya ugoni, sasa ninaanza kuona kuwa kuna tatizo kubwa sana katika mitazamo
 
Wewe ni mmoja katika uchunguzi wa kuteswa kwa ulimboka?
 
Mkuu, mara nyingi sikurupuki. Na habari hii haijapinda hata kidogo. Utaona kesi hizi mbili zitakavyoisha kwa ajabu ajabu kwasababu sio kesi za kisiasa. Ni kesi binafsi ambazo wanasiasa wamezibatiza kuwa za kisiasa kwa faida za kisiasa.

Watanzania tunadhani wahariri na public figures hawana maisha binafsi wala ugomvi binafsi unaoweza kuhatarisha maisha yao na inapotokea wamepigwa basi moja kwa moja tunahusisha taaluma au position zao na hivyo kuingiza siasa.

Tuna tatizo endapo tunadhani wahariri au waandishi kama ilivyo mdokta au walimu kwamba hawana maadui binafsi. Ajabu tunalazimisha kila kesi kuwa ya kisiasa ata kama aliyepigwa anasema sio hivyo.

Kibanda kasema kwa mdomo wake kwamba sakata lake halihusiani na siasa lakini bado JF tunataka liwe la kisiasa!!! Ifike muda tuambizane ukweli kwamba kesi fulani sio za kisiasa. Hili ni gumu kwasababu mazingira ya mateso yanaweza kuwa ya aibu kwa mteswa kuyasema. Yule kiongozi aliyeibiwa simu na ela Morogoro alikubali kwamba ilikuwa kazi nzuri ya changudoa? Polisi walisema hivyo? Kwanini leo walioteswa kwa ugoni waseme chanzo au polisi waseme chanzo?

Kesi hizi zitaishia hivi hivi na werevu eatajuwa kwamba polisi waki report ukweli watakuwa wanafanya kile wazungu wanaita blaming the victim.

MTAZAMO hajakuambia mara ngapi!.. Hizo awamu chache sana mojawapo ni hii!.. Kubali kukosolewa!
 
Polisi wanapata wakati mgumu ku deal na kesi za ugoni kwasababu walioteswa aidha hawataki kutoa ushirikiano kwa kuogopa aibu na kuharibu ndoa zao au wanaomba polisi waache kuchunguza. Matokeo yake wanatumia mwavuli wa siasa kuficha ukweli kwamba mateso yao ni vita binafsi. Haiji akilini kwamba mtu anapigwa halafu anakimbia kutoa ushahidi wa waliompiga au a atoa ushahidi nusunusu. Bora hata mteswa moja amesema kwamba sakata lake sio lakisiasa kuliko jamaa wa Mabwepande asiyesomeka kabisa. Ugoni noma!!
Kwa heshima zote!
Nakuomba ukatafute mahali popote uwezapo na usome kuhusu athari za mateso kwa mtu aliyeteswa.
Mateso ysiwe kupigwa makofi lakini yawe ni torture kama kung'olewa kucha bila ganzi,kung'olewa jino zima bila ganzi,kuwekwa maji ya moto kwenye njia ya haja kubwa,kupimwa sehemu za siri n.k.

Kitaalamu ni kuwa ikifanyiwa mateso hayo kiwiliwili chako kinajenga chuki na nafsi yako na huwi mtu mmoja yule wa kabla na ni mara chache utapenda kusimulia hayo kwani kuna kukinzana ndani ya mwili mmoja.

Wanawake wanabakwa alkini mara nyingi wanaamua kuugulia labda pawe na ushahidi wa watu waliiona lakini most of the time hawaelezi kwa mtu.Watu wanaonajisiwa kwa nguvu ndani ya magereza mara nyingi hawasimulii.

jambo la pili ni wazi kabisa nalo ni kuwa ikiwa vyombo vya dola ndivyo villivyofanya hivyo na unapotaka kuropoka wakakutishia kuwa next time itakuwa mara mbili ya ile ya mwanzo,je utazungumza?Unless ukimbie nchi.
 


JUMAPILI, MACHI 24, 2013 08:55 NA WAANDISHI WETU


​


Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ACP Ahmed Msangi.
Hii nchi...Msangi..!
Ah, anyways. Acha nielekee zangu shambani mida maana the first bird has already spoken a while ago.
 
Watanzani kwanza hawajui kama wana haki ya kupata huduma za serikali. Hawajui wajibu wa serikali kwao na hata wanapohudumiwa katika mtindo huu uliojaa uzandiki, ubaguzi, kiburi, maringo na ulio chini ya kiwango, wanapiga makofi wakijua ni hisani tu wala si haki yao.

Kwa mtindo huo utaona pamoja na yote lakini kwa kukosa ufahamu huo, wnazidi kuishi kwa unafiki wakipiga makofi kwa serikali huku mioyo yao ikilia machozi ya damu, wakidhani labda wakijipendekeza hivyo watatupiwa tupiwa japo mifupa zaidi.

Unless ccm inaondoka madarakani, Watanzania tusahau kupata huduma sahihi kutoka chombo chochote che serikali kwa sababu serikali haiko kwa ajili ya wananchi. WE ARE NOT THE GOVERNMENT'S PRIORITY ZAIDI YA KITENDENDEA KAZI CHAKE, KULIPA KODI NA KUTUMIA UWEPO WETU KATIKA KUKIDHI PERSONAL INTERESTS ZA WATAWALA.
 
Mkuu, mara nyingi sikurupuki. Na habari hii haijapinda hata kidogo. Utaona kesi hizi mbili zitakavyoisha kwa ajabu ajabu kwasababu sio kesi za kisiasa. Ni kesi binafsi ambazo wanasiasa wamezibatiza kuwa za kisiasa kwa faida za kisiasa.

Watanzania tunadhani wahariri na public figures hawana maisha binafsi wala ugomvi binafsi unaoweza kuhatarisha maisha yao na inapotokea wamepigwa basi moja kwa moja tunahusisha taaluma au position zao na hivyo kuingiza siasa.

Tuna tatizo endapo tunadhani wahariri au waandishi kama ilivyo mdokta au walimu kwamba hawana maadui binafsi. Ajabu tunalazimisha kila kesi kuwa ya kisiasa ata kama aliyepigwa anasema sio hivyo.

Kibanda kasema kwa mdomo wake kwamba sakata lake halihusiani na siasa lakini bado JF tunataka liwe la kisiasa!!! Ifike muda tuambizane ukweli kwamba kesi fulani sio za kisiasa. Hili ni gumu kwasababu mazingira ya mateso yanaweza kuwa ya aibu kwa mteswa kuyasema. Yule kiongozi aliyeibiwa simu na ela Morogoro alikubali kwamba ilikuwa kazi nzuri ya changudoa? Polisi walisema hivyo? Kwanini leo walioteswa kwa ugoni waseme chanzo au polisi waseme chanzo?

Kesi hizi zitaishia hivi hivi na werevu eatajuwa kwamba polisi waki report ukweli watakuwa wanafanya kile wazungu wanaita blaming the victim.

Kwa hiyo tuko lisipokuwa la kisiasa watuhumiwa hawana haja ya kupatikana ???
 
Kwa hiyo tuko lisipokuwa la kisiasa watuhumiwa hawana haja ya kupatikana ???

Ipo haja na ni haki watuhumiwa wakapatikana, lakini hili litendeke wateswa lazima watoe ushirikiano mkubwa katika msako. Wafanye hivyo bila aibu. Ajabu wateswa wamekuwa wakijichanganya kila wanapotakiwa watoe ushirikiano.

Sasa wengi wenye uelewa mdogo watadai kwamba wateswa wanahofia maisha yao endapo watatoa ushirikiano. Hii sio kweli maana zipo taasisi za kimataifa zenye jukumu la kulinda uhai wa mtu yeyote. Taasisi hizi ziko tayari kutoa kibali kwa mtu yeyote kwenda kuishi nchi nyingine (political refugee) endapo tu wamejiridhisha kwamba serikali ya nchi yake inahatarisha uhai wake.
 
Back
Top Bottom