Polisi wamsaka MwanaCHADEMA aliyeiba kadi za ACT

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,985
Reaction score
1,286
Mwanachama wa CHADEMA, Thobias Sebastian anasakwa na jeshi la polis kwa tuhuma za kuiba vifaa vya uenezi vya ACT TANZANIA kadi na bendera. Ameiba vifaa hivyo na kuvipeleka kwenyue ofisi za chadema. Amefanya hivyo huku akidanganya umma kwa kusema kadi hizo zimerudishwa na wanachama, kadi gani ya kurudishwa haina jina, picha na sahihi ya afisa wa chama?

Huu wizi umefanywa kwa makusudi ili kukwamisha shughuli za uenezi wa chama chetu, na ikumbukwe kutengeneza kadi na bendera ni gharama, na kwa kiasi fulani huyu Bwa Thobias ametukwamisha kwani zile kadi zilihitajika sana Mbeya na wengi wamekosa kadi kutokana na kitendo chake hiki kishetani.

Kiogozi wa ACT mkoa wa Mbeya alilipoti polisi na ametoa taarifa kwenye vyombo vya habari na gazeti la JAMBO LEO LIMEANDIKA SEHEMU YA TAARIFA HIYO.

ACT.jpg

ACT 2.jpg

IFUATAYO CHINI NI SEHEMU YA TAARIFA YAKE KWA UMMA.

KATIKA hali ya kuonyesha ACT ni tishio kwa vyama vingine vya siasa, viongozi wa CHADEMA Mkoani Mbeya wamelazimika kuiba kadi za chama hicho kipya na kuzipeleka ofisini kwao ili ionekane kwamba zimerudishwa kwao na wanachama wa ACT.Tukio hilo lilitokea tarehe 9/8/2014 jijini Mbeya wakati wa sherehe za ufunguzi wa ofisi ya ACT-Tanzania Mkoa wa Mbeya.

Tukiwa kwenye sherehe za ufunguzi wa ofisi za chama chetu mkoa wa Mbeya, alitokea kada wa CHADEMA Thobias Sebastian ambaye hapo kabla aliwahi kufika katika ofisi za chama chetu kuomba uanachama wa ACT na kukataliwa. Kwa mara ya kwanza alifika ofisini wiki moja iliyopita na kuomba uanachama wa chama, ambapo kamati ya muda ya uongozi wa ACT Mbeya baada ya kujadili maombi yake ya uanachama ikajidhirisha kwamba Thobias hana mwenendo mzuri katika siasa za jijini Mbeya ilimkatalia kumpa uanachama.

Siku ya sherehe za ufunguzi wa ofisi za chama mkoa wa Mbeya tarehe 10/08/2014, kada huyo wa CHADEMA alionekana akiranda randa kwenye maeneo ya ofisi zetu. Mnamo majira ya saa 11 jioni wakati sherehe imeshika kasi na nje ya ofisi viongozi wa ACT wakiwa wanazungumza na wananchi waliojitokeza kwenye tukio hilo, ghafla tulimwona Thobias akitokea ndani ya ofisi zetu na kuanza kutimua mbio huku akiwa ameshika kadi mpya za ACT mkononi mwake. Viongozi kwa kuhofia kuharibu sherehe waliamua kwenda kuripoti tukio hilo kituo kidogo cha polisi Uyole. Na kwa uzito wa tukio lile na muda ule wa jioni, askari wa zamu alitupa maelekezo viongozi wa ACT kupeleka shauri kituo kikuu cha polisi jijini Mbeya siku itakayofuata. Tumekwisha ripoti kituo kikuu cha polisi na kupaitwa RB NO UY/RB/1815/2014

Pia tumesikitishwa na taarifa za upotoshaji na zisizofuata maadili ya uandishi wa habari kwa kutopata ufafanuzi wa upande wa pili na kupotosha umma wa watanzania zilioandikwa na gazeti la Tanzania Daima la tarehe 11/8/2014. Ni aibu kwa chombo cha habari kuandika habari inayojichanganya, sehemu moja wakisema kadi zilitupwa sehemu nyingine picha ikionyesha anayetuhumiwa kuiba hizo kadi akimkabidhi mbunge wa CHADEMA.

Tunaamini kwa kuwa jambo hili limeripotiwa kwenye vyombo vya usalama jijini Mbeya, sheria itachukua mkondo na vifaa vya ACT vitarudishwa na matendo haya ya kihuni yatakomeshwa kwenye siasa za Tanzania.

KATIBU WA ACT-TANZANIA
MKOA WA MBEYA.
 
Nyie ACT hamna ajenda nyingine zaida ya CHADEMA.?
 
Wajinga kweli hawa ACT Mpanda wamefukuzwa kwenye ofisi baada ya utapeli kodi , Mona kutokomea na kodi ya chumba cha ofisi .....
 
tujiulize maswali haya,
1. je hizo kadi ziliibiwa wapi?
2. kama ofisini, je mlikuta ofisi imevunjwa?
3. na kama ameporwa mwanachama wenu ilikuwaje tukio hilo la uporwaji?
4. ni nani mwenye mjukumu ya kusimamia hizo kadi zenu na alikuwa wapi wakati tukio linatokea?
lakini ninaweza amini kuwa mligawa kwa wanachama mliowalaghai, kisha wao wakaamua kufanya hvyo walivyofanya.
 
tujiulize maswali haya,
1. Je hizo kadi ziliibiwa wapi?
2. Kama ofisini, je mlikuta ofisi imevunjwa?
3. Na kama ameporwa mwanachama wenu ilikuwaje tukio hilo la uporwaji?
4. Ni nani mwenye mjukumu ya kusimamia hizo kadi zenu na alikuwa wapi wakati tukio linatokea?
Lakini ninaweza amini kuwa mligawa kwa wanachama mliowalaghai, kisha wao wakaamua kufanya hvyo walivyofanya.

njoo na lissu mahakamani aulize maswali hayo,,, lakini wewe huwez,,, na huyo lisu ataumbuka tuu
 
Ccm wana mbinu mfuuu na ACT dhidi ya ukombozi wetu Mungu yupo nasi Amen
 
walaji kama wengine tu hakuna siasa Tanzania mnaongozwa na matukio tu...... siasa Tanzania imekufa kama chama mna mikakati gani ya kushawishi uma kuwa na ninyi na si kutafuta popul;arity kupitia migongo ya vyama vingine... ujinga tu huu. over bye...
 
walaji kama wengine tu hakuna siasa tanzania mnaongozwa na matukio tu...... Siasa tanzania imekufa kama chama mna mikakati gani ya kushawishi uma kuwa na ninyi na si kutafuta popul;arity kupitia migongo ya vyama vingine... Ujinga tu huu. Over bye...

kwanini mwiibe vifaa vya uenezi???
 
tujiulize maswali haya,
1. je hizo kadi ziliibiwa wapi?
2. kama ofisini, je mlikuta ofisi imevunjwa?
3. na kama ameporwa mwanachama wenu ilikuwaje tukio hilo la uporwaji?
4. ni nani mwenye mjukumu ya kusimamia hizo kadi zenu na alikuwa wapi wakati tukio linatokea?
lakini ninaweza amini kuwa mligawa kwa wanachama mliowalaghai, kisha wao wakaamua kufanya hvyo walivyofanya.

Huna ABC ya sheria! kwani jinai ya kuvunja unadhani mtuhumiwa mpaka ashike fatuma? Hata kusukuma mlango kisha ukaingia ndani tayari ni uvunjaji. Huyo kijana wa CHADEMA na viongozi wa CHADEMA waliomtuma wote ni wajinga kweli.
 
walaji kama wengine tu hakuna siasa Tanzania mnaongozwa na matukio tu...... siasa Tanzania imekufa kama chama mna mikakati gani ya kushawishi uma kuwa na ninyi na si kutafuta popul;arity kupitia migongo ya vyama vingine... ujinga tu huu. over bye...

tatizo maswali yangu wanakimbia, nawaambia njooni kwa wananchi, mbona mnapambana kwenye mitandao, na unakuta waanzisha mada wengine ni vijana wa ccm, wanabaki kutukana, mimi si mwanachama wa chama chochote ila nasikitika hizi siasa za maji taka zilivyo. watanzania si wajinga kwa sasa kiasi hiko, mtu anakuja kunifananisha na lissu badala ya kujibu hoja. twende mwaya kule kwetu kwenye mambo yalee kule.
 
Huna ABC ya sheria! kwani jinai ya kuvunja unadhani mtuhumiwa mpaka ashike fatuma? Hata kusukuma mlango kisha ukaingia ndani tayari ni uvunjaji. Huyo kijana wa CHADEMA na viongozi wa CHADEMA waliomtuma wote ni wajinga kweli.

kwanza sijasoma sheria na si mwanasiasa, ila ni mtaalamu wa masuala mengine na ndio ninayowasaidia vijana wenzangu kwa elimu yangu, baada ya kuona hamuwasaidii. pili jaribu kuelewa maswali yangu ndio ujibu, si unakurupuka kuja na ABC zako hizo za sheria, mimi nazijua ABC za HIV/AIDS. anza kusoma maswali ndio hujibu ndugu, ubongo wako usiliwe na mchwa wa siasa.
 
njoo na lissu mahakamani aulize maswali hayo,,, lakini wewe huwez,,, na huyo lisu ataumbuka tuu

swali huwa linaenda na jibu, si kwa porojo, pia mimi siwezi kuuliza, hapo juu ameuliza lisu? pia fahamu mimi si mwanasiasa ila kama mwananchi mwenye uelewa nauliza, sasa nyie mnajua bado mnawatawala wananchi wa zamani, halafu njooni huku kwetu mfanye mikutano huo uenezi upo mitandaoni tu?
 
Mwanachama wa CHADEMA, Thobias Sebastian anasakwa na jeshi la polis kwa tuhuma za kuiba vifaa vya uenezi vya ACT TANZANIA kadi na bendera. Ameiba vifaa hivyo na kuvipeleka kwenyue ofisi za chadema. Amefanya hivyo huku akidanganya umma kwa kusema kadi hizo zimerudishwa na wanachama, kadi gani ya kurudishwa haina jina, picha na sahihi ya afisa wa chama?

Huu wizi umefanywa kwa makusudi ili kukwamisha shughuli za uenezi wa chama chetu, na ikumbukwe kutengeneza kadi na bendera ni gharama, na kwa kiasi fulani huyu Bwa Thobias ametukwamisha kwani zile kadi zilihitajika sana Mbeya na wengi wamekosa kadi kutokana na kitendo chake hiki kishetani.

Kiogozi wa ACT mkoa wa Mbeya alilipoti polisi na ametoa taarifa kwenye vyombo vya habari na gazeti la JAMBO LEO LIMEANDIKA SEHEMU YA TAARIFA HIYO..

IFUATAYO CHINI NI SEHEMU YA TAARIFA YAKE KWA UMMA.

KATIKA hali ya kuonyesha ACT ni tishio kwa vyama vingine vya siasa, viongozi wa CHADEMA Mkoani Mbeya wamelazimika kuiba kadi za chama hicho kipya na kuzipeleka ofisini kwao ili ionekane kwamba zimerudishwa kwao na wanachama wa ACT.Tukio hilo lilitokea tarehe 9/8/2014 jijini Mbeya wakati wa sherehe za ufunguzi wa ofisi ya ACT-Tanzania Mkoa wa Mbeya.

Tukiwa kwenye sherehe za ufunguzi wa ofisi za chama chetu mkoa wa Mbeya, alitokea kada wa CHADEMA Thobias Sebastian ambaye hapo kabla aliwahi kufika katika ofisi za chama chetu kuomba uanachama wa ACT na kukataliwa. Kwa mara ya kwanza alifika ofisini wiki moja iliyopita na kuomba uanachama wa chama, ambapo kamati ya muda ya uongozi wa ACT Mbeya baada ya kujadili maombi yake ya uanachama ikajidhirisha kwamba Thobias hana mwenendo mzuri katika siasa za jijini Mbeya ilimkatalia kumpa uanachama.

Siku ya sherehe za ufunguzi wa ofisi za chama mkoa wa Mbeya tarehe 10/08/2014, kada huyo wa CHADEMA alionekana akiranda randa kwenye maeneo ya ofisi zetu. Mnamo majira ya saa 11 jioni wakati sherehe imeshika kasi na nje ya ofisi viongozi wa ACT wakiwa wanazungumza na wananchi waliojitokeza kwenye tukio hilo, ghafla tulimwona Thobias akitokea ndani ya ofisi zetu na kuanza kutimua mbio huku akiwa ameshika kadi mpya za ACT mkononi mwake. Viongozi kwa kuhofia kuharibu sherehe waliamua kwenda kuripoti tukio hilo kituo kidogo cha polisi Uyole. Na kwa uzito wa tukio lile na muda ule wa jioni, askari wa zamu alitupa maelekezo viongozi wa ACT kupeleka shauri kituo kikuu cha polisi jijini Mbeya siku itakayofuata. Tumekwisha ripoti kituo kikuu cha polisi na kupaitwa RB NO UY/RB/1815/2014

Pia tumesikitishwa na taarifa za upotoshaji na zisizofuata maadili ya uandishi wa habari kwa kutopata ufafanuzi wa upande wa pili na kupotosha umma wa watanzania zilioandikwa na gazeti la Tanzania Daima la tarehe 11/8/2014. Ni aibu kwa chombo cha habari kuandika habari inayojichanganya, sehemu moja wakisema kadi zilitupwa sehemu nyingine picha ikionyesha anayetuhumiwa kuiba hizo kadi akimkabidhi mbunge wa CHADEMA.

Tunaamini kwa kuwa jambo hili limeripotiwa kwenye vyombo vya usalama jijini Mbeya, sheria itachukua mkondo na vifaa vya ACT vitarudishwa na matendo haya ya kihuni yatakomeshwa kwenye siasa za Tanzania.

KATIBU WA ACT-TANZANIA
MKOA WA MBEYA.

Source: Facebook.
 
tujiulize maswali haya,
1. je hizo kadi ziliibiwa wapi?
2. kama ofisini, je mlikuta ofisi imevunjwa?
3. na kama ameporwa mwanachama wenu ilikuwaje tukio hilo la uporwaji?
4. ni nani mwenye mjukumu ya kusimamia hizo kadi zenu na alikuwa wapi wakati tukio linatokea?
lakini ninaweza amini kuwa mligawa kwa wanachama mliowalaghai, kisha wao wakaamua kufanya hvyo walivyofanya.

RB ni ya Tarehe Ngapi?
 
Back
Top Bottom