Polisi wamsaka kapteni mv spice islander

Paw

JF-Expert Member
Staff member
Joined
Nov 14, 2010
Messages
2,101
Points
1,500

Paw

JF-Expert Member
Staff member
Joined Nov 14, 2010
2,101 1,500
Developing story....
JESHI LA POLISI LAMSAKA KAPTENI WA MELI YA MV SPICE ISLANDER ILIYOZAMA BAHARINI

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi-Zanzibar

ZANZIBAR ALHAMIS SEPTEMBER 15, 2011.


Jeshi la Polisi nchini limeanza juhudi za kumtafuta kapteni wa meli ya MV Spice Islander iliyozama Baharini katika eneo la Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja usiku wa kuamkia Jumamosi September 10, 2011.

Taarifa ya Jeshi la Polisi iliyotolewa na Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa, imemtaja Kapteni wa Meli hiyo kuwa ni Said Abdalla Kinyanyite, ambaye ni mkaazi wa Nzasa Mbagala charambe wilaya ya Temeke jijini Dares Salaam.
Kamishna Mussa amesema kuwa Kapteni wa Meli hiyo, ambaye hakuweza kupatikana mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo , ni mwenyeji wa Kijiji cha Mbwemkuru tarafa ya Pande katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.

Kamishna Mussa amewaomba wananchi kupitia mpango wa Polisi jamuii na Ulinzi Shirikishi kutoa taarifa katika Kituo chochote cha Polisi endapo watapata taarifa za mahali alipojificha Kapteni huyo ili akatoe maelezo kuhusiana na jinsi ajali hiyo ilivyotokea.

Taarifa hiyo inasema kuwa tangu kuzama kwa Meli ya MV Spice Islander, Kapteni wa Meli hiyo hakuweza kupatikana hali ambayo iliyowalazimu Polisi kutafuta Picha yake kwa lengo la kurahisisha utambuzi kwa watu wasiomfahamu pindi wamuonapo.

0876 886488/ 0784 886488/ 0715 886488
 

Forum statistics

Threads 1,390,254
Members 528,131
Posts 34,047,420
Top