Polisi wamelielewa somo la 'Kwani wewe nani?'. Hongera sana Rais Samia

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,226
5,947
Leo katika mihangaiko yangu na kigari changu cha zamani nilisimamamishwa na polisi wa usalama barabarani kwa mbwebwe zao.

Akaniuliza kulikoni na kama nilikuwa na shida yoyote. Nikamjibu niko sawa. Akaniuliza mbona umewasha taa mchana kweupe hivi.

NIikamjibu sikujua kama taa zilikuwa zinawaka. NilIpo angalisha kiwasha taa nikaona kweli nilikuwa nimewasha.

Akaniambia tena naona kama taa yako ya kulia ina chongo- ni mbovu. Nikamwambia sikuwa najua hivyo. Akaniagiza kwa vile ninaenda mjini nikairekebishe mara moja. Nami pale pale nikampigia simu fundi wangu aje kazini kwangu airekebishe.

Nikakumbuka mukasa wa Mh. Rais- Mama Samia- naona somo lile kwani wewe nani- MIE SAMIA lilieleweka
 
Kwamba Hilo tukio halijawahi kukutokea kabisa traffic police kukuelekeza tu na akakuachia uende zako????

Kama jibu lako itakuwa ndio haijawahi kukutokea basi itabidi nikuulize swali jingine kwani umeanza kuendesha gari mwaka gani au kumiliki hilo gari lako lenye chongo?

Pia hivi pale kwenye dashboard so huwa inaonyesha green light symbol kwamba kunantaa zimewashwa? Au mpaka uangalie kiwashio sio???

Haya
 
Unashabikiaga Sana mwamba Mbowe kuonewa mahakamani. Hongera kwa kumiliki gari unatembea huku umekaa.

Wacha weeee!
 
Hivi kuwasha taa mchana ni kosa? mbona mimi naona kufanya hivyo ni usalama zaidi? coz hata Magari ya siku hizi yanakuja na zile daylight au kwa jina lingine zinaitwa Daytime running lights DRLs lengo ni ku increase the visibility of ur car,so other drivers can see you on the road.
 
Leo katika mihangaiko yangu na kigari changu cha zamani nilisimamamishwa na polisi wa usalama barabarani kwa mbwebwe zao.

Akaniuliza kulikoni na kama nilikuwa na shida yoyote. Nikamjibu niko sawa. Akaniuliza mbona umewasha taa mchana kweupe hivi.

NIikamjibu sikujua kama taa zilikuwa zinawaka. NilIpo angalisha kiwasha taa nikaona kweli nilikuwa nimewasha.

Akaniambia tena naona kama taa yako ya kulia ina chongo- ni mbovu. Nikamwambia sikuwa najua hivyo. Akaniagiza kwa vile ninaenda mjini nikairekebishe mara moja. Nami pale pale nikampigia simu fundi wangu aje kazini kwangu airekebishe.

Nikakumbuka mukasa wa Mh. Rais- Mama Samia- naona somo lile kwani wewe nani- MIE SAMIA lilieleweka
Ulikutana na mzimu, sio polisi hawa wanaokula kwa urefu wa kamba zao, huku kamba zao zikining'inia shingoni kama tai, hazijafungwa popote kuwadhibiti
 
Hivi kuwasha taa mchana ni kosa? mbona mimi naona kufanya hivyo ni usalama zaidi? coz hata Magari ya siku hizi yanakuja na zile daylight au kwa jina lingine zinaitwa Daytime running lights DRLs lengo ni ku increase the visibility of ur car,so other drivers can see you on the road.
Hii nchi imejaa siasa, dhuluma na kutengeneza mianya ya rushwa kwenye kila kitu. Wao wanaita kuchangamkia fursa
 
Hivi kuwasha taa mchana ni kosa? mbona mimi naona kufanya hivyo ni usalama zaidi? coz hata Magari ya siku hizi yanakuja na zile daylight au kwa jina lingine zinaitwa Daytime running lights DRLs lengo ni ku increase the visibility of ur car,so other drivers can see you on the road.
Mkuu hivi umeona mahala nimeandika aliniambia kuwasha taa mchana ni kosa?
 
Yaani taa zinawaka halafu dereva hajui?

Pengine haukuwa hata na dakika tano toka uanze safari.

Au na wewe ni chongo?
 
UMEJUAJE? UTAKUWA MTABIRI BAADA YA KIFO CHAKO
 
Mkuu hivi umeona mahala nimeandika aliniambia kuwasha taa mchana ni kosa?
Akaniuliza: "Mbona umewasha taa mchana kweupe hivi?"

Nikamjibu: "Sikujua kama taa zilikua zinawaka"

Sasa kama kuwasha taa mchana kweupe ni jambo la kawaida kwanini alikuuliza? na wewe kwanini ulimjibu kua hukujua kama taa zilikua zinawaka?
 
Zuga tu hiyo.. hakikisha taa unarekebisha hiyo jioni ukirudi unaye huyo.. anakusikilizia hatua chache ulipokutana naye
 
Akaniuliza: "Mbona umewasha taa mchana kweupe hivi?"

Nikamjibu: "Sikujua kama taa zilikua zinawaka"

Sasa kama kuwasha taa mchana kweupe ni jambo la kawaida kwanini alikuuliza? na wewe kwanini ulimjibu kua hukujua kama taa zilikua zinawaka?
Sasa hapo Kuna sehem kaambiwa ni kosa? Mtu akikuuliza kwann unakula umesimama wakati Kuna kiti Kwan anamaanisha kula umesimama ni kosa?
 
Sasa hapo Kuna sehem kaambiwa ni kosa?
Mtu akikuuliza kwann unakula umesimama wakati Kuna kiti Kwan anamaanisha kula umesimama ni kosa?
Ukiambiwa kwanini unakula umesimama wakati kuna kiti ina maana kula huku umesimama si jambo la kawaida,ukiambiwa kwanini umewasha taa mchana kweupe ina maana kuwasha taa mchana si jambo la kawaida,ndio maana nikasema nowadays magari yanakuja na Daylight coz tafiti zimeonyesha kua kuwasha taa mchana kuna fanya madereva wengine wakuone zaidi,

So,issue ya kuwasha taa mchana si jambo la ajabu tena kwa Dunia ya leo.
 
Huyu hakuwasha DRLs yeye aliawasha full beam headlight mchana ambayo siyo kitu Cha kawaida hasa kwa Tz kutokana na mazingira ukiona gar imewasha hivyo mchana labda ni sehem yenye ukungu sana wa baridi ambao unasababisha usione mbali au upo kwenye vumbi kali ili mtu akuone au gar limepata tatizo au kuna convoy ndo unaweza kuwasha full mchana kama ishara ya kua haupo kwenye hali ya kawaida, pengine ndo maana jamaa akamuuliza mbona umeiwasha taa mchana
 
Kwamba Hilo tukio halijawahi kukutokea kabisa traffic police kukuelekeza tu na akakuachia uende zako????

Kama jibu lako itakuwa ndio haijawahi kukutokea basi itabidi nikuulize swali jingine kwani umeanza kuendesha gari mwaka gani au kumiliki hilo gari lako lenye chongo?

Pia hivi pale kwenye dashboard so huwa inaonyesha green light symbol kwamba kunantaa zimewashwa? Au mpaka uangalie kiwashio sio???

Haya
Gari nimeendesha toka 1992. karibu swali la pili. hoja ya tatu, gari langiu usililinganishe na haya ya siku hizi. Usajili wake ni B na lilipokuja likuwa na miaka 20 toka litengenezwe
 
Back
Top Bottom