POLISI waliovuka Mpaka na Kuingia MALAWI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

POLISI waliovuka Mpaka na Kuingia MALAWI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Feb 16, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  CCM ing'olewe hakuna ubishi na hili hawa jamaa hawana faida hata chembe ,ile chembe ya faida hawana ,ndio maana juzi wamepewa kisago na wananchi wenye Uchungu na nchi yao pale Malawi ,wamekaa kimya ,hakuna anefurukuta si Waziri wa Ulinzi,Si Waziri Mkuu ,si Said Mwema si Raisi ,watu hawa wanne wanashindwa nini kuitisha uchunguzi wa ndani ya nchi na kuchunguza madai yaliojiri ? Nini kinawashinda ?

  Waziri wa Ulinzi hatujamsikia kusema kitu yaani inawezekana hata habari hana na imechukuliwa kama ni jambo jepesi.Jambo ambalo linaweza likazusha mtafaruku kwa uzembe wa polisi wala rushwa ,bado waziri amekaa kimya ,baba yke yupo atamlinda au sivyo ?

  Kuvuka mpaka na kuingia na uniform za Jeshi la Polisi katika Nchi nyengine sio mchezo si jambo la kusema tu ,wameshafahamiana ni kitu hatari kabisa ,Utawala wa CCM tulionao unatwambiaje WATANZANIA ? Kuhusu hili
  tumevamia nchi ya watu au sivyo?

  Wananchi wa Malawi wamewakamata wavamizi na kuwapa kibano kitakatifu na bunduki wamepokonywa ,Mkuu wa Jeshi la Polisi unatwambiaje kuhusu hili ? Na zaidi kuhatarisha amani ya nchi ,just Malawi kama angetaka kupakazia angesema majeshi ya Tanzania yamevamia Malawi na kuibua kwenye TV na kila kona ya dunia ,wangeliwabambikizia uwongo tu kama wao wanavyobambikizia watu mngesemaje ?

  Ila hii ndio utawala wa CCM wa kulindana yaani sasa hivi Serikali ya CCM inasubiri watu wapige makelele ndio utaona wanakurupuka ,uongozi gani huu ?
  Polisi waliovuka mpaka na kuingia Malawi na uniform za Jeshi wana kesi ya kujibu ,yaani hata kwenye mahakama za kijeshi ndio huko huko wakahojiwe na kiini kijulikane ,haya wamekaa kimya gazeti linaandika WaMalawi wafichua siri , hii kama si aibu ni kitu gani ? Wananchi tunahitaji maelezo.
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu Mwiba nakubaliana nawe kwa kiasi fulani na post yako.Ila tu sikubaliani jinsi unavyo liunganisha suala lenyewe na siasa, hususan CCM.
  Mimi si kwamba naitetea lakini sioni inavyoingia hapo moja kwa moja.
  Suala la askari wale ni kukosa nidhamu, period.
  Na inaelekea Kamanda Zelotte Steven ana suala la kujibu hapa.
  Hawa jamaa mpakani hapo hawana supervision ya aina yoyote.

  Kuonyesha askari hawa hapo mpakani ni sugu, niwaeleze kisa changu mwaka jana mwezi wa nane 2008.
  Nilikuwa sijawahi kufika Ileje ingawaje naenda sana Mbeya ,Tukuyu.
  Siku moja nikaamua kufika Ileje kwa njia ya kupitia KK,Chuo cha Magereza na kutokea njia panda Ilomba.
  Sikujua hii ni njia ndefu sana maana ni milima mikali na sikujua Tanzania ni nzuri huko juu, maana you are literaly on top of the mountains.
  Baada ya muda tulifika makao makuu ya Ileje ,Itumba,ambapo,tulikuta roadblock lakini hata hivyo hatukujali sana maana tulijua sisituko nchini mwetu hivyo tukashuka garini kupata soda baada ya mwendo mrefu.
  Hapo ndio tukanote funny movements , akatumwa askari mmoja toka roadblock kutuchunguza kama ni watanzania au la na akaondoka.
  Baada ya mapumziko kama ya dakika 10 tukaanza kuondoka, na pale roadblock sasa kukawa na askari kama wanne, wawili traffic na wawili kawaida mmoja sajenti, tukasimamishwa pale.

  Kama kawaida wakaniuliza vielelezo vya gari (ambalo ni 4WD na brand new), nikawapa.Mmoja akaniamuru kutoka kwenye gari na kujaribu usukani kama wheel lock iko dis abled kwa kuhofia kuwa sisi niwezi tunaotoka S Africa na hivyo tunatumia panya routes kupeleka gari aidha Mbeya au Zambia au kwingineko.
  Gari akaona liko ok na vielezo vyote vipo.Shida akasema gari bima imekwisha !!
  Hii baada ya kuona ni sis ni wabongo halisi na si wageni.
  Nikawahakikishia kwamba ni wenda wazimu tu kusafiri na gari mpya bila bima.Nikawa nimechokoza munkari.
  Nikaamrishwa kupeleka gari kituoni, maana bima wameshindwa kuona vizuri.
  Saahizo ni saa 10 nami naona mwendo nilioenda ni masaa karibu 5 hivyo ikabidi tuingie chemba.
  Wakataka laki moja!!!
  Nikawaambia kwa kosa lipi na lipi.
  Mmoja akasema huyu mjuaji peleka gari kituoni na tumfungulie charge.
  Sasa hapo ikabidi nitumie akili maana nikajua hawa wamezoea kuwa kamua watu huku na waliyokuwa wakifanya ni kweupee kwenye road block.
  Tukabishana juu ya dau tukaishia kuwapa elfu 20 iliyoniuma sana.
  Baada ya kukaa hapo karibu saa nzima wakaturuhusu, kabla ya kuondoka yule sajenti nikamwambia Bwana tutaonana tu si leo wala kesho tutaonana tu, Daslam wanakuja watu wengi tu pale kwa uhamisho, Hata Kamanda Kova kahamia hapo.
  Jamaa akaniuliza jina nikampa nami nikamuuliza la kwake, kwanza akan'gaka lakini baadaye akaniambia.
  Jina hilo nalifahamu sana.
  Nikamwambia si fulani katika Idara fulani ya Serikali ni ndugu yako?
  Sajenti akatweta.
  Ee bwana nihifadhi mdogo wangu yule.
  Nami kumhakikishia nikampigia simu ya mkononi ndugu yake tuakongea na nikampa Sajenti aongee naye.
  Askari akatweta kweli kweli na kuomba radhi nami nikamuachia kwa kuwa kiendacho kwa mganga..
  Somo nililopata hapo ni kuwa Askari kwenye vituo hivi vya mipakani pamoja na kupewa madaraka makubwa ya ulinzi wa nchi lakini wanatumia madaraka yao kwa kuendekeza ufisadi.
  Haw wa kuingia Malawi sasa hiyo ni balaa tupu!
  Kamanda Zelotte tupia macho hapo.
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  CCM inaingia hapo kama Chama Tawala ,polisi wao wana yaokama ni chombo cha dola lakini cha kujiuliza nani sasa hivi ni dhamana wa Taifa hili la Tanzania na vyombo vyake vya dola? Kama nchi itavurugika kwa uzembe wa polisi ambao wanalipwa na serikali ya CCM basi ,wakulaumiwa ni Viongozi wa juu ambao mmoja wao ni mwenyekiti wa CCM na sera za Serikli ni za CCM,Chama kilichounda serikali ndio mhusika mkuu ,hivyo serikali ya CCM ndio ya kuwakemea na kuhakikisha sheria zinafuatwa na kulindwa ,polisi wamevuka mpaka nani amewaruhusu , Jemedari Mkuu anasemaje hapo atakubali kama yeye alitoa ruhusa ? Nini walifuata ? Nini matokeo ? Wamekamatwa wamepigwa na silaha wamepokonywa au sio hiyo ni aibu au si aibu ? ,maana hivi sasa huwezi kwenda Malawi wasitucheke ? Na sababu ya kutucheka wanayo.
   
Loading...