Polisi waikimbia masasi baada ya kukosa posho.

Polisi waikimbia masasi baada ya kukosa posho.

Ukana Shilungo

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2012
Posts
3,041
Reaction score
2,423
wanajamvi heshima kwenu !,polisi ambao walipelekwa masasi,toka mtwara mjini, lindi na dsm,ambao walitumwa rasmi kwenda kuongeza nguvu mara baada ya vurugu zilizokuwa zimetokea. Zilizosababisha kuchomwa moto ofisi na magari ya serikari na chama cha ccm.
Askari hao wameondoka mjini masasi baada ya kuona maisha magumu, kuishi bila kulipwa posho ambazo inasemekana ni shilingi 40,000/= kwa siku kwa askari mmoja,na walipaswa wakae angalau miezi miwili .inasemekana pesa zilitengwa kwa mpango huo maalumu ,zimeliwa na vigogo wa polisi,jambo lililosababisha askari hao kuamua kurudi katika maeneo yao ya kazi kinyemela kuliko kuishi maisha magumu na mazingira hatarishi ya uadui na raia.
Source mimi mwenyewe nimeongea na mmoja wa askari aliyekuwepo kwenye operesheni hiyo na ambaye tayari amerudi toka masasi na kwenda kituo chake cha kazi.
 
Hiyo ndiyo zawadi ya wanafiki, kulinda maslahi ya vigogo wanaotafuna rasilimali za nchi.Hakika hao Policcm mwaka 2015 watavua gwanda na kukimbilia uhamishoni,huku wakiwaacha mabwana zao wakihukumiwa na raia.
 
Siku zote mtu mwenye nia mbaya hujikuta anaumbuka.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Tsh 40000 per diem?wakati kigogo bandari tsh 600000 per diem
 
Hiyo ndiyo zawadi ya wanafiki, kulinda maslahi ya vigogo wanaotafuna rasilimali za nchi.Hakika hao Policcm mwaka 2015 watavua gwanda na kukimbilia uhamishoni,huku wakiwaacha mabwana zao wakihukumiwa na raia
Ndio hivyo mkuu hali ni tete,hata polisi wenyewe amba Masasi ni sehemu ya ya kazi wanaishi kwa tahadhari kubwa mana madereva wa bodaboda bado wana hasira mno.
 
sifikiri kama Chagonja ana taarifa, inaweza kuwa magumashi haya yanafanyika bila yeye kujua hilo,na jeshini ni nidham inatawala ,hivyo hawa askari wadogo hawana mahali pa kupeleka manung'uniko yao nadhani.
 
Wanafiki hao. Kwanini wasianze kugomea madai yao ya siku nyingi kuhusu kuboreshewa mazingira ya kazi ikiwemo makaazi, vifaa bora na vinavyoenda na wakati?
 
Tsh 40000 per diem?wakati kigogo bandari tsh 600000 per diem
Ndio mkuu walipaswa kupewa laki tano kwa awamu ya kwanza,kinyume wakapewa 100,000/= kwa mkupua wa kwanza yani ni kama pesa ya siku mbili,hivyo ndivyo serikari inavyowatania wana usalama.
 
Ivi kwnn askar wasigome kama walivyofanya wa south africa mpka serikali ikasurrender na kuwapa wanachokitaka!!! Askar wana2mika kuwalinda wakubwa 2 af wenyewe wakibak na maisha dunii,, polen cna
 
kuna gazeti moja lilitoa makala ya kuwashawishi askari kugoma likafungiwa! ata mimi nashauri wajeshi wote wagome maana serikali tawala imekuewa ikitoa mashalahi makubwa kwa wenye vyeo vikubwa ili wawatumikishe hawa wadogo!
 
wanajamvi heshima kwenu !,polisi ambao walipelekwa dmasasi,toka mtwara mjini, lindi na dsm,amddbao walitumwa rasmi kwenda kuongeza nguvu mara baada ya vurugu zilizokuwa zimetokea. Zilizosababisha kuchomwa moto ofisi na magari ya serikari na chama cha ccm.
Askari hao wameondoka mjini masasi baada ya kuona maisha magumu, kuishi bila kulipwa posho ambazo inasemekana ni shilingi 40,000/= kwa siku kwa askari mmoja,na walipaswa wakae angalau miezi miwili .inasemekana pesa zilitengwa kwa mpango huo maalumu ,zimeliwa na vigogo wa polisi,jambo lililosababisha askari hao kuamua kurudi katika maeneo yao ya kazi kinyemela kuliko kuishi maisha magumu na mazingira hatarishi ya uadui na raia.
Source mimi mwenyewe nimeongea na mmoja wa askari aliyekuwepo kwenye operesheni hiyo na ambaye tayari amerudi toka masasi na kwenda kituo chake cha kazi.
Unreliable source
 
Nakumbuka wakati wa uchaguzi wa 2010 askari waliokuwa wanalinda kura kituo cha loyola, Mnyika aliwaambia kuwa anajua kuwa wanalinda maslahi ya wakubwa lakini atakaposhinda na kuwa ubunge atahakikisha anapiginia haki zao Hebu kama askari mpo humu mkumbusheni ahadi yake.
 
Back
Top Bottom