Polisi waibiana Sh3 bilioni za posho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi waibiana Sh3 bilioni za posho

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Apr 15, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Salim Said
  SIRI ya kuchelewa kwa posho za askari polisi mwezi Febuari mwaka huu imefichuka baada ya kudaiwa kuwa maafisa watatu wa jeshi hilo walitoweka na hundi ya malipo hayo yanayofikia Sh3 bilioni.

  Baadhi ya maofisa wa polisi waliozungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti wiki hii, walielezea mazingira ya wizi huo na kusisitiza kuwa ngazi ya juu ya jeshi hilo imekuwa ikificha taarifa hizo, kwa hofu ya kuchafua sifa ya chombo hicho cha dola.

  Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina yao gazetini, walisema fedha hizo ziliibwa na maofisa hao watatu baada ya kubadili maelezo kwenye hati ya malipo na kuielekeza katika akaunti za mmoja wao.

  Wakadai kwamba, kilichosababisha siri hiyo kufichuka ni baada ya kuchelewa kwa posho hizo na kusababisha baadhi ya askari hao kuanza kulalamika kwa maofisa wao wa juu.

  Askari hao ambao baadhi walifika kwenye ofisi za gazeti hili walisema, kwa kawaida posho hizo zinatakiwa kutoka tarehe 15 ya kila mwezi, lakini mwezi Februari zilichelewa hadi Aprili 9 mwaka huu.

  "Awali IGP alikanusha tuhuma hizo, lakini ni kweli zilipotea kwa sababu askari watatu waliotuhumiwa kuhusika walikamatwa na kupelekwa kizuizini katika vituo vya Msimbazi na Salenda Bridge vya jijini Dar es Salaam," mmoja wa askari hao alisema huku akihoji:

  "Sasa askari wanajiuliza kwamba, kama IGP alikanusha tuhuma za wizi huo, kwanini askari hao walikamatwa?"
  Juzi, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema alikataa kuzungumzia kukamatwa kwa polisi hao, ingawa Aprili 8, mwaka huu alikiri kupata malalamiko ya askari kuhusu tukio hilo.

  Afande Mwema akalitaka gazeti hili liwasiliane na Msemaji wa Jeshi la polisi nchini, Kamanda Abdalah Mssika kwa maelezo zaidi kuhusiana na suala hilo.

  Hata hivyo, Mssika alishindwa kutoa maelezo ya kina kuhusu tukio hilo akisema hakuwepo ofisini muda mrefu kwa sababu za kiafya.

  Mimi sina taarifa yoyote kuhusu tukio hilo, kwa sababu nipo katika matibabu, sipo kazini, lakini nipe muda niulizie halafu nitakujibu, naomba namba yako ya simu ya mkononi, alisema Mssika.

  Kwa muda wa siku wa mbili tangu aahidi kumpigia simu mwandishi, Kamanda Mssika hajapiga simu na alipopigiwa tena alisema: "Siwezi kukusaidia kwa hilo sasa, bado niko kwenye matibabu lakini suala hilo naendelea kulifanyia kazi."


  Taarifa zaidi zimeeleza kuwa askari hao walikamatwa baada ya akaunti ya mmoja wao ambaye ni mwanamke kukutwa na kiasi hicho cha fedha na kushindwa kuzitolea maelezo ya kuridhisha.
  Kinachoumiza zaidi ni kwamba posho zetu zimechelewa na aliyechelewesha amebainika halafu anawekwa ndani kwa muda mfupi na kuachiwa bila ya kuchukuliwa hatua,alilalamika askari mwingine aliyezungumza na gazeti hili.

  Alisema hivi sasa maslahi ya polisi yamekuwa tatizo; posho zinachelewa, nafasi za masomo kwa askari wa kawaida hakuna na hata kupandishwa vyeo ni shida kwao.

  Posho ya uhamisho ni haki yako, lakini polisi tunafahamishwa na kila siku tunasafiri kwa fedha zetu. Tukifika tulikohamishiwa inaweza ikapita hata miezi miwili bila kupewa posho ya safari, alisema mmoja wa askari hao na kuongeza:
  Askari unalinda nyumba za viongozi, maofisi ya viongozi, lakini hata ukiomba maji katika nyumba za viongozi hao hupati, achilia mbali chakula. Tunalinda huku tukiwa na njaa.

  Taarifa zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kwamba, ingawa baadhi ya askari polisi jijini Dar es Salaam wameanza kupata posho zao za Februari, maeneo mengi ya Tanzania Bara na Visiwani hazijaanza kutolewa.

  Baadhi ya mikoa ambayo askari wake waliliambia gazeti hili kwamba hawajapata posho, ni Tarime-Rorya kwa Tanzania Bara na baadhi ya mikoa ya Zanzibar hawajapata posho hizo.

  Hadi sasa ndugu mwandishi hatujapata posho yetu, tunateseka kweli, tunaishi katika hali ngumu," alisena polisi mmoja wa Tarime.

  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alipoulizwa kuhusu kukamatwa kwa maofisa wa jeshi hilo wanaodiwa kuiba fedha hizo, alikataa kuzungumza kwa maelezo kuwa suala hilo liko juu ya uwezo wake bali aulizwe afande Mssika.

  Hili suala Mwananchi halipo katika mamlaka yangu, mpigie Mssika. Unataka niseme jambo halafu nionekane sielewi majukumu yangu, alisema Kova.
  Aprili 8, mwaka huu IGP alikiri kupata taarifa za wizi huo kutoka kwa baadhi ya askari wake ambao pia walimtaka achunguze kuhusu tukio hilo.
  Lakini baadaye alikanusha wizi na kueleza kuwa posho zao zilicheleweshwa kutokana na matatizo ya kiutawala na mahesabu.
  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=19225
   
 2. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2010
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  balaa kubwa hilo. kama wenyewe wanaibiana je sisi wengine itakuwaje?
   
 3. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  afadhali sasa wakiaanza kuibiana wenyewe kwa wenyewe mitaani wizi utapungua ss
   
 4. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,122
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Unaweza kuelekeza 3 billion kwenye account yako? Hairaise alarm zozote kwenye banking procedures? Na zaidi ya hapo unazitoaje hizo 3 billion bila watu kushtuka?
   
 5. N

  Nanu JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kikulacho kinguoni mwako!!!!!!
   
 6. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  napatwa na wasiwasi pia. milioni 100 tu ikiingia kwa pamoja kwenye akaunti yako ya akiba unapigiwa simu na manager!, bil3 kwenye savings?.....duh.
   
 7. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kichwa cha hii habari kina uata....mwandishi hawezi kusema Polisi "WAIBIANA".
   
 8. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hakuna kushangaa hapa.hao tulisha wazoea hakuna uaminfu tena.wana kwiba mpaka vitu vya ushahidi.
   
 9. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,860
  Trophy Points: 280
  Asemeje?
   
 10. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #10
  Apr 16, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Lile ni kundi la wahuni, si tunakaa nao mitaani, wauza unga wao, bangi wao, pombe haramu wao,wizi wa kura wao,ujambawazi wao, uporaji wageni wao, kila aina ya uchafu wao. Wananichefuachefua saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana
   
Loading...