Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Shangwe Ayo, Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma wa ACT Wazalendo na Waziri Kivuli wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), ametangaza kuwa Polisi wamevamia ofisi za chama hicho na kumkamata Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake Taifa, Janeth Rithe.
Shangwe ameandika kuwa polisi wamedai kuwa wanatekeleza agizo kutoka kwa ZCO (Ofisa Upelelezi wa Mkoa). Hata hivyo, haijabainika wazi ni kwa sababu gani kiongozi huyo wa wanawake anatafutwa na vyombo vya dola.
Janeth Rithe pia amethibitisha kupokea ujumbe kuhusu kutakiwa kwake na Vyombo vya Usalama, akisema: "Ni kweli nimeletwa ujumbe kwamba nahitajika, ndiyo naelekea kwa ZCO."
Janeth Rithe pia amethibitisha kupokea ujumbe kuhusu kutakiwa kwake na Vyombo vya Usalama, akisema: "Ni kweli nimeletwa ujumbe kwamba nahitajika, ndiyo naelekea kwa ZCO."