Polisi wadaiwa kuua raia Mbeya.

Polisi wadaiwa kuua raia Mbeya.

lukanima

Member
Joined
Apr 6, 2013
Posts
52
Reaction score
34
Mbeya. Polisi mkoani Mbeya wanatuhumiwa kumshushia kipigo Barnabas Kahemele akiwa mahabusu na kusababisha kifo chake.

Kufuatia tukio hilo, ndugu wa marehemu Kahemele wamegoma kuuchukua mwili wa marehemu huyo uliohifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Rufaa Mbeya wakidai kwamba mazingira yanaonyesha kuwa kifo chake kimetokana na kipigo cha polisi baada ya kumkamata.

Inadaiwa kuwa marehemu na wenzake wawili walikamatwa usiku ya Jumatano wiki hii, baada ya askari hao kufika nyumbani kwa marehemu, eneo la Uyole ya Kati. Mke wa marehemu Sara Muhwanji, alidai kuwa wakiwa wamelala walisikia mtu akigonga hodi na ndipo alipoamka na kutoka sebuleni.

“Nilitoka sebuleni na kuuliza nani anayegonga, ndipo nikasikia sauti ya mtu anasema kuwa mimi Mhagama, huyo ni jirani yetu pale nyumbani. Lakini sikufungua mlango na nikaenda kumwamsha mume wangu, naye akauliza nani jibu likawa mimi Mhagama nina shida, fungua mlango. Ndipo marehemu alipofungua mlango, polisi wanne wakaingia ndani na kumwambia kuwa yupo chini ya ulinzi,” alisema Sara.

Alifafanua kuwa baada ya hapo polisi hao waliondokana naye na kwamba alipojaribu kuhoji kosa alijibiwa kuwa afike polisi asubuhi ataambiwa kosa la mume wake. “Nilipofika asubuhi ambayo ni juzi Alhamisi nikauliza mapokezi na kuwaambia kuwa nimekuja kumwona mume wangu, askari wa mapokezi wakatafuta jina lake lakini hawakuliona,” alisema.

Alieleza kuwa baada ya hapo askari walimfuata na kumchukua, kisha kumpeleka ofisi zilizo ghorofani na wakamwingiza kwenye chumba cha mahojiano, ambapo alihojiwa na askari wa kiume.

Alisimulia kwamba baada ya kumaliza walimtaka aendelee kukaa kituoni hapo akisubiri taratibu zinazoendelea kuhusu mume wake.

Alisema kuwa baada ya muda mfupi majibu yakawa tofauti na kuambiwa kuwa imetokea bahati mbaya mume wake amefariki dunia.Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki alipohojiwa kwa njia ya simu kuhusu tukio hilo alisema kuwa hana taarifa.
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi (April 13 2013) Polisi wadaiwa kuua mtuhumiwa kituoni - Kitaifa - mwananchi.co.tz

 
Inasikitisha sana kuona maisha ya mtanzania hayana thamani. Haki ya mtu kuishi si tena jambo la maana kwa polisi Tanzania. Hili si tukio la kwanza: wengi wamepoteza maisha mikononi mwa chombo cha "usalama". Hili suala si la kufumbia macho maana halikubaliki hata kidogo. Hatutashangaa kusikia hao hao "wana usalama" wanaunda tume "kujichunguza". Ni jambo la huzuni sana mke wa marehemu anavyosimulia jinsi alivyopewa taarifa za kifo cha mumewe. Yeye alikwenda kujua sababu za mumuwe kukamatwa lakini akaishia kuambiwa "ameshafariki". Ama kweli Tanzania kuna "amani!!!"
 
hii ni mbaya sana na kimcngi c hii moja zipo nyingi watanzania tuwe macho kujua haki zetu na wajibu wa polic c jambo jema mwana usalama kusababisha kifo cha makusudi
 
Tunaona watu wanavyouwawa kinyama tuko kimya tukisubiri ndugu zetu wauwawe ndiyo tupase sauti, watanzania tuacheni ubinafsi wanaouwawa ni binadamu kama sisi ni watanzania kama sisi wanauliwa na watu wanaopaswa kulinda usalama wao..tukatae uhuni huu
 
Nafkri sasa imefika mwisho wa uvumilivu, inakuwa vip jamani kama tumelogwa, watu wanauwa na polisi lakini bado tunakaa kimia. jamani ifike mahali tuache tofauti zetu tutetee uhai wetu kwa umoja. leo amekufa huyo kesho mimi au wewe tunakwenda wapi. Haya ndio mambo muhimu ya kuungana hatuweze kuendelea kuvumilia. Maisha hayana spare na kila mtu anahaki ya kuishi hata kama ana makosa. kwanini polisi inakua sio mahali salama tena. Mie na fikri huu utawala zalimu kiasi hiki una mwisho wake na haya matukio lazima yawekwe kwenye kumbukumbu ili siku itakapofika huyo mkuwa wao atajibika kwa damu zilizomwagika chini ya utawalawa wake bila hatia. a day is coming our children and grand children will note this terrible system. Its so painful, juzi tu dar mwingine alitwesa polisi dar- long number of such events. Mungu amlaze pema na kuwapa faraja mke na watoto wa marehemu. Lakini naona kunahaja ya kutumia Jamii forum as a place to moblize and take action huku watawala wakielewa what is going on. this is too much haiwezi kuvumilika. Napata hasira hii ni Tanzania au ni kitu gani. Mie nafkri mashirika vyama mbalimbali ni muda kuungana na kutetea haki yetu ya kuishi hatuweze kufanya hili jambo kuwa mazoea. kila mahali tunaharibu tunakwenda wapi? lets join our hands
 
Hivi ni hadi lini watanzania tutaendelea kudhulumiwa na polisi wanaolipwa kwa fedha zetu wenyewe?
 
Kwa mbeya mbona wengi sana wameuawa na polisi? Kwan Kahemele ni wa Kwanza? NCH YA TANZANIA
 
Kwa mbeya mbona wengi sana wameuawa na polisi? Kwan Kahemele ni wa Kwanza? NCH YA TANZANIA

Sasa tufanyeje kusudi wasiendelee kufanya unyama na uzandiki huu kwa raia wenzetu mkuu
 
Yote hii ni mfumo mbovu
wa serikali. Wewe angalia ni idara gani ya Seirikali inayofanya kazi katika kiwango kinachokubalika ama misingi ya hakii?st

Ni system ndiyo maana serikali inaona sawa na ukianza kupiga kelele wakikufahamu lazima wakushughulikie.

NASISITIZA DAWA YA YOTE HAYA TUNAYOYAONA NI KUINDOA CCM MADARAKANI ILI IUNDWE SERIKALI MPYA YENYE MFUMO MPYA WENYE VIWANGO SAHIHI VINAVYOPIMWA NA KUSIMAMIWA IPASAVYO. VINGINEVYO CCM NDIYO IMETUFIKISHA KWENYE HILI KABURI.
 
Wakati huyu mpangaji wetu wa magogoni anaanza kazi nilikuwa na imani kwamba zile enzi za Mahita ndiyo mwisho wake,lakini hakuna kipindi nilichoshuhudia ukiukwaji wa haki za binadamu wa hali ya juu kama kipindi hiki cha awamu ya nne.Inasikitisha sana.
 
Jamani watanzania tusiwe RADICALZ Polisi(kama taasisi) haiwezi kuua raia. Kuna usemi usemao '' guns never kill people,but people kil people. Tafakari,..
 
Lazima watakuwa wametumwa na CHADEMA hahahahaaaaaaaaaaaa its only joke
 
Huu upuzi wa 'hiki ni kisiwa cha amani' uantumika kuwatakasa wakubwa kwa gharama za roho zetu...naona sasa niwakati wa "liwalo na liwe" ili wajue sisi siyo makondoo...wameisha ona ni kam kamchezo
 
Jamani watanzania tusiwe RADICALZ Polisi(kama taasisi) haiwezi kuua raia. Kuna usemi usemao '' guns never kill people,but people kil people. Tafakari,..

Hujaeleweka jombaa!hivyo unapinga kuwa si polisi waliyemuua/wanayeua raia?eti people kill people,so what's your point here?that police are not among the people? The truth is Police use their guns to kill people!!nothing more nothing less.
 
Back
Top Bottom