Polisi wa pikipiki kazi yao ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wa pikipiki kazi yao ni nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jahom, Dec 1, 2009.

 1. J

  Jahom JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2009
  Joined: Aug 26, 2008
  Messages: 349
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hawa jamaa wenye pikipiki na mavazi mazuri, wakiwa na bunduki zenye akili nilidhani ni askari polisi wa kudili na ujambazi na kwamba wanatumia pikipiki ili kufika sehemu ambazo gari isingefika haraka kutokana Traffic jam.

  Sijasikia hata kazi yao moja yenye akili. Labda sijui hasa kazi yao nini kwa kuwa mara nyingi naona wanafanya bargaining njiani na watu ambao huhitaji bunduki kuongea nao. Tunaenda wapi? Tumwambie nani kuhusu hili kwa kuwa sina imani kuwa wakubwa wao hawajui kama hawa jamaa wanavizia madili tu na kwamba huenda ndio malengo waliyowekewa. Siwapendi!!!
   
 2. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wanaonekana ni majambazi pia! Siku moja nimepakia maharage kwenye gari yangu ndogo ndani ya buti natoka Ally Hasani Mwinyi road naingia kanazi street jamaa hawa hapa "wanauliza eti nimebeba nini nikawaambia maharage, fungua tuone nikawaonyesha" sasa kwa hali ya kawaida jambazi hafuatwi hivyo! kweli wanavizia dili tu njiani " HATA MIMI SIWAPENDIIII"
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mmewaita mahali wakashindwa kushughulikia ishu?

  Au unakerwa kuwaona wanapiga misele vile?

  Na zile ishu zinazotangazwa kila mara na Afande Kova kwenye runinga una uhakika gani si za hawa jamaa?

  Au kila wakishashughulika wakubip?
   
 4. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  nimekuwa nikijiuliza mara nyingi sana bila kupata jibu la uhakika kuhusiana na hawa askari, kwanza badala ya kuwa msaada wao wapo ktika kukutisha zaidi, wanaweza wakakusimamisha kwenye gari kabla hamjafanya chochote wao wanakuwa wamesha jiandaa kukuua, yaani kama hawana umuhimu wowote kwa jamii
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Dec 1, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  ni njaa yao tu, maana Wajibu wao ni doria dhidi ya majambazi sio kupambana na wahuni wa daladala, hii inafanana na wale Police pale NMB Bank house hapo DSM , wanakalia kukamata gari zinazovunja sheria ya one way pale Samora..ni hatari na hawa wanaganga njaa.
   
 6. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #6
  Dec 1, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Nenda pale TAZARA nyuma la jengo la RTD utawakuta wametia kitako hapo, pita basi mara wakague stika mara tairi utadhani wao ni trafiki! Halafu nasikia hao ndio wa mwisho kwenye masomo ya uaskari
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Dec 1, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  jamani mnaweza kuta ni MFBI hao ndo maana wanazunguka zunguka tu
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Dec 1, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  FBI wanahangaika kutwa na daladala, aah wacha masihara. nnchi ya kitu kidogo hii, iko siku na mgambo wa jiji utawakuta wanakamata na kutoza faini daladala na gari korofi, mambo habelahobela kil mtu na lwake.
   
 9. H

  Hashim Mohamed Member

  #9
  Dec 1, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wana JF nadhani tunaongozwa na hisia zetu zaidi katika mijadala kuliko uhalisia wa mambo. Kazi ya polisi ni kusimamia sheria ya nchi zisivunjwe bila kujali ni sheria ya usalama barabarani au ya makosa ya jinai. mi nadhani tusiwalaumu kwa kushughulukia makosa madogo badala yake tuwatie moyo pamoja na madogo pia waongeze bidii katika makubwa.

  Ila matatizo makubwa niliyoyaona katika hili ni wao wenyewe kuvunja sheria wakati wa ukamataji kwa kuomba rushwa.

  Na katika hili nadhani itakuwa vema kama tukitafuta namna ya kufikisha kilio chetu kwa viongozi wao ili kuwachukulia hatua za kinidhamu.
   
 10. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #10
  Dec 1, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  tatizo umesahau kuna mgawanyo wa kazi ndani ya Jeshi, lazima uconcetrate kwenye eneo lako la kazi maana utendaji na ufanisi wako utapimwa hapo.
  sasa kama kutwa unasurvey barabarani, aah Jambazi hapori barabarani, wako mitaani na kwenye maduka makubwa ya thamani na mabenki. sasa kama alivyoeleza ndugu huko juu, kuwa pale Tazara kutwa wameganda katika miti wakivizia daladala,.
  hawa wanahangaikia kitu kidogo,zipo tetesi kua wanatengeneza vitabu vyao vya receipt siku hizi, wakitoza faini ile ya juu kwa juu wanajiandikia humo na hawa submit hiyo pesa...aibu.
   
 11. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #11
  Dec 1, 2009
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,167
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Nilitoka Tanga hivi juzijuzi, jamaa wanawaita hawa askari TIGO. Hivi kwa wale wa2 wa huko kwa nini munawaita tigo?
   
 12. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #12
  Dec 1, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,364
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Teh teh teh,wachamehe njomba,hawajui wachemaloo!!
   
 13. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #13
  Dec 1, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Sio FBI hawana hata dalili zozote, mimi wamewahi kunitoa 3,000/ nilikuwa naendesha pikipiki bila helmet (kofia) unaona walivyo na njaa, lakini nashukuru Mungu, wamekuwa wanakimbiza pikipiki, na kutokuwa na uzoefu wa barabara, wanaanguka na kufariki,

  Natamani wafe wote waishe wabaki wale wenye faida na jamii tu.
   
 14. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #14
  Dec 1, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu Nguvumali,

  Ni kweli kabisa hawa police walinikamata siku moja eti nimevunja sheria ya one way na walitaka niwape chochote ili wasinipeleke central police station. Niligoma kutoa rushwa na nikawaambia niko tayari wanipeleke lakini ajabu hakuna mmoja wao aliyekubali kuingia kwenye gari twende kituoni.

  Hao police wa pikipiki kwa kweli wakati mwingi hawafuati majambazi wala nini. Siku moja nilikuta wamepack pikipiki yao mahali wakanisimamisha na kuniuliza kwa nini sijafunga mkanda, you can imagine ilikuwa ni kwenye barabara ya vumbi huko maeneo ya mabibo. Nikawauliza kama wanajua maana ya kufunga mkanda na kwa nini uwa tunafunga mkanda. Wakasema hiyo ni sheria. Nikawaambia hiyo sheria naijua sana lakini katika barabara ile iliyojaa maandaki siwezi kuendesha kwa kasi zaidi ya KM 10 kwa saa nafunga mkanda wa kitu gani?

  Utendaji wao inabidi uangaliwe upya. Kwa sasa wanaganga njaa badala ya kufanya kazi tulinayotarajia wawe wanafanya.

  Tiba
   
 15. M

  Mundu JF-Expert Member

  #15
  Dec 1, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kazi yao ni kula rushwa tu. kila siku kuwapiga mabao waendesha magari hususan dldl. Wanafanya kazi za askari wa usalama barabarani. Tofauti ni kuwa wanabeba bunduki za kuulia.
   
 16. J

  Jahom JF-Expert Member

  #16
  Dec 1, 2009
  Joined: Aug 26, 2008
  Messages: 349
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Thoughts become things when are operationalised. Hisia hazitoki kwa alinacha, bali ni kwa mambo yanayotuzunguka. Shughuli ngapi za majambazi zimekamilika mchana kweupe na wao kujificha? (TKM NMB walikuwa wapi?) Au walikuwa wanapambana na majambazi wengine ambao record hazipo? Unahitaji bunduki kukamata stika, asiyefunga mkanda, aliyebeba maharage, asiyevaa helemet n.k? Kuna tatizo limeachwa kwa makusudi na hao unaodhani wanaweza kuchukua hatua za kinidhamu.
  Askari hao wamekuwa kero kuliko kutokuwepo. Walinikamata wakaniacha kwa kauli "hana hela achana naye"
   
 17. nyaunyau

  nyaunyau Senior Member

  #17
  Dec 1, 2009
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  WanaJF Askari hana mpaka katika kazi,ukamataji wa makosa ni wajibu wa kila askari awapo kazini au offduty ni kwa makosa yote yanayotendeka mbele yake kukamata na kufikisha kituoni kwa hatua zaidi za kisheria,kero kubwa ni ukamataji wa makosa kwa nia ya kujipatia chochote toka kwa mtuhumiwa.
   
 18. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #18
  Dec 1, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160

  Mundu Umemaliza! wale ni rushwa tu
   
Loading...