Hili suala hata mimi linanipa wasiwasi,majambazi wanafanya vibaya kuua watu,lakini polisi wasijisifie kuyaua majambazi kwani wanahalalisha sheria mkononi. Kama kuna uwezekano wa kuyakamata yakamatwe.
Nashukuru wote kwa michango yenu. Ila swali bado halijapata jibu.
Unapozungumzia swala la kujibizana kwa risasi hii inamaanisha ni mapambano ya kutetea uhai. La kushangaza na nielewavyo mimi kuwa jambazi kama jambazi ni mtu ambaye anakuwa amejiandaa vilivyo ili kutimiza azma yake.
Naomba nitoe mifano ya kujibizana risasi ambapo jambazi hakuuwawa, Kumbukeni tukio la ubungo junction, pale mapambano yalikuwa ni dhahiri ila jamaa hakuuwawa.
Haya matukio mengine kama ya Dodoma (last year) na Moshi (recently) yamenipa wasi wasi mpaka nikaona ni vyema tujue ukweli kuhusiana na visa hivi.
Inakuwaje jambazi anapigwa risasi ya kichwa katika majibizano au ina maana askari wanashabaha pasi mfano, au jambazi anapigwa risasi mgongoni. Jamani eeh, tutafute ukweli wa mambo
Hiyo mbona simpo kuna majambazi baada ya kuona mapambano yamekuwa makali huwa yanaamua kukimbia/kulala mbele pale ndipo polisi huyatungua kwa nyuma, hiyo possible kabisa wala haina shaka, na ujue hapo kulikuwa na resistance flani ya hatari ya kuuana hivi.
Katika siku za karibuni kumekuwa na habari mbalimbali zikiripotiwa kuwa Polisi wamefanikiwa kuyaua Majambazi kadhaa katika matukio ambayo yalisababisha kurushiana risasi.
Jambo linalonishangaza ni kuwa,
"Je, kunakuwa na ni nani hasa anatakiwa kuthibitisha maelezo yanayotolewa na Polisi?"
"Hivi inakuwaje ni Majambazi tu ndio wanauwawa na sio Polisi katika matukio ya kurushiana risasi?"
Nawasilisha.
Katika siku za karibuni kumekuwa na habari mbalimbali zikiripotiwa kuwa Polisi wamefanikiwa kuyaua Majambazi kadhaa katika matukio ambayo yalisababisha kurushiana risasi.
Jambo linalonishangaza ni kuwa,
"Je, kunakuwa na ni nani hasa anatakiwa kuthibitisha maelezo yanayotolewa na Polisi?"
"Hivi inakuwaje ni Majambazi tu ndio wanauwawa na sio Polisi katika matukio ya kurushiana risasi?"
Nawasilisha.
Hadithi kutoka kwa majambazi wastaafu zinadai kwamba kuna masharti yaliyobarikiwa na polisi kwa majambazi. Iba lakini usiue. Toa taarifa unaenda kuiba wapi. Hakikisha kundi la kijambazi liwe na msimamo mmoja bila kuzikana mafao, tena polisi wapelekewe chao haraka.
Wanaendelea kusisitiza kwamba ndio maana hata kipiga sim kuita msaada wa mapolisi watajivutavuta kupitisha muda na baadaye wanakuja kwenye eneo la tukio wakiuliza maswali ya kiajabuajabu kutimiza wajibu tu, wakati huo tayari wanakuwa wameambiwa na majambazi wamevuna nin na watarajie nini mafao yao. Utaambiwa ukaandikishe polisi. Maelezo yako ya kipolisi yanawasaidia polisi to verify kama kweli mafao waliyoambiwa watapata ni "haki" au la.
Ikitokea hawana habari na tukio la ujambazi linalotarajiwa sehemu husika wanapenda kuwahi haraka wajue nani kaingia kwenye anga zao bila kibali. Wakiwatambua au majambazi yakijieleza kutoa taarifa kituo kingine basi mapolisi wanathibitisha hilo halafu mchezo unaisha. Ndio maana utasikia majambazi yamekamatwa na kesho unayakuta mtaani huru.
Wakati mwingine wanafanyiziana tu, kama siku za nyuma hawakutimiziana chao basi wanategesheana. Safari hii wwanbishana wee, kisipoeleweka wanatumana, ndio unasikia majambazi yameuawa. Majambazi nayo yakishituka yanawatuma wenzao ambao ndio wanaenda kuuliwa na yenyewe yanabaki huru.
ANgalia ukitoa taarifa za kiuhalu polisi inategemea taarifa hiyo imemkuta nani, wakati mwingine unatoa taarifa, wanakuuliza wewe uko wapi, wanpata maelezo yako na kuwajulisha majambazi ambao wnakushughulikia ipasavyo. Wapo polisi serious, sio woteni wahalifu. Lakini kumjua polisi serious sio kazi ndogo, saa nyingine wanajuana utakuta wananyoosheana vidole, wachapa kazi wazuri wanafanyiwa kila hila ili wakosee na watimuiwe au wauliwe.
Polisi wakati mwingine sio watu hawa. Hata wenyewe wanajua ukweli huo. Waliwahi kunifanyia hila hizo mimi mwenyewe nimewaogopa kiasi kwamba siamini polisi mpaka nimfahamu vizuri. Alikuja polisi mmoja kwenye kijiwe changu akitaka kupiga simu bure tena sio ya kikazi. Alipokataliwa akaahidi kabisa kwamba tutamtambua yeye ni nani sio muda mrefu. Kweli hatukukaa sana pakabomolewa na kuibiwa. Taarifa ilipopelekwa kituoni wala hawakuja kwenye eneo la tukio mpaka siku mbili baadaye walipofika na kusemasema kimzaha. Ati, 'Ah hawa wezi bwana, waliiba nini na nini? msijali, mkimhisi mtu tuambieni" ikaa ndio mwisho.
Majambazi hawawezi kufanya vitu vitu vyao kibudu. Wanajulikana na wanajuana, hata aina ya silaha wanazotumia zinajulikana. Ukisikia jambazi kauawa ujue kavunja mwiko wa mitandao inayowahusisha mapolisi. Mchapa kazi mwaminifu hadumu kwenye mapambano ya kipolisi na majambazi.
Leka
duh, Leka umenifumbua macho na hii hadithi ya majambazi wastaafu. Nimeishiwa nguvu kabisa. Kumbe basi hata hawa polisi baadhi yao ni majambazi!
POLISI KAGERA WAUA MAJAMBAZI WAWILI NA KUPATA SMG 2 NA MABOMU YA MKONO NGARA KAGERA DESEMBA 22, 2009.
Polisi mkoani Kagera wameyaua majambazi mawili kwa kuyapiga risari katika mapambano makali na kufanikiwa kupata silaha mbili aina ya SMG, risasi 62 na mabomu matatu ya kutupa kwa mkono.
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera ACP Henry Salewi, amesema kuwa tukio hilo limetokea leo 22/12/09 alfajiri huko kwenye Pori la Mjerumani karibu na kijiji cha Bugalama wilayani Ngara wakati Polisi walipokuwa kwenye doria ya kudhibiti ujambazi wa kuteka magari kwenye pori hilo.
Kamanda Salewi amesema Askari hao wakiongozwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Ngara mkoani humo, SP Mohammed Milanzi na Mkuu wa Upelelezi wa mkoa huo SP Peter Matagi, waliwaona watu wanne kati yao watatu wakiwa na silaha aina ya SMG na mmoja akiwa na begi lililokua na mabomu matatu ya kutupwa kwa mkono pamoja na magazine iliyokuwa na risasi 30.
Hata hivyo Kamanda Salewi, amesema kuwa wakati wa mashambulizi hayo, majambazi wawili walifanikiwa kutoroka wakiwa na silaha moja aina ya SMG.
Kamanda Salewi amesema kuwa Polisi inaendelea kuwasiliana na wananchi mbalimbali ili kwenda katika Hospitali ya Wilaya ya Ngara kwa ajili ya kufanya utambuzi wa majambazi hayo.
Amesema Makachero wa Polisi mkoani humo wanaendelea kufuatilia taarifa ya kuyapata majambazi yaliyotoroka na kwamba amewataka wananchi kutoa taarifa Polisi kama watawaona watu wawili wakiwa na majeraha wakitafuta tiba ili wakamatwe.
Hivi karibuni Polisi mkoani humo waliyaua kwa risasi majambazi nane katika matukio mawili tofauti yaliyotokea wilayani Biharamulo na kufanikiwa kupata silaha saba aina ya SMG na risasi 607 na mabomu mawili ya kutupwa kwa mkono.
Mwisho
source:www.policeforce.go.tz
Ukiwa polisi kwenye doria ukapata habari kuna ujambazi unatendeka, na ukifika kwenye tukio unakutana na watu wenye bunduki wanapambana na wewe, unahitaji uhakika gani tena kuwa hawa ni majambazi? Au benki inavamiwa majambazi wanaonekana kabisa wakirusha risasi hovyo kusambaratisha watu, unataka polisi watafute uhakika gani kwenye hali kama hii? Jambazi yuko mbele yako na SMG mtutu unatema kama mvua unataka polisi akamkamate, atamkamataje? Unacheza wewe! Jambazi auawe tu, hakuna kubembelezana. Watu wenye mawazo kama haya ya kwako mi nawaona mdebwedo tu.
Majambazi mengi huwa yanauliwa kwenye mapambano kwa sababu ya kuzidiwa nguvu ya ziada ya polisi, wananchi na hali ya mfadhaiko kuwa huenda mwisho mwao umefika, na katika kufadhaika huko hushindwa kufikiri upesi na kufanya maamuzi ya kukimbia hovyo ili kuokoa maisha yao. Na hapo ndipo huwa target nzuri ya Polisi. Lakini wengi wa majambazi wana elimu hiyo hiyo labda kama ya polisi na wakati mwingine huwa ni askari wastaafu.polisi wanapewa mafunzo na wanajua namna ya kutumia silaha lkn majambazi waliowengi kwanza hawana elimu na hata utumiaji wa silaha ni kubahatisha kwahiyo ndio maana mara nyingi majambazi wanauliwa!
This question is not easy as other people think.
No one is safe! I repeat kama hamjui polisi wanatakiwa kufanya nini msishabikie haya mambo. better know what polisi are supposed to be
unaweza kuzushiwa mwizi any time, unaweza ukapaki gari mtu akatilia mashaka na kuita polisi. hivi mnawajua polisi wanavyofanya kazi
I hate majambazi, lakini kuna sababu ya polisi kuji-equip their solution iswe kuua tu. some of them are innocent!
majamabazi wanaweza kumteka tax driver wakavamia sehemu polisi wanavyokuja tax driver naye anauawa!
wanachojitetea wao ni kuwa zana hafifu za kazi!
naona kuna majibu mapesi hapa kwa swali gumu