Polisi Tanzania wamekithiri kwa uongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi Tanzania wamekithiri kwa uongo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Synthesizer, Sep 7, 2012.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Wengi wetu tunajua kuna baadhi ya watu wanafungwa kwa makosa ya kubambikiwa kesi na kupandikiziwa vidhibiti vya uongo na polisi, kama bangi, madawa nk. Hilo linajulikana, sula la kesi za kubambikiwa Tanzania liko wazi.

  Nakumbuka wafanya biashara wa madini waliouwawa polisi wakasema walikuwa majambazi, kumbe ni uongo.

  Morogoro walisema muuza magazeti alirushiwa na waandamaji kitu cha ncha kali kikaamua. Iringa Commissioner mzima wa polisi alidanganya umma na kusema Mwangosi aliwakimbilia na mtu fulani akawarushia bomu likamuua.

  Matukio ya polisi kusema uongo yanaongezeka siku hadi siku.

  Najiuliza sana, tuna polisi wa aina gani ambao hawaoni aibu kusema uongo? Uongo wa polisi umeathiri watu wangapi ambao ilibidi wapelekwe gerezani?

  Polisi hawana kiapo cha kusema ukweli? Jamii ya Watanzania itawezaje kuamini chochote kinachosemwa na polisi ikiwa wanaonyesha kusema uongo ni tabia iliyojijenga miongoni mwao? Kwa nini polisi wanaosema uongo wanaendelea kulitumikia jeshi hilo hata inapokuja julikana walidangnanya? Polisi kusema ukweli chapaswa jkuwa sifa namba moja ya kuwa askari polisi.

  Polisi waongo ni jambo zito sana katika suala la haki za raia.
   
 2. Big One

  Big One JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 759
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  si hatuna polis tuna migambo tu
   
 3. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280

  Katika namna nyingi, zaidi ya mauaji ya raia, polisi wanakuwa wahalifu wenyewe. Polisi wa hivyo ni hatari sana. NImeona kwa wenzetu nchi za magaharibi si lahisi kupinga ushahidi wa polisi, maana kila mmoja anajua wanaaminika kusema ukweli, lakini hapa kwetu, polisi akikamata mtu unajiuliza hivi kweli huyu jamaa alifanya kosa au ameuziwa kosa na polisi!
   
 4. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ningeshauri jeshi lichukue nchi..polisi kazi zimewashinda
   
Loading...