Polisi na kilo 30 za mihadarat(Bangi)i. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi na kilo 30 za mihadarat(Bangi)i.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Mar 24, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Polisi wawili mkoani Mwanza wanashikiliwa mahabusu baada ya kutwangana makonde na kuumizana wakigombea kilo 30 za mihadarati.

  Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema lilitokea juzi saa 7.30 mchana kwenye kituo cha mabasi cha Buzuluga ambapo askari G.2748 Konstebo Daniel wa kituo cha Nyakato na G.3704 Konstebo Willy wa kituo kikuu cha polisi mjini Mwanza walipigana na kujeruhiana vichwani wakigombea begi lililokuwa na mirungi.

  Chanzo cha habari cha gazeti Uhuru kinasema begi hilo lilitupwa na abiria aliyekuwa kwenye basi la kampuni ya Zuberi, lililokuwa likitoka Musoma. Alitupa begi hilo baada ya kushitukia kuwa atakamatwa na polisi.

  "Abiria huyo mwanamke aliposhuka kwenye basi akiwa na begi jeusi lenye mirungi, alitaka kukamatwa na Daniel, hivyo akalitupa na kutoweka," alisema shuhuda wa tukio hilo, ambaye ni mpiga debe kituoni hapo.

  Alisema baada ya mwanamke huyo kutupa begi, Daniel alilichukua na baadae Willy alikwenda kumnyang'anya akimtaka wagawane. Kwa mujibu wa mpiga debe huyo, askari hao ambao hawakuvaa sare walianza kupigana hadi kuumizana, kabla ya kutiwa mbaroni na polisi waliokuwa doria.

  Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Nonosius Komba alikiri kukamatwa kwa askari hao, ambao alisema watashitakiwa kijeshi.

  "Niko Uwanja wa Ndege nasubiri kumpokea Makamu wa Rais. Askari hao wako mahabusu na tutawashitaki kijeshi," alisema.
  [​IMG]

   
 2. aye

  aye JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,988
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 160
  duh iyo sasa imekaa vibaya ni njaa izo lakini
   
Loading...