Polisi mnaokamata gongo hamfanyi haki

Polisi mnaokamata gongo hamfanyi haki

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
23,717
Reaction score
57,245
Enzi za Magufuli alisema muache kukamata wanaouza gongo kwani hata mama zenu waliwasomesha kwa hio biashara.leo hii mnataka hela mnaanza Tena kusumbua watu Kama kweli nyie mnapenda afya za watu Basi kamateni na wauza sigara,madawa ya kulevya,pombe kali n.k

Msitake kusema kwamba gongo ndo yenye sumu peke yake.kg nitembezee pegi.
 
Wakamate tu.....kuna viburudisho raha yake uvitumie huku machale yanacheza.(mjomba gongo na bamkubwa majani)vikihalalishwa uhondo unapotea
 
Kutokana na kutamalaki kwa pombe feki mitaani nadhani idadi kubwa ya wanywaji wa pombe wanananyweshwa gongo bila kupenda. Hakuna pa kutokea iwe Konyagi, K- vant , Johnny walker niyaleyake gongo tupu
 
Kutokana na kutamalaki kwa pombe feki mitaani nadhani idadi kubwa ya wanywaji wa pombe wanananyweshwa gongo bila kupenda. Hakuna pa kutokea iwe Konyagi, K- vant , Johnny walker niyaleyake gongo tupu
Acha tu mkuu..ndio Mana wakati mwingine naonaga Bora kunywa Gongo gredi One
 
Mkuu wamekuja kukufanyia fujo ukiwa unakunywa supu ya maninja nini?
 
Serikali nashindwa kuielewa pale wanavyotuambiaga tupende vitu vyetu vya asili kama
1.ngoma za asili
2.vyakula vya asili ie kuku wa kienyeji,matunda na mboga
Sasa linapokuja swala la pombe za asili sioni kiongozi yoyote akisifia kama vile chang'aa,wanzuki,pombe ya mnazi,mataputapu ukijumlisha na gongo ndo kabisa unaitafuta jela
 
Back
Top Bottom