MWANZA: Watu wanne wamekatwa na pombe haramu ya Gongo

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
MWANZA.jpg


Jeshi la polisi mkoa wa mwanza.
Watu nane wanashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kukamatwa na pombe aina ya gongo katika msako uliofanyika maeneo ya luchelele wilayani nyamagana.

Kwamba mnamo tarehe 16.06.2016 majira ya saa majira ya saa 14:00hrs katika eneo la luchelele wilaya ya nyamagana mkoa wa mwanza, askari polisi walifika katika eneo hilo tajwa na kufanya misako pamoja doria nakuweza kufanikiwa kukamata watu nane wakiwa na pombe aina ya gongo pamoja namitambo ya kutengenezea pombe hiyo kitendo ambacho ni uvunjwaji wa sheria na taratibu za nchi.

Watuhumiwa waliokamatwa, 1. Jescar Simoni miaka [14], mwanafunzi, ambaye alikamatwa akiwa na lita 42 za pombe aina ya gongo, 2.NYANGE Bihemo miaka [46] aliyekamatwa akiwa na mitambo miwili ya kutengenezea pombe ya gongo, 3. Mariam Omary miaka [28] aliyekamatwa na pombe ya gongo lita 3, 4.

Maola Luchupa miaka 32 aliyekamatwa akiwa na lita 20 za pombe aina ya gongo. Wengine ni, 5. Elizabeth john miaka 35 aliyekamatwa na mitambo mitatu ya kutengenezea pombe ya gongo, 6. Anastazia aloyce miaka 25 aliyekamatwa na pombe ya gongo lita 2, 7. Tedy Pius miaka 40 aliyekamatwa na lita 30 za pombe ya gongo na, 8. Paskazia Thomas aliyekamatwa na mitambo miwili ya kutengenezea pombe ya gongo, watuhumiwa wote ni wakazi wa luchelele.

Aidha inadaiwa kuwa watuhumiwa hufanya biashara haramu ya pombe ya gongo na wakazi wa maeneo hayo, huku wakiihalalisha biashara hiyo kuwa kama chanzo chao kikuu cha kipato cha kila siku kitendo ambacho ni uvunjwaji wa sheria na taratibu za nchi. Ndipo jeshi la polisi lilipokea taarifa za kiintelejensia kuhusiana na uhalifu huo unatendwa na baadhi ya wakazi wa luchelele na kufanikiwa kukamata watuhumiwa tajwa hapo juu.

Watuhumiwa wote wapo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi huku mahojiano dhidi ya uhalifu wanaoufanya wa kujihusisha na biashara haramu ya pombe aina ya gongo ukiendelea, pindi uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayo wakabili.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi ahmed msangi anatoa wito kwa wananchi wa jiji na mkoa wa mwanza akiwataka wafanye kazi nyingine halali ambazo zitawaingizia kipato, lakini biashara haramu za pombe ya gongo na madawa ya kulevya nawaomba muache kujihusisha nazo kabisa, kwani jeshi la polisi mkoa wa mwanza limejipanga vizuri kukabiliana na wahalifu wa aina kama hiyo na kuhakikisha wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Imetolewa na:
SACP: ahmed msangi
Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza.
 
Back
Top Bottom