Polisi mkoani Kigoma wanamshikilia mwalimu wa Shule ya Msingi Mwanga kwa tuhuma za ubakaji na ulawiti wa mtoto wa miaka kumi

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Polisi Mkoani Kigoma wanamshikilia mwalimu wa shule ya msingi Mwanga iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji Zakaria Richard mwenye umri wa miaka 30 kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti Mwanafunzi mwenye miaka 10 anayesoma darasa la tano katika shule hiyo.

Mwanafunzi huyo [Ambaye jina lake limehifadhiwa] alikabidhiwa na wazazi wake kwa mwalimu huyo, kwa lengo la kumfundisha masomo ya ziada [tution] na badala yake mwalimu huyo alianza kumfanyia vitendo vya kikatili.

Hata hivyo uchunguzi bado unaendelea na pindi utakapo kamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa ajili ya taratibu za kisheria.

Pia, Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma amewaasa wazazi kua makini pale wanapowakabidhi watotot wao kwa walimu kwa ajili ya kufundishwa masomo ya ziada. Amesema wahakikishe wanafalitia kwa karibu maendeleo ya watoto wao
 
Hao wabakaji na wanaolawiti serikali isiwe inawafunga mana serikali inaingia gharama kutunza watu wapuuzi.
Hao dawa yao ni kuhasiwa tu kishaa waachwe kama wataendelea lawiti au wao ndo watalawitiwa.

Mtu umebaka vipimo vikaonesha pasipo shaka kuwa wewe ndiye mhusika basi unahasiwa tu...
Hii ingekomesha ubakaji
 
Inasikitisha sana matukio kama haya kuendelea kutokea katika jamii zetu,adhabu kali zitolewe ili iwe fundisho.
 
Hebu nielewesheni wakisema kulawiti si ni inamaanisha aliyeingiliwa ni mwanaume? Angekua mwanamke wangeandika kuingiliwa kinyume na maumbile?

Naona wadau wanaconclude ni binti.
 
Yaani mtaani kulivyo sasa ni kujichagulia tu.
Unaamua leo nile mbuzi au kondoo, kitimoto au ng'ombe, kuku au bata!

Eti mwalimu unaenda kula kifaranga!?
 
Yani apatiwe adhabu kali kabisa, umri huo kwenda kumlawiti mtt mdg km huyo

Ana utamu gani ,au ana ushawishi gn mtt wa miaka10 kwa mbaba kama huyo.

Pia wanawake wote waliojaa kweli ,ameshindwa kutongoza ili aweze kidhi mahitaji yake...

Ama kweli izi kesi za ubakaji zimezd sn siku hz, serikali ibadilishe adhabu kwa watu km hawa, nadhn wataacha km adhb itakua kali zaidi.
 
Hivi kweli mtaani kulivyo na wanawake wa kila aina huyu aliona nini kwa mtoto wa miaka kumi?
Adhabu kali itolewe kwa huyo mbakaji ili iwe fundisho kwa wenye tabia kama zake
Itakua amefata nyayo za kiongozi wao mkuu kiimani
 
Hebu nielewesheni wakisema kulawiti si ni inamaanisha aliyeingiliwa ni mwanaume? Angekua mwanamke wangeandika kuingiliwa kinyume na maumbile?

Naona wadau wanaconclude ni binti.
Ushasikia amem'baka na kumlawiti Kuna matendo mawili Hapo
 
Wakati mwngne si imani za kidhirikina wala nini...

Basi tu tamaa ya mwili ndiyo huwa inawaponza


Basi ni uwendawazimu tu, hivi kwa wanawake waliojaa mitaani humu kwenda kumfanya vibaya mtoto wa watu hivo hasa kilichomtamanisha ni nini??
 
Duh, watu wana roho ngumu jamani, mtoto Mdogo kama huyo ana ladha gani sasa, aargh ,sheria Kali ichukuliwe dhidi yake
 
Back
Top Bottom