Polisi mkoani Kigoma wakabiliana na Majambazi, waua mmoja

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
mtui.jpg



Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limekabiliana kwa risasi na kundi la majambazi katika msitu wa Maghorofani katika barabara ya Kigoma-Mpanda ,na kufanikiwa kumuua mtu mmoja na kukamata bunduki moja ya kivita aina ya SMG na risasi 74 zilizokuwa zitumike kufanya utekaji wa magari katika barabara hiyo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa polisi Ferdinand Mtui amesema awali polisi walimkamata mtuhumiwa Hamis Kabeteye mkazi wa kijiji cha Kitahana wilayani Kibondo, na kufanikiwa kupata risasi 51 katika kijiji cha Kalenge wilayani Uvinza,ambapo baada ya mahojiano aliwapeleka eneo la tukio ambako walikabiliana na wenzake waliokuwa wanajiandaa kuteka magari ambapo walifanikiwa kukimbia huku mtuhumiwa mmoja akiuawa,na polisi kufanikiwa kupata risasi zaidi .

Katika hatua nyingine polisi wamekamata zaidi ya pikipiki mia nne na bajaji thelathini kutokana na makosa ya usalama barabarani ikiwa ni pamoja na madereva wake kutokuwa na leseni na kutozingatia sheria za usalama barabarani.

Chanzo: ITV
 
yaani hawa jamaa kwa sasa kama una kisasi nao utashangaa ,hata bunduki hujawahi igusa lakini wakijakupekuwa kwako itakutwa uvunguni tena na maelezo yao itakuwa ulikuwa unarushiana nao,wameambiwa wapokonye silaha kwa haraka wanatimiza kazi yao
 
Back
Top Bottom