Polisi mfuatilieni Mtu huyu

Abdull Kazi

JF-Expert Member
Dec 29, 2012
323
255
Hivi Karibuni katika maeneo ya Chanika kuna mtu ameibuka akijitambulisha kuwa ni Askari, anatumia gari binafsi yenye namba T673 DRL na mara zote hutembea na Redio mfano wa Redio call akiwa amevaa nguo za kiraia.

Kazi aliyojipa mtu huyu ambaye wajihi wake ni mweusi na mfupi wastani wa futi Tano ni kukamata magari ya daladala Majira ya jioni kwa Yale yanayofanya makosa Kisha hutoa plate number na kuwaagiza wahusika wamfuate.

Jana Mei 28 alikamata magari mawili yanayofanya safari kati ya Chanika na Segerea kwa tuhuma za kukatisha ruti na nyingine kuovateki sehemu isiyo sahihi.

Baada ya kukamata moja alitoa plate number na nyingine akamuambia dereva amfuate.

Wote walielekea eneo la baa ya Sonate Chanika na kupaki hapo Kisha wahusika wakatoa fedha na kuachiwa.

Nimeongea na baadhi ya madereva wakaeleza mtu huyo huanza majukumu yake hayo kuanzia saa 11:30 jioni.
 
Hii habari ina ukakasi.

Hana uniform, jina hamumjui means haonyeshi kitambulisho sasa watu wanakubali vipi kufanyiwa hayo?

Ni kama hao wananchi/madereva hawajielewi
 
Bima hii imekwisha siku 636 zilizopita. KATA BIMA MPYA, TII SHERIA BILA SHURTI!

Motor Vehicle Insurance Cover Validation | Uhakiki wa Bima ya Chombo cha Moto

Vehicle Registration Number | Namba ya Chombo cha Moto

gari haina bima miaka miwili iliyopita!!!
 

Hii nchi watu wazembe sana acha watapeliwe tu
 
Unasimamishwa na mtu wa aina hiyo, kabla hajamaliza mazungumzo yake unaondoka.

Kama kuna shida awaambie polisi waje kukukamata.
 
Nimeongea na baadhi ya madereva wakaeleza mtu huyo huanza majukumu yake hayo kuanzia saa 11:30 jioni.
OVERTIME!
 
Tatizo la wabongo ni waoga sana kuhoji. Kitendo cha huyo mtu kutokuwa na uniform tayari kunatia shaka kiasi cha kuhalalisha maswali.
Ila ndio maana anafuata magari ya abiria maana anajua mengi yao huwa hayapo kamili kivibali.
 
Tatizo la wabongo ni waoga sana kuhoji. Kitendo cha huyo mtu kutokuwa na uniform tayari kunatia shaka kiasi cha kuhalalisha maswali.
Ila ndio maana anafuata magari ya abiria maana anajua mengi yao huwa hayapo kamili kivibali.
Magari ya abiria ndio yanakuwa na vibali vilivyokamilika zaidi kuliko ya private, hupendelea kukamata magari ya abiria sababu ndio yanatembea na pesa muda wote, na pia kuliko kupoteza root moja kwa siku kwa kupotezewa muda na askari ni bora kumpa hela uendelee na mishe.

Hata askari hutumia njia ya kupoteza muda ili utoe rushwa anajua kbs daladala haiwezi kuvumilia na abiria wakishuka ndo hasara kbs!
 
Daladala wanawajua askari wote hadi ukiona wanakubali kunyofolewa plate number jua hio ni askari na sio tapeli. Huyo ni askari anayo haki ya kula mbuzi zilizokata kamba. Kama wanavunja sheria kwa mujibu wa ruti zao kwenda bar kubargain ni sahihi. Wewe shika jembe.
Huyo askari hana kosa na hizo daladala hazina kosa, wanasaidiana maisha, we kashike jembe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…