Nyanimweupe
Member
- Feb 25, 2013
- 26
- 1
Habari iliyopo hapa wilayani MAKETE ni Juu ya askari polisi kumuua mwalimu wa shule ya msingi,
Taarifa zinasema kuwa mwaalimu huyo aliuliwa jana usiku mida ya 2:30 na askali walio kuwa zamu kwenye bank ya NMB aidha Jeshi la polisi halijatoa ufafanuz wowote ule bali ndugu wa marehem wameambiwa kuwa askari walidhani mwaalimu huyo alikuwa jambazi hvyo walitaka kumfyatulia risasi ya mguu bahati mbaya wakampiga kifuani.
Taarifa zinasema kuwa mwaalimu huyo aliuliwa jana usiku mida ya 2:30 na askali walio kuwa zamu kwenye bank ya NMB aidha Jeshi la polisi halijatoa ufafanuz wowote ule bali ndugu wa marehem wameambiwa kuwa askari walidhani mwaalimu huyo alikuwa jambazi hvyo walitaka kumfyatulia risasi ya mguu bahati mbaya wakampiga kifuani.
WAKATI mtuhumiwa wa mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa kituo cha runinga cha Channel Ten mkoani Iringa Daudi Mwangosi, askari wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) akitarajiwa kufikishwa tena mahakamani leo kwa kesi hiyo kutajwa, askari wilaya ya Makete mkoa wa Njombe wanadaiwa kufanya mauwaji ya kinyama kwa kumpiga mteja wa benki ya NMB kwa risasi.
Huku askari mmoja anayetuhumiwa kufanya unyama huo aliyetambulika kwa jina moja la Jose akishikiliwa na jeshi la polisi kufuatia mauwaji hayo ya kinyama.
Tukio hilo limekuja huku bado watanzania hasa wakazi wa mikoa ya Iringa na Njombe wakiwa bado hawajasahau mauwaji ya kinyama yaliyomkuta mwanahabari Daudi Mwangosi ambapo kesi hiyo bado ikiendelea kutajwa na wanahabari waliokuwepo eneo la tukio siku ya mauwaji wakisubiri kuchukuliwa maelezo yao kama mashahidi wa kesi hiyo pindi itakapoanzwa kusikilizwa.
Mwandishi wa wetu kutoka Makete Njombe anaeleza kuwa tukio hilo wamedai kuwa mauwaji hayo ya kinyama yametokea jana jumatano majira ya saa 1.20 usiku baada ya mteja huyo aliyekuwa na usafiri wa boda boda kufika eneo hilo la benki kwa lengo la kuchukua fedha .
Imedaiwa kuwa aliyepigwa risasi anatambuliwa kwa jina la Casto Kawambwa mkazi Mbalizi mkoani Mbeya na kuwa baada ya kupigwa risasi alikimbizwa katika Hospitali ya wilaya ya Makete ambako inadaiwa kabla ya kupatiwa matibabu amefariki dunia .
Kutokana na tukio hilo jeshi la polisi liliwazuia wanahabari kutimiza wajibu wao kwa kupiga picha wala kusogea eneo hilo la Hospitali na badala yake kuweka ulinzi mkali eneo hilo la Hospitali ili kuzuia wanahabari kusogea eneo hilo .
Hata hivyo mmoja kati ya askari ambaye jina lake halikufahamika mara moja alisikika akidai kuwa chanzo cha mteja huyo wa benki kupigwa risasi alikuwa akihisiwa kuwa ni jambazi na hivyo baada ya kufika eneo hilo kwa usafiri wake wa piki piki (boda boda ) walihisi kuwa amefika kwa ajili ya kufanya vitendo vya uporaji katika benki hiyo na hivyo askari katika hali ya kujihamia aliamua kumpiga risasi.
Jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi wa mkoa wa Njombe ili kuzungumzia undani wa tukio hilo linafanyika na mtandao huu .
CHANZO: Blog ya Francis Godwin