Muda mfupi ujao watanzania tutaingia kwenye simanzi kufuatia amri iliyo tolewa kwa jeshi la polisi kutumia nguvu kwa kadri itakavyo wezekana kuwatoa wamachinga walio jigawia maeneo ya biashara katika eneo ambalo lipo Kilombero linalo daiwa kuuzwa kwa mtu binafsi.
Katika juhudi za kutafuta taarifa nimefanikiwa kuongea na jamaa mmoja kutoka jikoni akanihakikishia kuwa muda wowote FFU kutoka Babati, Karatu na Moshi watawasili kutekeleza amri.
Aidha inasemekana Mkuu wa mkoa amejiandaa vyema na mkuu wa polisi kwa kuiua Chadema kwakile wanacho dhani kuwa Chama hicho ndicho kinachowapa jeuri wa machinga.
Ikumbukwe mzozo huu unatokana na sakata linaloendelea Arusha kwa machinga kutaka maeneo ya biashara.
MUNGU IBARIKI TANZANIA