Muda mchache uliopita nilikuwa natoka KIA naelekea A Town, nikampa lift askari mmoja wa usalama barabarani ndipo nikaipata hii habari, kuwa jeshi la polisi nalo limepewa lengo la kukusanya mapato kiasi cha 1.7b kwa mwaka na kwamba makosa yameongezwa kutoka 15 hadi 30 hivyo kila askari wa usalama anatakiwa kukamata kosa moja kwa siku ili hilo kosa litozwe faini, hivyo kwa mwezi kila mmoja awe amekamata makosa 30 ili kufikia lengo, zaidi ya hapo unaweza ondolewa kwenye hicho kitengo. Na inasemekana baada ya TRA wanaofuata ni Polisi kwa ukusanyaji wa mapato. Swali ninalojiuliza hawa polisi wanabiashara gani hadi wapangiwe lengo? Na je kazi yao ni kujitahidi kupunguza makosa au ni kuyaongeza uli kupata fedha kufikia malengo? Na kuwa POlisi siku hizi ni sehemu ya mapato ya serikali? Tujadili.