Polisi kukwepa mauaji ya Suguta!

Polisi kukwepa mauaji ya Suguta!

Jeshi la polisi lipo kimkakati kukwepa kuwa wao ndiyo wauaji wakuu wa Suguta aliyechomwa kisu na askari wa doria.
Wanadai askari alikuwa na ugomvi binafsi na marehemu suguta wakasahau kuwa huyo afande Marwa hakuwa pekee yake bali walikuwa askari wengine ambao kwa umoja wao wangezuia maafa hayo na kumkamata bwana Suguta na mmiliki wa bar na kuwafungulia kesi hadi kuwatia hatiani(ikiwa wangekutwa na kosa).
Nguvu hii kubwa kama itaachwa basi hakika walevi tutakoma maana itakuwa mkiwaona askari tu mnajua mwendo wa visu tu.
Jeshi la polisi kaeni chini mjitafakari mahusiano yenu na raia yakoje kwani kwa sasa hakuna anayeliamini jeshi hili imani pekee imebaki kwa JWTZ tu.
Angalieni komenti za watu inapotokea askari kafa au ajali mtajifunza mengi.
Hakuna kukwepa wala kuhusisha ugomvi binafsi na hili askari na jeshi la polisi ndiyo wauaji wakuu wa Innocent,Suguta.
Haitakuwa ya kwanza , Kuna Mwangosi na Akwilina , polisi wanatuona mafaaaaalaa !
 
Tii sharia bila shuruti, vinginevyo hata yatawapata sana tu
 
Masihara kwenye sensitive issues kama mauaji yanakusaidia nn...Tungekuwa bado tupo kwenye mfumo wa chama kimoja bado ungekuwa una comment kifedheha kwenye mambo ya mauaji ya raia ?...Ungekuwa unakipenda ccm kiukweli , ungekuwa wa kwanza kukemea kijitenge na mauaji ya raia inayopaswa kuwalinda- Kwa kuchukua hatua, siyo kuwasafisha wauaji!.
Nadhani kichwani una tatizo. Umeambiwa kuwa kulikuwa na ugomvi, pia hakuna ushahidi wa marehemu kuwa na kadi ya siasa, wewe limbukeni
 
Mwishoni utaambiwa... "marehemu alikwaruzwa na kitu chenye ncha kali hadi akafa".... Subiri ushangae
 
Back
Top Bottom