Polisi kuichunguza mitandao ya mawasiliano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi kuichunguza mitandao ya mawasiliano

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 23, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  POLISI kupitia Kamisheni ya Upelelezi wa Makosa ya Jina imeanzisha doria katika mitandao ya mawasiliano ili kukabiliana na ongezeko la uhalifu wa kwenye mitandao.

  Mkuu wa Kitengo cha Maabara ya Uchunguzi wa Uhalifu, Makao Makuu ya Upelelezi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Jamal Rwambow, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo ya doria katika mtandao (Online Patrol).

  “Ni imani yangu mafunzo mtakayopata yatakuwa taswira halisi ya maboresho ya ya Jeshi la Polisi na yatawawezesha kupata mbinu za kubaini uhalifu na wahalifu kabla ya tukio,” alisema.

  Alisema, baada ya mafunzo hayo, uhalifu ukitokea watakuwa na uwezo wa kupeleleza kesi kwa umahiri, ustadi na kwa njia sahihi za kisayansi kwa kukusanya ushahidi wa kutosha utakaomuunganisha mshitakiwa na kosa analokaabiliwa nalo.

  Kwa mujibu wa Rwambow, uhalifu wa sasa umebadilika kutokana na maendeleo ya kiuchumi, sayansi na teknolojia, harakati za kibiashara, mwingiliano wa watu kutoka mataifa mbalimbali, kuongezeka kwa watu, makazi na malezi katika jamii mbalimbali na sera za utandawazi duniani.

  Awali Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo wa Polisi, Abrahaman Kaniki alisema, wanaangalia uwezekano wa kufikisha mafunzo hayo kwa askari wote nchini lengo likiwa kuimarisha doria katika mtandao ili kupambana na uhalifu.

  Mafunzo hayo ya wiki mbili yanahudhuriwa na washiriki 12 kutoka mikoa ya Zanzibar, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Tanga na Rukwa.
   
 2. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Haiwezekani kuthibiti uhalifu unaotendeka katika mitandao ya komputa bila kuwa na sheria ambazo zitatumika kuwaadhibu wahalifu; kuna umuhimu wa kutunga sheia kwanza ama sivyo hizo kesi zitashindikana kuwahukumu watu mahakamani. Sina hakika kama Tanzania imetunga sheria kuhusiana na cybercrimes!!
   
Loading...