Fred Mwakitundu
JF-Expert Member
- Dec 31, 2018
- 227
- 383
Miaka mitano imepita tangu atoroke akiwa nje ya dhamana Kamran Ahmed raia wa Pakistan ambaye alikamatwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro(KIA)akisafrisha wanyama hai wenye thamani ya shilingi Milini 170.5 wakiwamo Twiga wanne kwenda Doha Qatqr Falme za kiarabu akitumia ndege ya jeshi .
Kamran alifikishwa mahakamani na wenzake wanne akishitakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi,wote walinyimwa dhamana na mahakama za chini mjini Moshi lakini walipewa dhamana na mahakama Kuu Kanda ya Moshi baada ya kupewa masharti sita magumu lakini waliyatimiza na kuwa nje kwa dhamana.
Washitakiwa wengine ni Martin Kimati,Hawa Mang'unyuka na Jane Mbogo ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kenya .
Raia huyo wa Pakistan alidhaminiwa na watu wawili wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro,Peter temba(marehemu) na Jackson Kimambo ambaye yupo hai mpaka sasa lakini mshitakiwa huyo aliruka dhamana na mmoja wa wadhamni wake(marehemu Peter Temba)akitiwa mbaroni na kwenda kutumikia kifungo chake .
Moja ya masharti ya dhamana ilikuwa ni wadhamini hao kuweka bondi ya maneno ya sh,Milini 14 kila mmoja,washitakiwa hawakuruhusiwa kutoka nje ya mkoa wa Kilimanjaro na Arusha bila kibali kutoka ofisi ya Naibu Msajili wa mahakama Kuu kanda ya Moshi.
Baada ya mshitakiwa huyo kuruka dhamana,Kimambo alikimbia kukwepa mkono wa dola na kwenda kujificha kusikojulikana kwa zaidi ya miaka miwili lakini hivi sasa amerejea uraiani na polisi hawajaweza kumkamata japo wanamuona kila siku na wanapiga naye story za hapa na pale.
Ikumbukwe kuwa jinai siku zote huwezi ukaikimbia na unaweza ukahukumiwa bila wewe kuwepo na mahakamani lakini baada ya miaka mitano unaweza ukakamatwa na kwenda kutumikia kifungo chak,maana yake ni kwamba Kimambo bado ni mtuhumiwa na akikamatwa atatumikia kifungo chake kama mwenzake.