Polisi ichunguze tukio Lissu kushambuliwa?

Polisi ichunguze tukio Lissu kushambuliwa?

Umkilo

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2018
Posts
470
Reaction score
421
Leo nimekaa nikajiuliza vimaswali flani hivi korofi kwenye tukio la shambulizi la Lissu.

Hivi ni kweli kuwa kukosekana kwa dereva wa lissu ndio sababu hadi leo polisi wameshindwa kupata mshukiwa hata mmoja hata kuhisi?

Kuna siku nilisikia magari yamekamatwa je ni magari pekee au magari na madereva? kama ni magari pekee hivi magari ndio yaliyopanga na kumshambulia lissu au ni wamiliki/madereva na abiria wa magari siku ya tukio?
Je magari hayo bado yapo polisi au yameachiwa baada ya dereva wa lissu kukosekana.

kingine tunataka uchunguzi ufanyike au watu flani tunaowahisi wachunguzwe? je polisi wakifanya uchunguzi wakamate watu flani tusiojulikana kuwa ndio waliomshambulia badala ya bashite na jpm tutakuwa tayari kupokea majibu? tutalizika?

vipi wakiwakamata wapendwa wetu baada ya uchunguzi kuwa ndio wahusika tutakubaliana mfano polisi waje na ripoti ya uchunguzi kuwa Lema, nasari, boniface, mbowe au Lowasa mhusika wa kupanga au kupanga na kutekeleza je tutakubali/ tuko tayari kuipokea ripoti ya namna hiyo bila kinyongo? Je wakisema ni jpm tuko tayari kupokea? je polisi wanauwezo wa kulitangaza hilo?
 
Tujiandae kuchezewa muvi ya yule Joshua wa Kova na Ulimboka. Safari hii sijui ataenda kutubu kwa nani...au labda kwa Kakobe au nabii Tito?
 
Back
Top Bottom