MGOGO27
JF-Expert Member
- Jan 5, 2016
- 459
- 218
Jamani wanajamvi wenzangu niliwaza sana kuhusu sekta zilizobinafsishwa kama afya, elimu na ulinzi(binafsi) na labda maana ya kubinafsisha zitakuwa zilifanya vizuri mimi sijui?
Nilienda usiku kituo cha kati cha polisi nikakuta wameweka geti! sasa nilikuwa na haraka sana na ilikuwa ni muhimu kwenye taarifa niliyokuwa napeleka hapo ila hawa jamaa walinisimamisha na kunihoji sana sasa kama umeenda kuripoti maswala ya uhalifu unaoendelea itakuwaje? watawahi au watachelewa?
Baadae tulipomalizana nikahoji kwa nini wanaweka mageti?nikaambiwa kwa sababu ya kuogopa kuvamiwa na wananchi /raia wa kawaida sasa swali langu ni hivi suluhisho la watu au raia wema kuvamia vituo vya polisi kuweka mageti au kujua kwamba kwa nini raia wanavamia vituo vya polisi na kushughulikia sababu hiyo?
Polisi hawana watu au wataalam wa saikolojia? kama hawana basi wazo langu ni kubinafsisha ili kuleta ufanisi wa kazi zao mbona walibinafsisha sekta muhimu kama afya na elimu? kama wataalamu wapo mbona hawafanyi kazi zao???????Aibu kubwa sana hii kwa taifa.