Polisi Hata hili hamlijui? Huu ni Udhalilishwaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi Hata hili hamlijui? Huu ni Udhalilishwaji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mgt software, Jan 25, 2012.

 1. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,717
  Likes Received: 1,627
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD] Wauza dawa za kulevya waja na stahili mpya kali na Mwandishi wetu[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD] WAUZAJI wakubwa wa dawa za kulevya nchini, wamekuja na mbinu mpya ya kuingiza biashara hiyo haramu nchini, Tanzania Daima Jumatano limebaini. Katika mbinu hiyo, wafanyabiashara hao hujifanya wasamaria wema kwa kuamua kugharimia matibabu ya wagonjwa walio na hali mbaya kiasi cha kupoteza matumaini na kuwasafirisha kwenda nchini India kwa matibabu, huku wakijua fika kwamba hawawezi kupona. Imeelezwa kuwa baada ya kufika India na mgonjwa kufariki akiwa hospitali, hujitolea kugharamia kurejesha mwili ukiwa umebebeshwa shehena ya dawa za kulevya tumboni. Hivi karibuni, gazeti hili lilifuatilia kwa kina nyendo za mwili wa kijana mmoja aliyefariki katika hospitali moja nchini India ikiwa ni siku mbili tu baada ya kuwasili katika hospitali hiyo. Vyanzo vyetu vya habari vilisema kuwa kijana huyo (jina limehifadhiwa) ambaye alikuwa maarufu kwa uuzaji wa simu za mikononi katika eneo la Posta, alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya figo kwa muda mrefu. Inaelezwa kuwa baada ya kutibiwa katika hospitali mbalimbali na kupoteza matumaini ya kuishi, alirejea nyumbani, huku ndugu zake wakiwa wamekata tamaa ya kumponyesha ndugu yao. “Madaktari walisema kabisa mgonjwa wetu asingepona. Lakini walikuja watu waliojifanya wasamaria wema na kuomba wamsafirishe kwenda India kwa matibabu,” alisema mmoja wa ndugu wa karibu wa kijana huyo. Kwa mujibu wa habari hizo, kijana huyo alisafirishwa hadi India Jumatatu iliyopita na kufariki siku ya Jumanne. “Kwanza alisafirishwa bila ndugu, lakini tulipata taarifa za kifo chake siku moja tu baada ya kuwasili katika hospitali hiyo. Mwili wake ulirejeshwa Ijumaa iliyopita na ulizikwa siku hiyohiyo katika makaburi ya Kinondoni,” kilisema chanzo chetu cha habari. Habari hizo zilisema kuwa mwili wa marehemu ulipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, ulikaa kwa muda mfupi na baadaye kusafirishwa kwa gari la wagonjwa kwenda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ukisindikizwa na pikipiki maalum ya polisi. Mwili huo ulipowasili katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ulihifadhiwa kwa takriban saa mbili na hakuna ndugu aliyeruhusiwa kuuona mwili wa marehemu. “Pale Muhimbili ndugu walizuiliwa kabisa kuuona mwili hadi baadaye waliitwa ndugu wachache pamoja na mama wa marehemu ambao waliruhusiwa kuiona sura na kuthibitisha kuwa ni mwili wa ndugu yao. Baada ya hapo ulifugwa tena kwenye sanduku maalumu walilokuja nalo na kwenda moja kwa moja makaburini,” alisema mtoa habari wetu. Kwa mujibu wa habari hizo, gharama za kununua eneo la mazishi na nyingine zote, zilifanywa na wasamaria wema hao na baadaye kumpatia mama wa marehemu ubani wa sh milioni mbili. Siri kwamba mwili wa marehemu huyo ulibebeshwa shehena ya dawa za kulevya, ilitolewa na mmoja wa wafanyakazi wa chumba cha kuhifadhia maiti ambaye alimjulisha mmoja wa ndugu wa marehemu kwamba tumbo la ndugu yao liliondolewa kila kitu ili kuhifadhi dawa hizo za kulevya. Kamanda wa polisi wa kupambana na dawa za kulevya nchini, Godfred Nzowa, akizungumza na gazeti hili, alisema hiyo ni staili mpya kutumiwa na wafanyabiashara hao, lakini kwao inaweza kuwa ni staili ya zamani. “Hii ni mbinu mpya na kali maana ndiyo kwanza naisikia. Moja ya changamoto tunayokutana nayo katika vita hii ni mbinu mpya zinazotumika kuingiza biashara hii haramu nchini. “Unapotoka na mgonjwa kwenda nje kwa matibabu, unakuwa na nyaraka zake zote, hivyo urejeshwaji wa mwili wake kama atafariki, unakuwa na urahisi hasa kama chanzo cha kifo chake kinajulikana, ndio maana mbinu hiyo ni rahisi kuliko ile ya kuja na mwili ambao haujulikani mgonjwa alifariki kwa sababu gani,” alisema Nzowa. Kamanda Nzowa aliwataka wananchi kutoa ushirikiano hasa kama kuna mtu alisafirishwa kwa matibabu nje katika mazingira ya aina hii na kurejeshwa. Alisema kikosi chake kinalifanyia uchunguzi tukio hilo na kusisitiza kuwa wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano kukabiliana na vita hii[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. m

  moshingi JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii wala siyo mpya sana, wakati Kova akiwa Mbeya, Polisi wetu walifanikiwa kukamata madawa ya kulevya yaliyokuwa ndani
  ya maiti aliyekuwa akisafirishwa kutokea Mbeya kuja DSM. Hili linawezekana tu endapo patakuwepo watu ambao wataacha unafiki na kuripoti tukio kwa haraka hata kwa Inspekta Jenerali mwenyewe namba yake ya simu ipo wazi wakati wote, ili wahusika wakamatwe na ndipo mtuletee story iliyokamilika ambayo itanoga kwenye magazeti yenu, kuliko kuandika story huku tayari madawa yapo sokoni yanaua kizazi chetu haina maana sana. Huu ni kama udaku tu.
   
Loading...