Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 11,269
- 23,093
Shida ni hio TEKNO uliyotumia mzee baba.
Tatizo niUngekuwa na akili ungegundua kuwa
1. Hiyo picha imepigwa mbali
2. Imekuwa cropped sana kuondoa some details.
Simu ambayo imepiga hii picha ni moja ya the best simu camera. Sony Ericsson tuulize tulioanza kutumia simu miaka ya 1998. Tunaweza kukueleza kila simu uzuri wake na ubaya wake.
Kwenye mafunzo ya udereva wanafundisha, askari yoyote anaruhusiwa kukusimamisha, kukuhoji, na kukukamata ikibidi.
Hao ni askari wa doria, na wamepangiwa sehemu hiyo na kazi yao kubwa ni kuangalia usalama wa raia na mali zao, katika eneo hilo ikiwemo kukamata magendo.
Tatizo pale wanapofanya kazi ya utrafiki.
Jiulize, huyo polisi akikumata ukamwambia wewe siyo trafiki, akakubali, akakwambia twende kituoni ukaonane na trafiki, na una makosa kibao, je utaenda au utatoa rushwa? Mfano, ukienda kuonana na trafiki utalipa faini elfu 90, huyo jamaa anataka ten! Rushwa ina faida na hasara.

Wanakaguwa usalama,nadhani ni jambo jema.Kumezuka mtindo askari waliovaa mavazi kama ya FFU combat za kijani kukamata magari kwa visingizio mbalimbali.
Wengi pia hukamata waendesha boda boda na kuwakung'uta mifuko yaani kuwapiga mkwara watoe rushwa. Pichani askari wawili wa aina hiyo wakiwa wanazunguka zunguka kutafuta wateja maungio ya barabara inayotoka Karume na inayotoka Veta Chang'ombe.
Ukivuka tu reli kama umetoka ile barabara inayotoka Ilala, Karume ikapita Machinga Complex kukutana na Nyerere Road.
Ni mara nyingi hawa askari huwa wanapita wakiwa na silaha kutafuta tafuta watu wa kuwapiga mkwara na kupewa rushwa.
Tabia hii naomba niulize kwa mamlaka je hawa FFU pia hufanya kazi za traffic? Maana mara nyingi nimewakuta hata wakisimamisha magari na kukagua. Lakini cha kujiuliza hawana hata zile mashine za kutoa risiti wakilipwa pesa.
Je hawa wamehalalishwa kufanya haya wayafanyayo? Ni nani anapasea kukamata raia kwa makosa ya vyombo vya usafiri au madereva barabarani?
View attachment 1257944
View attachment 1257945
Wanajua sana na wamefundishwa hivyo, sema ndo mambo yanaenda hovyobovyo tu, na wao wanakukamata ili kupata chochote na ndo mana wanakusimamisha kwa mkwara.Lakini askari anapomsimamisha mtu anatakiwa kumpa sababu za kumzuia,
Lakini wengi ama hawajaelimishwa juu ya hilo, wengine huwa wahawajulishi wananchi sababu za kuwasimamisha au kuwazuia ,
Na mwananchi anapouliza imekuwaje askari anachukia na kumwambia usinihoji [emoji15][emoji15]
Kwanini kusiwepo na mawasiliano kati ya askari na mwananchi?
Kwani mwananchi ni mtuhumiwa? Hata mtuhumiwa anazo haki zake vivyo hivyo hata mfungwa anazo haki zake!
Wote Wanaruhusiwa Kufanya Kazi, Shida Ipo Kwenye Kuomba Kiwi
mkuu kama sheria inampa mamlaka askari kukusimamisha na kukuhoji,ni ukichaa kuuliza anakusimamishia kitu gani.ndio maana jibu huja USIHOJI.Lakini askari anapomsimamisha mtu anatakiwa kumpa sababu za kumzuia,
Lakini wengi ama hawajaelimishwa juu ya hilo, wengine huwa wahawajulishi wananchi sababu za kuwasimamisha au kuwazuia ,
Na mwananchi anapouliza imekuwaje askari anachukia na kumwambia usinihoji [emoji15][emoji15]
Kwanini kusiwepo na mawasiliano kati ya askari na mwananchi?
Kwani mwananchi ni mtuhumiwa? Hata mtuhumiwa anazo haki zake vivyo hivyo hata mfungwa anazo haki zake!
muongozo upo kwenye katiba yao ya majukumu.huwezi kuikuta kwenye sheria za kwaida maana zinawatambua kama wote ni polisi wa chuo cha polisi moshi,ila kitabu chao cha ndani ndio kinagawa majukumu.Lete muongozo unaosema wote wanaruhusiwa kufanya kazi za usalama barabarani tuone.
muongozo upo kwenye katiba yao ya majukumu.huwezi kuikuta kwenye sheria za kwaida maana zinawatambua kama wote ni polisi wa chuo cha polisi moshi,ila kitabu chao cha ndani ndio kinagawa majukumu.
sasa shikwa na FFU jitetee,mwambie wewe sio traffic uone kama utashinda hiyo case.