Polisi Dodoma: Daktari toka hospitali ya Milembe athibitisha kuwa nabii Tito ana tatizo la akili

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
WhatsApp Image 2018-01-23 at 16.52.00.jpeg

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema daktari wa Hospitali ya Milembe mkoani humo amethibitisha kuwa Tito Machibya maarufu kwa jina la Nabii Tito ana tatizo la akili.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 23, mwaka 2018 baada ya kumkamata nabii huyo, Muroto amesema baada ya kumkamata leo wataendelea kumshikilia kwa ajili ya usalama wake kwa kuwa anajenga chuki dhidi ya dini za watu wengine wenye imani tofauti.

Amesema Nabii Tito alikamatwa na Polisi Januari 16, baada ya kuhojiwa alionekana kuwa na tatizo la akili na kuamua kumpeleka katika hospitali hiyo ya wagonjwa wa akili.

Amebainisha kuwa alipofanyiwa uchunguzi na daktari aliyemtaja kwa jina moja la Philipo alibaini kuwa nabii huyo ana tatizo hilo.

Nabii huyo amekuwa akionekana mitaani akihubiri huku akiwa anakunywa pombe.



Chanzo; Mwananchi

Soma zaidi hapa: Dodoma: Serikali kumshughulikia anayejiita Nabii Tito. Afika Kituo Kikuu cha Polisi kwa mahojiano
 
Wasitulishe pumba maswali madogo tu tunaitaji majibu Kama ni chizi
Je pesa ya mvinyo anapata wapi?
Je yale madhari ya clip tunazoziona huandaa nani?
Je nani husambaza clip tunazoziona?
Wasitupe majibu mepesi Kwa maswali magumu au kisa machibya msukuma ebu waache usanii
 
nilijua tu huyu jamaa si mzima

Kwa sababu afande kasema? huyu jamaa hata ukimsikiliza unaona kabisa ana kaili timamu, sema ameona hiyo ndio namna yake ya kupata umaarufu na kuweza kutoka... hiyo ya kusema hana akili na kumshikiria ni kiki tu..
 
Sasa kama ni chizi polisi wanamshikilia ili nini?

Mbona machizi kibao mtaani hawawashikilii??
walipomshika hawakua wakijua kama ni mgonjwa mpaka dokta alipothibitisha,lakini pia baada ya kuthibitisha wametoa sababu kwa usalama wake watamshikilia ila nadhani baadae watamwachia ama kupewa medical assistance mirembe
 
Back
Top Bottom