Polisi, Chadema ‘wavurugana’ Arusha ... CUF Hawakuvurugana na Polisi walipokewa AIRPORT ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi, Chadema ‘wavurugana’ Arusha ... CUF Hawakuvurugana na Polisi walipokewa AIRPORT ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 10, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 10 October 2012 05:01[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]


  Waandishi Wetu, Arusha na Dodoma

  JIJI la Arusha jana lilikuwa na hekaheka inayofanana na sinema baina ya polisi na wafuasi wa Chadema baada ya askari hao kumkamata mgombea wa udiwani wa Kata ya Daraja Mbili kupitia chama hicho, Prosper Msofe (44).

  Hali hiyo ilitokea baada ya kiongozi huyo kukamatwa akiwa katika hali mbaya na kulazwa rumande, kisha asubuhi yake kupelekwa katika zahanati ya polisi, kabla ya kumpeleka mahakamani na kurudishwa hospitali.

  Mgombea huyo, kabla ya kupelekwa Mahakama ya Mwanzo, Maromboso, aliandikiwa cheti na Ofisa wa Afya wa Zahanati na polisi ili aende kuchunguzwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kutokana na maumivu ya uti wa mgongo alioeleza kuwa aliumizwa kwa kupigwa na polisi.

  Hata hivyo, wakati mgombea huyo akiagana na viongozi kadhaa wa Chadema na wafuasi katika zahanati hiyo saa nne asubuhi akiwaeleza kuwa anapelekwa Hospitali ya Mount Meru, polisi walimpandisha kwenye gari lao na kumpeleka katika Mahakama ya Maromboso na kumwacha mahabusu kisha kuondoka.

  Baada ya kufikishwa mahakamani hapo, viongozi wa Chadema na wafuasi wao waliokuwa wanaongozwa na Katibu wa chama hicho, Wilaya ya Arusha, Martin Sarungi na aliyekuwa Mbunge wa Arusha, Gobless Lema walifika kufuatilia tukio hilo wakihoji mgombea huyo, kupelekwa mahakamani badala ya hospitali.

  Hata hivyo, baada ya majadiliano baina ya maofisa wa mahakama, walisitisha kumsomea mashtaka mgombea huyo na kuwataka polisi wampeleke hospitali. Polisi hao walikubali na kumpakiza kwenye gari lenye ulinzi mkali na kumpeleka Hospitali ya Mount Meru.

  Baada ya mtuhumiwa huyo kufikishwa hospitalini hapo, alichukuliwa maelezo na baadaye kulazwa katika wodi namba moja ya wagonjwa majeruhi na hadi jana mchana alikuwa akipata matibabu.

  Chanzo cha kukamatwa

  Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas akizungumzia tukio hilo alisema juzi saa 2:30 usiku, walipata taarifa za mtu mmoja kufanya shambulio la kawaida dhidi ya Ramadhani Kalamba aliyepewa tenda ya kuwaondoa wafayabiashara wadogo katikati ya mji.

  Alisema tukio hilo lilitokea eneo la Friends Corner na baada ya polisi kupata taarifa hiyo, walielezwa na Kalamba kuwa aliyemshambulia ni Prosper Msofe na ndipo alikamatwa na kufikishwa Kituo Kikuu cha Polisi.

  "Baada ya jana kumkamata, tulimwambia atafute mdhamini, lakini aligoma na ndiyo sababu alilala hadi leo (jana) asubuhi na tukampeleka mahakamani," alisema Sabas.

  Hata hivyo, alisema polisi walikuwa hawana taarifa kama alikuwa ameumia na ndiyo maana walimpeleka mahakamani.

  Taarifa ya polisi yapingwa

  Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha, Martin Sarungi alisema baada ya kutoka kwenye kampeni, walipata taarifa kuwa mgombea wao, amekamatwa na walifika polisi kumwekea dhamana, lakini polisi waligoma.

  Sarungi alisema baada ya polisi kugoma kutoa dhamana walilazimika kurejea asubuhi siku iliyofuata na ndipo mgombea wao alieleza kuwa alipigwa akiwa mikononi mwa polisi huku akiwa anaumwa, lakini wakashangaa anapelekwa mahakamani.

  Akizungumzia chanzo cha mkasa huo, alisema mara baada ya mgombea huyo kutoka kwenye kampeni alikwenda benki kuchukua fedha na alikutana na Kalamba akiwakamata kina mama wanaouza mbogamboga kando ya barabara.

  "Mgombea alimuuliza Kalamba kwa nini ananyanyasa kinamama tena usiku na bidhaa hizo anapeleka wapi muda huo, ndipo malumbano yalianza na baadaye Kalamba kuita polisi akidai kupigwa," alisema Sarungi.

  Kada wa CCM aliyepigwa aeleza

  Kwa upande wake, Kalamba ambaye ni kada maarufu wa CCM mjini Arusha, alisema alipigwa ngumi kifuani na mgombea huyo wakati akimzuia kuwaondoa wafanyabiashara hao.

  "Baada ya kunipiga niliita polisi wakamkamata na mimi nikamfungulia kesi namba AR/RB/12648/2002 ya shambulio la kawaida,” alisema Kalamba ambaye jana alikuwa akiendelea na kazi kama kawaida katika maeneo ya Jiji la Arusha.

  Tukio hili limekuja siku moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, kuwaonya wanasiasa kuacha vurugu katika kampeni za uchaguzi huo mdogo na kuwataka polisi kuwachukulia hatua kwa kuvunja sheria.

  Vurugu Dodoma

  Mjini Dodoma, kumezuka vurugu kati ya wafuasi wanaodaiwa kuwa ni wa CCM na Chadema na kujeruhi wanachama watano wa chama tawala wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Msalato.

  Uchaguzi huo mdogo unafanyika baada ya kiti cha udiwani wa kata hiyo kuwa wazi kutokana na kifo cha aliyekuwa diwani wake, George Hoya aliyefariki mwanzoni mwa mwaka huu.

  Vurugu hizo zilizuka baada ya wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CCM kuzuia msafara wa pikipiki wa wafuasi wa Chadema na hata kumjeruhi mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, Danson Kaijage.

  Mwandishi huyo amesharipoti tukio la kupigwa kwake katika Kituo cha Polisi cha Kati na kufunguliwa jalada lenye namba Dom/RB/10951/2012.

  Chanzo cha habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, mkoani hapa kilisema miongoni mwa watu waliojeruhiwa katika vurugu hizo ni Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Ali Swaleh ambaye bado amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma akipatiwa matibabu.

  Wengine ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa chama hicho Wilaya ya Dodoma Mjini, Fatma Muhidini, Diwani wa Kata ya Uhuru, Ali Kimaro, Hussein Mtengule na Waziri Shaaban.

  Hata hivyo, hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Zelothe Stephen hakupatikana jana kwani ilielezwa kuwa yuko safari na atatoa taarifa kwa waandishi wa habari mara tu atakaporudi.

  Wakati ikielezwa CCM ndiyo chanzo, Katibu wa CCM wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Saad Kusilawe alisema tukio hilo lilitokea saa 8.30 mchana wakati wanachama wa Chadema walipouvamia msafara wa CCM na kuanza kuwashambulia wanachama kwa mawe na silaha nyingine.

  Alibainisha kuwa, kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi, CCM walipangiwa kufanya mkutano wao wa uzinduzi wa kampeni katika eneo la Gulioni Msalato wakati Chadema walitakiwa kufanya mkutano wao katika eneo la Msalato Bible umbali wa Kilometa mbili kutoka eneo walilopangiwa CCM.

  Imeandikwa na Mussa Juma (Arusha) na Masoud Masasi (Dodoma).
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]   
 2. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Yana mwisho chadema be strong.

  Hawa polisi watakuja piga magoti wakiomba msamaha only time will tell.

  hawawezi kumshughulikia mke wa boss wao.
   
 3. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,655
  Likes Received: 3,308
  Trophy Points: 280
  Ccm watarukaruka sana mwishowe wataanguka,hata hivyo sasa imezoeleka kwa mwathirika kubebeshwa hatia,hasa kama ataonekana na viji element vya u-chadema,ambavyo ni pamoja na tabia ya kudai haki stahili za jamii,hilo ni kosa kubwa sana mbele ya govt ya ccm na vibaraka wake wakiwemo polisi na migambo na vikosi vingine vya siri kama hicho cha rama kalamba,hata hivyo!mwisho wa uongo ni ukweli,wanajua kabisa kuwa hawawezi kuipata Daraja 2,hasa baada ya mtu pekee aliyeweza kupeperusha bendera yao na kuaminika yaani marehema Msangi(Rip)kuondoka,aibu waliyopata kwenye mkutano wao pale lamlawa imewatia kichaa,na sasa wapo tayari kuua,wakiongozwa na huyo kalamba,ambaye historia yake ni chafu hapa mjini,alishaleta jeuri kama hiyo 2010 kwenye kampeni sokon 1 ila akadhibitiwa vilivyo na vijana wa Kivuyo,akahama mtaa kwa muda,ila kwa sasa Hatakaa kwa Amani TENA.
   
 4. m

  malaka JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nadhan wale Green guard waliokuwa kambini wameshasambazwa tayari.
   
Loading...