kunena
JF-Expert Member
- Nov 29, 2016
- 506
- 717
Wenyeviti hao ni wa mitaa iliyopo Burka jijini Arusha. Lengo lao ni kuvamia ardhi mpakani mwa jiji hilo na wilaya ya Arumeru. Polisi iliwakamata eneo la tukio na kuwaweka lupango tangu jana hadi leo asubuhi walipotoka kwa dhamana. Diwani wa kata ya Burka-chadema alithibitisha uhalifu huo na kukiri hali hiyo.
Baada ya kutoka mahabusu Wenyeviti hao walielekea ofisi za Jiji na kufanya kikao cha faragha kilichowahusisha baadhi ya madiwani na meya wa jiji ajenda ikiwa ni namna ya kujinusuru na aibu hiyo. Hata hivyo baada ya kikao hicho meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro alisema suala hili limepelekwa ofisi ya mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani Kihamia ili alisimamie lifikie mwisho.
Wenyeviti hao walilalamika kuwa walipokamatwa taarifa zilimfikia mkurugenzi huyo wa jiji la Arusha kupitia diwani wa kata ya Burka ili asaidie kuwatoa wasilale polisi lkn alijibu kuwa hakuna kikao cha jiji kilichowatuma Wenyeviti hao kuvamia maeneo ya wazi hivyo sheria iachwe ichukue nafasi yake. wananchi zaidi ya 45 walifika ofisini kwa mkurugenzi wa jiji kulalamikia jinsi Wenyeviti hao wanavyokiuka maadili ya uongozi ingawa hawakumkuta mkurugenzi huyo ambaye ilielezwa na afisa tawala Frank Sanga kuwa mkuruogenzi alielekea katika ukaguzi wa shule za Msingi zinazojengwa madarasa mapya.
HITIMISHO:
Wenyeviti hawa waache kufanya kazi kwa mazoea kwani enzi za ubabaishaji zimekwisha Watafute kazi za halali za kufanya sio kuvamia maeneo ya wazi kwa lengo la kuyauza.
POLISI IACHWE IFANYE KAZI YAKE