Polisi Arusha yamsaka Mfungwa aliyekimbia hukumu

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Jeshi la polisi mkoani Arusha linamsaka mwanamke anahefahamika kwa jina la Oliver Yasent ambaye ni mfungwa kisheria aliyehukumiwa na mahakama lakini hakutumikia kifungo chake..

Oliver Yassenti,mkazi wa Mto wa mbu ,mkoani Arusha anatuhumiwa kukimbia kifungo baada ya kuhukumiwa kutumikia kifungo cha miezi 12 jela kwa kosa la wizi.

Kamanda Shanna alidai kwamba Oliver alifanikiwa kutoroka baada ya kuwekewa dhamana na kwamba kesi hiyo iliendeshwa bila yeye kuwepo mahakamani na baadaye hukumu ilitolewa na kutiwa hatiani.

Kamanda Shanna alidai kwamba Oliver alihukumiwa , desemba 20,2019 baada ya mahakama ya mwanzo MTO wa Mbu kumtia hatiani kwa kosa la kuiba mataili ya mwajiri wake Deepyen Barneda yenye thamani ya shilingi 2,400,000.

IMG_20200512_123021.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom