Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,016
- 9,885
Hii ni ishara mbaya sana, ni dalili za nchi kukosa uelekeo.Tanzania sasa hivi polisi wanaua watu kadri wanavyojisikia halafu wanakupa kesi ya ujambazi
Yaani haya maigizo ni yakizamani sana,kwa hiyo myuhumiwa walikuwa wamemwachia na hakufungwa pingu?Mauaji ya majambazi kwa nini yasiidhinishwe na bunge ili kuwakolea polisi muda wa kurudia maneno haya
"Tuliandaa mtego na kumuachia kuonyesha wenzake lakini alianza kukimbia eneo la kwa Idd na kutoa ishara kuwa kuna polisi eneo hilo ndipo wenzake walianza kufyatua risasi na wawili waliuawa na wengine kutoweka"
Mkuu kwa majambazi sawa sawa tuTanzania sasa hivi polisi wanaua watu kadri wanavyojisikia halafu wanakupa kesi ya ujambazi.
YANI HAWANA MBINU MPYA HAWA JAMAA AU NI MBINU YA KUTULIZA MASWALI WAKATI WALIUA BILA HATA HUJUA MHALIFU NA ASIYE MHALIFU, FIKIRIA LABDA YAMEMTEKA DEREVA WA TEKSI SI NA YEYE ANAUWAWA TUMauaji ya majambazi kwa nini yasiidhinishwe na bunge ili kuwakolea polisi muda wa kurudia maneno haya
"Tuliandaa mtego na kumuachia kuonyesha wenzake lakini alianza kukimbia eneo la kwa Idd na kutoa ishara kuwa kuna polisi eneo hilo ndipo wenzake walianza kufyatua risasi na wawili waliuawa na wengine kutoweka"
Wewe utakuwa mmoja wao majambazi, kama sio wewe basi ndugu yakoYaani haya maigizo ni yakizamani sana,kwa hiyo myuhumiwa walikuwa wamemwachia na hakufungwa pingu?
Eti mtuhumiwa aliwahashiria majambazi wenzake warushe risasiYaani haya maigizo ni yakizamani sana,kwa hiyo myuhumiwa walikuwa wamemwachia na hakufungwa pingu?
Hivi hawana mwandishi wa script mpya?Watu wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa na polisi mkoani Arusha.
Tukio hilo limetokea katika eneo la Sakina Idd mjini humo ikielezwa kuwa kabla ya kukutwa na mauti yalitokea majibizano ya risasi.
Akizungumza leo Alhamisi Desemba 24, 2020 kamanda wa polisi mkoani humo, Salum Hamduni amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo saa 7:10 usiku.
Amesema watuhumiwa ni Joseph Bernard (24) mkazi wa Sokoni One na mwingine ambaye hajafahamika anakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 30-34.
Amesema awali polisi walimkamata mtuhumiwa mmoja, Bernard aliyekiri kujihusisha na uhalifu na siku hiyo walipanga kuvamia duka na akakubali kwenda kuwaonyesha wenzake.
"Tuliandaa mtego na kumuachia kuonyesha wenzake lakini alianza kukimbia eneo la kwa Idd na kutoa ishara kuwa kuna polisi eneo hilo ndipo wenzake walianza kufyatua risasi na wawili waliuawa na wengine kutoweka," amesema
Amesema eneo la tukio zimekamatwa bastola mbili aina ya Browing zikiwa na risasi tisa na maganda matatu ya bunduki aina ya Shotgun na maganda sita ya bastola.
Amesema msako unaendelea kuwakamata waliokimbia, miili ya waliokufa imehifadhiwa hospitali ya rufaa ya Mountmeru.