Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,000
- 9,861
Watu wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa na polisi mkoani Arusha.
Tukio hilo limetokea katika eneo la Sakina Idd mjini humo ikielezwa kuwa kabla ya kukutwa na mauti yalitokea majibizano ya risasi.
Akizungumza leo Alhamisi Desemba 24, 2020 kamanda wa polisi mkoani humo, Salum Hamduni amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo saa 7:10 usiku.
Amesema watuhumiwa ni Joseph Bernard (24) mkazi wa Sokoni One na mwingine ambaye hajafahamika anakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 30-34.
Amesema awali polisi walimkamata mtuhumiwa mmoja, Bernard aliyekiri kujihusisha na uhalifu na siku hiyo walipanga kuvamia duka na akakubali kwenda kuwaonyesha wenzake.
"Tuliandaa mtego na kumuachia kuonyesha wenzake lakini alianza kukimbia eneo la kwa Idd na kutoa ishara kuwa kuna polisi eneo hilo ndipo wenzake walianza kufyatua risasi na wawili waliuawa na wengine kutoweka," amesema
Amesema eneo la tukio zimekamatwa bastola mbili aina ya Browing zikiwa na risasi tisa na maganda matatu ya bunduki aina ya Shotgun na maganda sita ya bastola.
Amesema msako unaendelea kuwakamata waliokimbia, miili ya waliokufa imehifadhiwa hospitali ya rufaa ya Mountmeru.