Polisi Arusha waua wawili wakidai ni majambazi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,645
2,000
Watu wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa na polisi mkoani Arusha.

Tukio hilo limetokea katika eneo la Sakina Idd mjini humo ikielezwa kuwa kabla ya kukutwa na mauti yalitokea majibizano ya risasi.

Akizungumza leo Alhamisi Desemba 24, 2020 kamanda wa polisi mkoani humo, Salum Hamduni amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo saa 7:10 usiku.

Amesema watuhumiwa ni Joseph Bernard (24) mkazi wa Sokoni One na mwingine ambaye hajafahamika anakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 30-34.

Amesema awali polisi walimkamata mtuhumiwa mmoja, Bernard aliyekiri kujihusisha na uhalifu na siku hiyo walipanga kuvamia duka na akakubali kwenda kuwaonyesha wenzake.

"Tuliandaa mtego na kumuachia kuonyesha wenzake lakini alianza kukimbia eneo la kwa Idd na kutoa ishara kuwa kuna polisi eneo hilo ndipo wenzake walianza kufyatua risasi na wawili waliuawa na wengine kutoweka," amesema

Amesema eneo la tukio zimekamatwa bastola mbili aina ya Browing zikiwa na risasi tisa na maganda matatu ya bunduki aina ya Shotgun na maganda sita ya bastola.

Amesema msako unaendelea kuwakamata waliokimbia, miili ya waliokufa imehifadhiwa hospitali ya rufaa ya Mountmeru.
 
KISIWAGA

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
3,432
2,000
Mauaji ya majambazi kwa nini yasiidhinishwe na bunge ili kuwakolea polisi muda wa kurudia maneno haya

"Tuliandaa mtego na kumuachia kuonyesha wenzake lakini alianza kukimbia eneo la kwa Idd na kutoa ishara kuwa kuna polisi eneo hilo ndipo wenzake walianza kufyatua risasi na wawili waliuawa na wengine kutoweka"
 
vvm

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
4,246
2,000
Ifike hatua polisi wetu wa vikosi maalumu vya kupambana na majambazi wawe wanafungiwa camera (body Cam) ili maelezo yakwamba tuliweke mitego yasihitajike sana yaani tujionee kwa macho
 
Tarakwa

JF-Expert Member
Apr 19, 2017
828
1,000
Natamani na Hawa vijana wana wanaozurura na kutukana hovyo, kukaba watu na kulewa asubuhi, wakamatwe wakapasue mawe kwenye miradi ya ujenzi mishahara yao iwe ugali bila mboga
 
mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
4,615
2,000
Mauaji ya majambazi kwa nini yasiidhinishwe na bunge ili kuwakolea polisi muda wa kurudia maneno haya

"Tuliandaa mtego na kumuachia kuonyesha wenzake lakini alianza kukimbia eneo la kwa Idd na kutoa ishara kuwa kuna polisi eneo hilo ndipo wenzake walianza kufyatua risasi na wawili waliuawa na wengine kutoweka"
Yaani haya maigizo ni yakizamani sana,kwa hiyo myuhumiwa walikuwa wamemwachia na hakufungwa pingu?
 
Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,107
2,000
Mara nyingi ni askari wa chini (Wapelelezi) ndio wanao waangusha ma RPC na kuonekana hawajui kazi zao.

RPC huwa ana deal na operation kubwa kubwa za ki-mkoa, askari wachini (Wapelelezi) huwa wakati mwingine operation unakuta ni ndogo ila wanataka kuzikuza au hawana utaalamu wa operation hizo na mwisho wana haribu.

Binafsi, si walaumu askari kuwaua majambazi wanaotumia silaha za moto kufanya matukio, kwasababu;

1) Huwa majambazi wanaotumia silaha hawana huruma kwa raia pindi wanapokua kikazi.

2) Roho ya ubinaadamu huwa imewatoweka.

3) Asili huwa hawaiachi, hata wakikamatwa mwisho wa siku wakifungwa (Au wakihonga na kutolewa) then wakitoka gerezani wanarudi kwenye asili ya kazi zao.

#NB Katika RPC ambaye ni mtendaji kazi kikweli kweli ni huyu RPC Salumu wa Arusha, hanaga kutafuta kiki/kujimwambafai/kujionesha onesha/press zake anaongea kwa umakini wa hali ya juu na huwa anaweka akiba ya maneno halafu ana "SURA YA KAZI (DANGEROUS COLD FACE = sura ya upole wa Kutisha kweli kweli kwa anaejua makamanda)" ila wahalifu wakiingia kwenye "TISINI ZAKE" huwa wanaisoma namba kikweli kweli dadeki, akikudaka una mawili uchezee shaba ufe au uwakamatishe wenzako ili usalimike.

Njombe aliisafisha kwenye yale mauwaji ya albino kwa mwezi mmoja tu mpaka leo kimya (Kama walikumbwa na tsunami). Nchi yetu ingekua na makamanda kama hao 5 tu basi wahalifu wangeipata kisawasawa na jeshi lingekua vizuri sana.

Ila RPC wa dodoma na Kanda Maalum Ya Dar Es Salaam hawana utaalamu wala weredi kabisa wa kijeshi. Kazi zao ni kutafuta vyeo kwa KIKI NA KUJIONESHA kwa kutumia vyombo vya habari na sinema za bongo movie. Hata sura zao wahalifu naamini wakiziona wanacheka kwa vituko wanavyofanya kwenye press.
 
Donnie Charlie

JF-Expert Member
Sep 16, 2009
10,341
2,000
Mauaji ya majambazi kwa nini yasiidhinishwe na bunge ili kuwakolea polisi muda wa kurudia maneno haya

"Tuliandaa mtego na kumuachia kuonyesha wenzake lakini alianza kukimbia eneo la kwa Idd na kutoa ishara kuwa kuna polisi eneo hilo ndipo wenzake walianza kufyatua risasi na wawili waliuawa na wengine kutoweka"
YANI HAWANA MBINU MPYA HAWA JAMAA AU NI MBINU YA KUTULIZA MASWALI WAKATI WALIUA BILA HATA HUJUA MHALIFU NA ASIYE MHALIFU, FIKIRIA LABDA YAMEMTEKA DEREVA WA TEKSI SI NA YEYE ANAUWAWA TU
 
Albinoomweusi

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
2,825
2,000
Watu wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa na polisi mkoani Arusha.

Tukio hilo limetokea katika eneo la Sakina Idd mjini humo ikielezwa kuwa kabla ya kukutwa na mauti yalitokea majibizano ya risasi.

Akizungumza leo Alhamisi Desemba 24, 2020 kamanda wa polisi mkoani humo, Salum Hamduni amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo saa 7:10 usiku.

Amesema watuhumiwa ni Joseph Bernard (24) mkazi wa Sokoni One na mwingine ambaye hajafahamika anakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 30-34.

Amesema awali polisi walimkamata mtuhumiwa mmoja, Bernard aliyekiri kujihusisha na uhalifu na siku hiyo walipanga kuvamia duka na akakubali kwenda kuwaonyesha wenzake.

"Tuliandaa mtego na kumuachia kuonyesha wenzake lakini alianza kukimbia eneo la kwa Idd na kutoa ishara kuwa kuna polisi eneo hilo ndipo wenzake walianza kufyatua risasi na wawili waliuawa na wengine kutoweka," amesema

Amesema eneo la tukio zimekamatwa bastola mbili aina ya Browing zikiwa na risasi tisa na maganda matatu ya bunduki aina ya Shotgun na maganda sita ya bastola.

Amesema msako unaendelea kuwakamata waliokimbia, miili ya waliokufa imehifadhiwa hospitali ya rufaa ya Mountmeru.
Hivi hawana mwandishi wa script mpya?
 
Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
15,453
2,000
Kama ni majambazi kweli sijawahi kuwaonea huruma hao jamaa,ila kama ndiyo story zilezile za kubambikiana....itakuwa jambo baya sana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom